WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amesema leo ataeleza mafanikio ya Serikali katika kutoa ajira kwa vijana ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kusema tatizo hilo ni bomu linalosubiri kulipuka na kuliomba Kanisa Katoliki liisaidie kutafuta ufumbuzi.
Juzi, akitoa salamu katika sherehe za uzinduzi wa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki la Ifakara, Morogoro, Lowassa alisema: Nawaomba maaskofu katika miradi yenu mlipe kipaumbele suala la tatizo la ajira kwa vijana... wengi wanaohitimu elimu ya sekondari na vyuo wanakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. Hili kama tulivyosema ni bomu linalosubiri kulipuka...
Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu tatizo hilo la ajira, Waziri Kabaka alisema leo atoa takwimu za ajira zilitolewa na Serikali kwa vijana na kueleza kile ambacho Serikali imekifanya na kuendelea kufanya katika kushughulikia tatizo la ajira nchini.
Profesa Lipumba: Tatizo la ajira halijapatiwa dawa
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana pia alizungumzia suala hilo la ajira kwa vijana akisema bado halijapatiwa ufumbuzi. Profesa Lipumba ambaye kitaaluma ni mchumi, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza Kuu la CUF.
Alisema vijana wengi wamekata tamaa kwa sababu ni wachache tu walioajiriwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.
Akitoa mfano, Profesa Lipumba alisema kati ya vijana 22 milioni waliopo nchini ni 93,000 tu, walioajiriwa katika sekta ya viwanda, idadi ambayo alisema ni ndogo... Hili ni tatizo kubwa ambalo Serikali inatakiwa kujitathmini namna ya kuondokana nalo kwa sababu vijana wanaendelea kuichukia.
Alisema sekta ya kilimo ambayo ndiyo ingeajiri vijana wengi, bado haijapewa kipaumbele na Serikali na kuonekana kama adhabu. Alisema mkulima anapolima na kuvuna mazao yake, Serikali inaingilia kati na kumpangia namna ya kuyauza.
Mkulima huyo amelima peke yake, ametunza mazao peke yake lakini anapovuna hana uhuru wa kutafuta masoko yenye maslahi, badala yake Serikali inampangia sehemu za kuuza zisizo masoko mazuri, alisema Profesa Lipumba.
Serikali kutoa tamko la ajira leo
Kuna gazeti limenukuu taarifa ya serikali kupitia waziri wa ajira Kabaka kuwa hakuna Bomu lolote la ajira litakalolipuka na kuwa wenye mawazo ya kuwa kuna bomu la ajira wana mawazo mgando na kuwa serikali imefanya jitihada na mbinu nyingi na sasa tatizo la ajira hakuna.my take huyu waziri aliitoa kauli hii akiwa amelewa baa au amekurupushwa usingizini!nawasilisha
You can imagine hawa ndio mawaziri wa JK. Tatizo liko wazi hata halihitaji tochi, jitu limelewa madaraka linasimam na kusema hakuna bomu. Liambie litoe takwimu katika wahitimu wa vyuo vyote wangapi wamepata ajira be it private, government or self employed. Ana takwimu?, sasa anasema kutoka wapi kuwa hakuna bomu.
.Unadhani serikali inaweza ajiri kila anayehitaji ajira?