Wizara ya Kilimo kimya: Mahindi Kusini, bei imeporomoka, soko limedoda na msimu wa mvua unakaribia

Nahisi wewe unachelewa kuielewa serikali yako:

2.mwaka huu hakuna chakula cha msaada lakini walikitoa japo mwishoni watu wanaelekea kuvuna( ni wajibu wa serikali kutoa chakula pale mkulima anapokumwa na sababu zilizoko nje ya uwezo wake mfano ukame/mafuriko.

3.pia ni jukumu la serikali kuhakikisha mkulima wanaemuhamasisha kulima anauza kwa bei ya faida kupitia vyama vya ushirika kama wanavyofanya kwenye korosho kwamba ukikamatwa na korosho ambazo hazikununuliwa katika mfumo uliowekwa zinataifishwa.

Serikali yako haina muda na mwananchi, si chakula tu ni kwa huduma zote ndo maana inafurahi pale mkulima anapouza kwa bei ya hasara na maajabu zaidi pamoja na kuwa na bei ndogo wanaendelea kuruhusu mengine toka nchi jirani.
Mkuu baadhi nakubaliana na wewe. Tupe ushauri,ni nini kifanyike na je Wizara ya Kilimo haina nafasi kabisa kusaidia kuondoa adha ya bei ndogo ya mazao?
 
Mkuu baadhi nakubaliana na wewe. Tupe ushauri,ni nini kifanyike na je Wizara ya Kilimo haina nafasi kabisa kusaidia kuondoa adha ya bei ndogo ya mazao?
Wizara yetu inajukumu kubwa sana kusimamia hili suala.

Tatizo linalotukuta ni kwamba wizara zetu hazifanyi kazi kutokana na taaluma bali wanasiasa wanataka nini na kwa wakati gani ili na wao walioteuliwa waendelee kukaa madarakani mkono upate kwenda kinywani!

Ndo maana inashindwa hata kuweka uhusiano mzuri baina ya mkulima na (vyuo vya kilimo, taasisi za utafiti, mashirika ya kilimo/wahisani na masoko ya ndani na nje ya nchi) kilichobaki ni kusikiliza rais na waziri mkuu wanataka nini na siyo mpango mkakati wa kilimo unasemaje ili kumunusuru mwananchi.

Hadi siku siasa ikifa mambo yatakuwa mazuri.
 
Mkuu "SIASA NI KILIMO" unaikumbuka? Labda ndo mwendelezo wake. Sipingani sana na wewe,ila nini zaidi kifanyike?
 
upload_2017-9-19_8-47-49.png
 
Waziri wetu wa Kilimo ninamjua ni mchapakazi. Alipita nchi nzima kuhamasisha wakulima walime kukabiliana na baa la upungufu wa chakula ulioashiria mwanzoni. Pia ilitangazwa,asiyelima,hakuna msaada wa chakula toka mamlakani. Matokeo,Kusini mwa Tanzania,hasa Ruvuma,Mbeya,Rukwa nk,wamefanikiwa kuvuna mahindi mengi. Soko lake linasuasua sana. Bei ni ndogo,siyo ya motisha. Wengi wameamua kuhifadhi hadi bei iwe nzuri. Haijajulikana bei itabadilika lini na kwa msukumo upi! Baadhi ya wakulima hawana maghala imara,pia uharibifu wa wadudu umeanza kwa kasi. Mvua nazo zinakaribia watu waanze msimu mwingine. Nini msukumo wa Wizara kuona soko lenye bei ya motisha linapatikana? Kimya kimekuwa kingi,yawezekana tafsiri ya PM kuwa mahindi yasindikwe,bado haijaeleweka kwa Wakulima. Huenda wanasubiri ufafanuzi zaidi kutoka Wizara yenye dhamana na mazao?
kwa hiyo ulitaka bei ya vyakula ipande.
 
Mkuu "SIASA NI KILIMO" unaikumbuka? Labda ndo mwendelezo wake. Sipingani sana na wewe,ila nini zaidi kifanyike?
Tulioshikilia makali hatuna cha kufanya tunasubiri walioshika mpini siku wakiona umuhimu wetu.
 
kwa hiyo ulitaka bei ya vyakula ipande.
Kama inputs(mbolea,diesel,trekta na vipuli vyake,ukodishaji ardhi,madawa,mbegu,human manpower nk) viko juu na vinaendelea kupanda uncotrolled,kwa nini soko la mazao liwe controlled . Umewahi kulima hata mara moja ukajua bei ya mbegu bora za mahindi ni kiasi gani? Ndugu,fanya utafiti kidogo,utanipa majibu mazuri.
 
hujajibu swali unataka bei za vyakula ziwe juu nchini ?
 
hujajibu swali unataka bei za vyakula ziwe juu nchini ?
Swali lako ni linganifu (comparative),halina mwelekeo. Ukisema ziwe juu unalinganisha na zipi?na kwa eneo gani? Soma thread vizuri. Thread iko specific na imetaja maeneo.
 
Kama inputs(mbolea,diesel,trekta na vipuli vyake,ukodishaji ardhi,madawa,mbegu,human manpower nk) viko juu na vinaendelea kupanda uncotrolled,kwa nini soko la mazao liwe controlled . Umewahi kulima hata mara moja ukajua bei ya mbegu bora za mahindi ni kiasi gani? Ndugu,fanya utafiti kidogo,utanipa majibu mazuri.
Usipoteze muda wako kujadiliana na MTU ambaye hajui hata mbegu znauzwa wapi?wa kwanza kuamka wa mwsho kulala...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani nilazima wayauze? Waweke hifadhi ya chakula njaa inaua watafute zao lingine la biashara. Hakuna chakula kutoka serikalini ebo
Ghala la taifa wawezeshwe kununua,kuhifadhi maghala kila mkoa na kuuza kwa wingi kote nchini kupunguza mfumko wa bei.Tukiweza control chakula sisi ni matajiri,tunaweza.
 
Back
Top Bottom