Ndiho
JF-Expert Member
- Feb 23, 2013
- 2,306
- 1,531
Wana Jamvi,
Nimesoma kwa masikitiko makubwa na mshangao juu ya Wizara ya Serikali yetu kusaidiwa MEZA na VITI na kampuni binafsi ya China kupitia Ubalozi wao. Jambo hill ni aibu na linatufanya tuonekani kweli bado hatuwezi kujitegemea.
Mbao tunazo, mafundi tunao, inawezekanaje kwamba ofisi ya serikali ngazi ya wizara haina Meza na viti?
Jeshi la magereza na Jkt wanazo karakana za useremala na wanatengeneza samani za majumbani na maofisini. Kwanini wasitumiwe hao kutengeneza samani za ofisi zetu?
Karne ya leo tunaposhindwa hata kutengeneza kiti na Meza kwa ajili ya ofisi zetu ni aibu ya karne.
Ikiwa watu wanatusaidia viti na Meza za ofisi zetu, watashindwa kubeba pembe za faru, na meno ya tembo wetu? Aibu ya karne hii!!!!