Wizara ya Kilimo kimya: Mahindi Kusini, bei imeporomoka, soko limedoda na msimu wa mvua unakaribia

Hujui hata unaongea nini. Kukiwa na ukame watu lazima waseme. Chakula kikizidi kikawa kinaharibika kisha ukazuia watu kuuza nje ni lazima waseme. Kama serekali inataka kuwa na chakula cha kudhibiti njaa nchini wawawezeshe majeshi kama magereza na JWTZ walime hicho chakula cha njaa kwani sasa hivi nchi haipo vitani. Ni rahisi jeshi kupewa matractor na combine havestor wazalishe kwa wingi. Halafu sisi wananchi tunaolima kwa mitaji yetu tuachiwe tuuze tunakojua. Kinyume na hapo ni uonevu wa wazi kwa wakulima.
mlisema kuna ukame nakutakua na njaa, hata miezi sits haijaisha mnaanza tens kulia chakula kingi ,
 
Falsafa ya chakula ndiyo kipimo cha mkuu wa INCHI au Kaya.
Yusufu aliyekuwa Waziri Mkuu wa MISRI enzi za Mfalme Farao anaheshima hadi sasa kwa sababu alikusanya chakula wakati wa shibe na baadaye kuwauzia watu wake wakati wa njaa.
Inchi yetu imesahau vipao mbele vyake ambayo tumekuwa tukivinukuu kila siku toka Uhuru hasa wakati wa NYERERE.
Mahitaji muhimu ya binadamu ni.
1. Chakula
2. Mahala pa kulala
3. Mavazi
Rais Mwinyi aliwahi kusema kila kitabu na zama zake.
Viongozi waliofuata baada ya Nyerere kila moja alikuja na vipao mbele vyake ambavyo haviendani kabisa na vya Nyerere.
Mwalimu Nyerere aliweka vipao mbele hivi kwa sababu alijali utu.
Kazi ya mkulima maskini ni kulima mazao ya chakula. anatakiwa abaki na chakula chake cha kumtosha na akiba auze.
Ni wajibu wa Serikali kumtafutia soko kwa wengi wa wakulima hawana uwezo wa kusafirisha mahindi yao mpaka mijini.
Wale walioruhusiwa na Rais kusafirisha magunia kumi kumi ili kukwepa ushuru ni walanguzi na hawana shamba wala jembe.
Serikali ifanye utaratibu wa kununua chakula chote za ziada toka kwa wakulima maskini na siyo kutoka kwa wafanyabiashara.
 
Una hoja nzuri, lakini bora wakulima wawauzie wafanyabiashara japo wanawalalia bei lakini wanalipa cash. Serekali wanalipa bei elekezi na bado watakulipa siku wanataka. heri 9 nenda(mfanyabiashara) kuliko 10 nenda rudi (serekali)
 
Huu ni upumbafu mkuu....mlikuwa mnasema nchi inanjaa...sasa mnasema mahindi hayana bei...??? Tuwaelewe vipi???
 
Safi sana.
Wakome kuichagua sisiem
Nyie si mlikuwa mnalia kuwa bei ya unga imekuwa juu???? Sasa serikali imezuia mahindi yasiende nje ,bei imeshuka ,mwapiga kelele tena ili yapande!!!!!! kwa sisi wenye familia tunashukuru bei ya mahindi kushuka.Nyie mnaokula kwa mashemeji zenu endelezeni siasa za kipumbafuu.....
Hilo nami nimelisikia. Ila mengi ya Zambia yanakuwa "ontransit" kwenda Kenya na Burundi. Wamepiku maeneo yale Watz walikuwa wakiuza!
 
Nyie si mlikuwa mnalia kuwa bei ya unga imekuwa juu???? Sasa serikali imezuia mahindi yasiende nje ,bei imeshuka ,mwapiga kelele tena ili yapande!!!!!! kwa sisi wenye familia tunashukuru bei ya mahindi kushuka.Nyie mnaokula kwa mashemeji zenu endelezeni siasa za kipumbafuu.....
kwenu imeshuka mpaka ngapi ?
 
Bei ya mahindi imeshuka, wakati huohuo serikli INA ruhusu mahindi toka Zambia yaingie Tanzania sasa hiyo ndo nini kuna mkulima atakaye faidika kweli na sekita hiyo?
Ikumbukwe Mkulima anapokosa soko/ bei nzuri serikali inafurahia kwani chakula kitakuwepo kwa bei nafuu hivyo kila mmoja ataweza kukipata na kupunguza mzigo wa njaa kwa serikali.
 
Mkuu kusema tu bei Ni ndogo bila details Na data Ni jambo lisilokubalika!
Hebu shusha data hapa!
Gunia/ au debe moja bei yake ikoje??
Ukilinganisha Na bei za mwezi kama huu mwaka jana!!
Kuna baadhi ya maeneo mahindi kwa wakati huu Ni dili sana!!
Mfano tanga- muheza

Gunia(debe 6) 36000/= hadi 42000/=

Wakati mwaka jana time kama hii 120000/= kwa gunia( debe 6)
 
Nyie si mlikuwa mnalia kuwa bei ya unga imekuwa juu???? Sasa serikali imezuia mahindi yasiende nje ,bei imeshuka ,mwapiga kelele tena ili yapande!!!!!! kwa sisi wenye familia tunashukuru bei ya mahindi kushuka.Nyie mnaokula kwa mashemeji zenu endelezeni siasa za kipumbafuu.....
unaeza thibitisha nilikuwa nalia bei juu? Nakula kwa shemeji thibitisha hili.

Unafurahia serikali kuwadhurumu wakulima eti bei imeshuka unajua wakulima wanavyotaabika we kenge?
 
Ikumbukwe Mkulima anapokosa soko/ bei nzuri serikali inafurahia kwani chakula kitakuwepo kwa bei nafuu hivyo kila mmoja ataweza kukipata na kupunguza mzigo wa njaa kwa serikali.
Sidhani kama serikali unayosema iko hivyo,kumbuka kauli hizi za viongozi kuhusu njaa.
1. Hapa kazi tu,asiyefanya kazi na asile.
2.Mwaka huu,hakuna chakula cha msaada,serikali haina shamba.
3. Ukiwa na debe moja,usikubali kuuza bei ndogo,ikibidi upewe ngombe 3 kwa debe moja.
Kwa kauli kama hizo,unaweza kuona kuwa, serikali inataka watu wafanye kazi sana(walime) ili wajitegemee kwa chakula,na ziada wauze kwa "bei ya juu".
 
Ikipanda kelele,ikishuka kelele,unga watu wamenunua 2k kelele kila mahal zilizagaa Leo kg shilling 800 bado mnapiga kelele,inatakiwa yashuke mpka kilo iwe jero nyambafuuuuu
Watanzania hatuna jema yani kila kitu lazima watu walalamike bei ikiwa juu vilio ikiwa chini malalamiko mpaka MTU unashindwa kujua yupi mkulima na yupi mlaji wa mwisho khaaa
 
Mfano tanga- muheza

Gunia(debe 6) 36000/= hadi 42000/=

Wakati mwaka jana time kama hii 120000/= kwa gunia( debe 6)
Mkuu utanidanganya kote lkn sio wilaya yoyote ya mkoa wa Tanga Na Mbeya!!
Gunia la mahindi kwa huko Muheza limefikia bei hiyo uliyoitaja mwanzoni mwa mwaka huu mkuu!
Kama nakumbuka Vizuri Ni February hadi April!!
Kuna biashara zangu nyingi huko nakuja sana!
Handeni, Kilindi, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga Na mwisho nachukua nazi Pangani!!
 
Sidhani kama serikali unayosema iko hivyo,kumbuka kauli hizi za viongozi kuhusu njaa.
1. Hapa kazi tu,asiyefanya kazi na asile.
2.Mwaka huu,hakuna chakula cha msaada,serikali haina shamba.
3. Ukiwa na debe moja,usikubali kuuza bei ndogo,ikibidi upewe ngombe 3 kwa debe moja.
Kwa kauli kama hizo,unaweza kuona kuwa, serikali inataka watu wafanye kazi sana(walime) ili wajitegemee kwa chakula,na ziada wauze kwa "bei ya juu".
Nahisi wewe unachelewa kuielewa serikali yako:

2.mwaka huu hakuna chakula cha msaada lakini walikitoa japo mwishoni watu wanaelekea kuvuna( ni wajibu wa serikali kutoa chakula pale mkulima anapokumwa na sababu zilizoko nje ya uwezo wake mfano ukame/mafuriko.

3.pia ni jukumu la serikali kuhakikisha mkulima wanaemuhamasisha kulima anauza kwa bei ya faida kupitia vyama vya ushirika kama wanavyofanya kwenye korosho kwamba ukikamatwa na korosho ambazo hazikununuliwa katika mfumo uliowekwa zinataifishwa.

Serikali yako haina muda na mwananchi, si chakula tu ni kwa huduma zote ndo maana inafurahi pale mkulima anapouza kwa bei ya hasara na maajabu zaidi pamoja na kuwa na bei ndogo wanaendelea kuruhusu mengine toka nchi jirani.
 
Waziri wetu wa Kilimo ninamjua ni mchapakazi. Alipita nchi nzima kuhamasisha wakulima walime kukabiliana na baa la upungufu wa chakula ulioashiria mwanzoni. Pia ilitangazwa,asiyelima,hakuna msaada wa chakula toka mamlakani. Matokeo,Kusini mwa Tanzania,hasa Ruvuma,Mbeya,Rukwa nk,wamefanikiwa kuvuna mahindi mengi. Soko lake linasuasua sana. Bei ni ndogo,siyo ya motisha. Wengi wameamua kuhifadhi hadi bei iwe nzuri. Haijajulikana bei itabadilika lini na kwa msukumo upi! Baadhi ya wakulima hawana maghala imara,pia uharibifu wa wadudu umeanza kwa kasi. Mvua nazo zinakaribia watu waanze msimu mwingine. Nini msukumo wa Wizara kuona soko lenye bei ya motisha linapatikana? Kimya kimekuwa kingi,yawezekana tafsiri ya PM kuwa mahindi yasindikwe,bado haijaeleweka kwa Wakulima. Huenda wanasubiri ufafanuzi zaidi kutoka Wizara yenye dhamana na mazao?

Hakuna maendeleo ya kilimo Tanzania kama mazao ya kilimo yataendelea kuchukuliwa kama kinga ya njaa tu. Ni kweli ni muhimu sana kuwa na uhakika wa chakula kwa Taifa, lakini tathimini hiyo lazima ifanyike vizuri ili kujua mahitaji halisi ya chakula ndani ya nchi ili kuepuka janga la njaa. Baada ya hapo ziada lazima iingie sokoni kama bidhaa ili kuweza kuchochea maendeleo ya kilimo kupitia uwekezaji mkubwa. Hakuna mkulima mkubwa ambaye atawekeza fedha zake kwenye kilimo akavuna gunia mathalani 2000 za mahindi halafu afanye tena hivyo msimu unaofuata kama soko ni la kupangiwa. Soko siyo lazima liwe la nje ya nchi tu. Serikali inaweza kuwa soko zuri tu kama itatoa bei ambayo ni competitive
 
Mkuu utanidanganya kote lkn sio wilaya yoyote ya mkoa wa Tanga Na Mbeya!!
Gunia la mahindi kwa huko Muheza limefikia bei hiyo uliyoitaja mwanzoni mwa mwaka huu mkuu!
Kama nakumbuka Vizuri Ni February hadi April!!
Kuna biashara zangu nyingi huko nakuja sana!
Handeni, Kilindi, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga Na mwisho nachukua nazi Pangani!!
Hahahaha yaani wewe kuwa na biashara zako huku siyo sababu kuu ya kujua bei ya mzao kwa muda huu?

Nataka nikwambie kuwa bei imeanza 5000/= kwa debe hapo mwezi August baada ya kuvuna baadae ikaenda hadi 6000/= muda huu iko kwenye 7000/=

Nimekusanya mahindi mimi kwa bei ya 5000/= debe hadi 6000/= kwa muheza(vijiji vya mafere, mkuzi, kilulu na mindu) na pangani( vijiji vya masaika, kigurusimba, mivumoni, mwembeni hadi madanga) tena baadhi wanaleta wenyewe kwenye kituo cha kukusanyia.

Sasa endelea kuwa na bei za kuhadithiwa!
 
Back
Top Bottom