Wizara ya Kazi na Ajira si chochote si lolote - bora ifutwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Kazi na Ajira si chochote si lolote - bora ifutwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Nov 24, 2010.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hii Wizara ya kazi na Ajira haina faida yoyote kwa Watanzania.

  Kwanza walitangaza mishahara ya sekta binafsi, wakashindwa kuisimamia. Mambo ni siasa siasa tu hamna lolote.

  Pili, Kazi za serikali hutangazwa na Ofisi ya Rais menejiment ya Utumishi wa Umma.

  Tatu, haina msaada wowote kwa vijana wa Tanzania wanaohangaika na kutafuta ajira.

  Je faida yake ni nini hii Wizara,

  Nashauri hii wizara ingeunganishwa na Ofisi ya raisi menejiment ya utumishi wa Umma. Kwa hiyo ingekuwa kama moja ya Kurugenzi ikiwa na Mkurugenzi wake.
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja!
   
 3. The last don

  The last don JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Naunga mkono hoja.
   
 4. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  naunga mkono joja
   
 5. T

  The Big G Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  fungu hili limeafikiwa
   
 6. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amesema leo ataeleza mafanikio ya Serikali katika kutoa ajira kwa vijana ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kusema tatizo hilo ni bomu linalosubiri kulipuka na kuliomba Kanisa Katoliki liisaidie kutafuta ufumbuzi.


  Juzi, akitoa salamu katika sherehe za uzinduzi wa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki la Ifakara, Morogoro, Lowassa alisema: "Nawaomba maaskofu katika miradi yenu mlipe kipaumbele suala la tatizo la ajira kwa vijana... wengi wanaohitimu elimu ya sekondari na vyuo wanakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. Hili kama tulivyosema ni bomu linalosubiri kulipuka..."

  Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu tatizo hilo la ajira, Waziri Kabaka alisema leo atoa takwimu za ajira zilitolewa na Serikali kwa vijana na kueleza kile ambacho Serikali imekifanya na kuendelea kufanya katika kushughulikia tatizo la ajira nchini.

  Profesa Lipumba: Tatizo la ajira halijapatiwa dawa


  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana pia alizungumzia suala hilo la ajira kwa vijana akisema bado halijapatiwa ufumbuzi. Profesa Lipumba ambaye kitaaluma ni mchumi, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza Kuu la CUF.

  Alisema vijana wengi wamekata tamaa kwa sababu ni wachache tu walioajiriwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.
  Akitoa mfano, Profesa Lipumba alisema kati ya vijana 22 milioni waliopo nchini ni 93,000 tu, walioajiriwa katika sekta ya viwanda, idadi ambayo alisema ni ndogo... "Hili ni tatizo kubwa ambalo Serikali inatakiwa kujitathmini namna ya kuondokana nalo kwa sababu vijana wanaendelea kuichukia."

  Alisema sekta ya kilimo ambayo ndiyo ingeajiri vijana wengi, bado haijapewa kipaumbele na Serikali na kuonekana kama adhabu. Alisema mkulima anapolima na kuvuna mazao yake, Serikali inaingilia kati na kumpangia namna ya kuyauza.

  "Mkulima huyo amelima peke yake, ametunza mazao peke yake lakini anapovuna hana uhuru wa kutafuta masoko yenye maslahi, badala yake Serikali inampangia sehemu za kuuza zisizo masoko mazuri," alisema Profesa Lipumba.

  Serikali kutoa tamko la ajira leo
   
 7. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,891
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  Mkubwa huyu mama alikuwa anamjibu Lowasa only. Wala usipoteze muda msg sent to Lowasa
   
 8. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuna gazeti limenukuu taarifa ya serikali kupitia waziri wa ajira Kabaka kuwa hakuna Bomu lolote la ajira litakalolipuka na kuwa wenye mawazo ya kuwa kuna bomu la ajira wana mawazo mgando na kuwa serikali imefanya jitihada na mbinu nyingi na sasa tatizo la ajira hakuna.my take huyu waziri aliitoa kauli hii akiwa amelewa baa au amekurupushwa usingizini!nawasilisha
   
 9. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  You can imagine hawa ndio mawaziri wa JK. Tatizo liko wazi hata halihitaji tochi, jitu limelewa madaraka linasimam na kusema hakuna bomu. Liambie litoe takwimu katika wahitimu wa vyuo vyote wangapi wamepata ajira be it private, government or self employed. Ana takwimu?, sasa anasema kutoka wapi kuwa hakuna bomu.
   
 10. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  mpaka liwalipukie ndipo watakapojua....
   
 11. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa mwaka vyuo vinazalisha watu 50,000 ajira ziko 100 pata picha mwaka 2015 itakuwaje Lowasa akiongea anaonekana ana akili zimeganda!chukua hatua mapema
   
 12. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kama waziri wa kazi anazungumza hivi-unaweza pima uwezo wa uelewa wake ulivyo
   
 13. S

  Shembago JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapendwa,

  Nashawishika kukubali usemi wa Mamvi kwamba serikali imelala kuhusu ajira kwa vijana kwa jambo moja tu ambalo japo itaonekana ni haba lakini inaleta picha mbaya kwa serikali ya chama cha magamba.

  leo hii kuna watu wanojiita wawekezaji ambao wanakuja na kuingiza watu wao ambao kwanza unqualified lakini na undugu nization wanauleta huku kwetu,utakuta huko kwao yamemshinda nakuja kupewa ajira TZ,wakati sheria ipo wazi kabisa kuhusu wafanyakzi wa nje ni kwa zile kazi ambazo kweli wa TZ hatuna ujuzi nazo!

  Hivi iweje mtu ambaye ni Plumber leo anakuja TZ anaombew kibali kama Operation manager wakati kazi anayoifanya haiendani hata na Title aliyoombewa kazi?

  Inauma sana!

  Nawakilisha
   
 14. k

  kaaa Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana kucheka cheka, haoni kama ni tatizo hilo.Yeye anaona sawa tuu:):thinking::thinking:
   
 15. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Aliyeshiba hamjui mwenye njaa bandugu
   
 16. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Tanzania imelala au ni vipofu?

  Anza na magraduate wanaozunguka na vyeti

  Fuatia form six leavers

  form form

  Darasa la saba

  Mafisadi na watoto wao wameshiba, shida ya ajira wataionaje?

  Pia hata Rich Mondului ni sehemu ya Tatizo. Kwa nini asikishauri chama chake? Ana tamaa ya uraisi

  Unakuta vigogo wanamiliki ardhi na kuwanyima wanyonge,...

  unakuta mikopo inakwenda kwa vigogo.


  Ajira ni bomu
   
 17. v

  valid statement JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Unadhani serikali inaweza ajiri kila anayehitaji ajira?
   
 18. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  Hakuna reli,viwanda, masoko ya uhakika wa mazao,umeme,maji ya umwagiliaji ajira itoke wapi zaidi ya uwakala wa china!
   
 19. S

  SI unit JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  .
  Ishu sio serikali iajiri kila anaehitaji ajira bro, but iwajengee uwezo (to empower) wananchi wake wajiajiri kwa kutumia rasilimali za nchi. Huwa tunapiga kelele kuhusu ujasiriamali n.k. but hatujiulizi jinsi serikali inavyosimamia na kuwezesha hao wajasiriamali. Kulikua na mamilioni ya baba mwanaasha one time, hatuelewi yalikoyeyukia. Tuwe wakweli bana, serikali haina sera ya msingi katika hili eneo la ajira, ama haijaweza kusimamia vema sera ya ajira (kama ipo sera makini)..
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,535
  Likes Received: 10,455
  Trophy Points: 280
  hizi shule za kata ndio kifo cha ccm.
   
Loading...