Wizara ya Habari yakanusha habari ya gazeti la MwanaHalisi kuhusu Mwakyembe

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,124
2,092
Taarifa ya wizara ya habari kupitia TBC imekanusha Mwakyembe kufanya mahojiano na gazeti Mwandishi wa habari hiyo (Mwakyembe: Maisha yangu yapo hatarini) na kusisitiza kuwa wizara inaangalia hatua za kuchukua.
cfa9b8c92ffd73df2d7cce63740c09c6.jpg
 
Hili gazeti si ndio linaidai serikali mamilioni ya shilingi kama fidia.... Mwakyembe umejipanga lakini.?
 
Kama ilivyokawaida ya huyu jamaaa naona mwanahalisi wamemkurupusha sasa kitakachofuata anakijua mwenyewe. Huyu jamaaa niliwahi kumshuhudia akiwafukuza waandishi wa habari kwenye chuo kimoja kilichoko Iringa na kuwatisha kuwa hataki habari zake kutembelea chuo hicho ziandikwe na kutangazwa na chombo chochote cha habari. Ajabu hata aliyoyaongea na kuyaahidi akiwa chuoni hapo alikuja kuyapinga kwa mdomo wake mwenyewe akiwa kwenye bunge la katiba. Kweli huyu jamaaa haaminiki kabisa, kuna umuhimu wa kumtilia shaka tena kwa kalamu nyekundu.
 
hapo kwwasababu waziri wa habari ndiye mlalamikaji patakuwa na mgongano wa kimaslahi. ni habari gani hiyo wakuu:)
 
Taarifa ya wizara ya habari kupitia tbc imekanusha mwakyembe kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hiyo na kusisitiza kuwa wizara inaangalia hatua za kuchukua. Source taarifa ya habari tbc saa 2 usiku



Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu awezaye kumuamini Mwakyembe,ni kiongozi mwenye ndimi mbili na asiyeweza kuyasimamia hata yale anayoyaamini.

Wakati yeye ana hofu juu ya mambo yasiyooneka,hofu ya kusadikika,wenzake tupo kwenye hofu halisi,hofu ya kutojua hatima yetu,hofu inayoyaweka maisha yetu rehani.Hatuna uhakika kesho yetu itakuwaje,hofu ya ugumu wa maisha.

Mtu anayerishwa na kulindwa kwa kodi zetu yeye pamoja na familia yake,anapokuja na kutuambia kuwa maisha yake yapo hatarini ni dhihaka kwetu tunaomtunza na kumlinda kwa mapato ya jasho letu.

Yeye ni nani kwetu,fursa alizonazo katika nchi hii hazijawahi kuwa msaada wowote kwetu,alitangulizwa mbele katika sakata la Richmond,akafanikiwa kuuhadaa umma wa watanzania kuwa alikuwa anapigana kwa niaba yetu,kumbe alikuwa anapigana kwa niaba ya tumbo lake na la wale waliomtuma,ndiyo! Yalikuwa ni mapambano juu ya vyeo!

Miaka 9 baada ya yeye kutumika kupigania tumbo lake na la wale waliomtuma,ameuthibitisha unafiki wake pale alipoidharau lipoti ya Nnape iliyowasilishwa Na timu aliyoiunda ili kumchunguza "mwana mfalme" katika kadhia ya kuvamiwa kwa Clauds.Mwakyembe aliita ripoti ile kuwa ni ripoti ya upande mmoja na hivyo imepoteza sifa eti kwa sababu haikumuhoji mkuu wa mkoa,ingemuhoji vipi wakati timu ile ilipofika ofisini kwa mkuu wa mkoa,mkuu huyo aliitoroka timu ile kwa kupitia dirishani?

Hoja kwamba timu ya uchunguzi iliyoundwa na mtangulizi wake kuwa imekosa weledi kwa sababu haikumuhoji Makonda,ilikuwa ni kejeli kwetu.Akiwa Mwenyekiti wa kamati teule ya bunge iliyoundwa ili kuuchunguza mkataba tata wa Richmond,kamati yake ilisafiri hadi"Ulaya" kwenda kuutafuta ukweli kuhusu Richmond,lakini ilishindwa kwenda kumuhoji Mh.Lowassa aliyekuwa mita chache sana pale Magogoni DSM.

Hata kama kamati teule ilikuwa imechoka kutembelea magari yenye viyoyozi kwenda kumuhoji Mh.Lowassa,tulikuwa radhi kuwabeba mgongoni wajumbe wa kamati teule ili wafike Ofisi ya Waziri mkuu pale Magogoni wakamuhoji na kutuletea ukweli juu ya uhusika wake katika sakata la Richmond.Lakini kwa sababu anazozijuwa yeye na wale waliomtuma,hakwenda kumuhoji Mh.Lowassa,badala yake walitumia kodi zetu kwenda kuzurura Ulaya eti wanatafuta uhusika wa Mh.Lowassa katika sakata la Richmond.

Asijaribu kuuhadaa umma uliokwisha mpuuza,hofu yake juu ya usalama wake ni matokeo ya siasa zake chafu,ni zao la unafiki wake na kutumika kwake kuwaangusha wenzake.Aache kukikimbia kivuli chake,kivuli hakikimbiwi kitaenda naye sambamba kwa spidi ileile anayoitumia yeye kukikimbia kivuli chake.

Maisha yake kuwa hatarini ni hoja ya kipumbavu zaidi ya upumbavu wa kiwango cha PhD ya maganda ya korosho!Hatari ipi inayomnyemelea na kwa lipi hasa?Ni jambo gani alilolisimamia hadi astahiri huruma yetu?Kama alilikana hadi andiko lake mwenyewe lililompa Permanent head Disorder(PhD),tunaanzia wapi kumuamini mwanasiasa huyu mchumia tumbo mwenye rangi nyingi zaidi ya kinyonga?Hakuna atakayeishi milele,sote tutakufa hivyo kama "ananyemelewa na kifo" afe tu nasi tutamfuata pale zamu yetu itakapofika.Aache siasa za kipumbavu na kilaghai.
 
Ina maana zile nukuu ni za uzushi?

Aseme tu kama katishwa.
Habari ikitolewa na kiongozi wa serikali au CCM lazima mjifanye kuibishia.. Ila habari ikitolewa na vyombo vingine ikiponda serikali au kiongozi wa serikali hamjishughulishi kutaka kupata ukweli ni doublestandard
 
Back
Top Bottom