Wizara ya Elimu yafanya ujenzi wa madarasa Tanga

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo amekagua na kufungua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi kilole, Matondoro, na Kilimani na kuweka jiwe la msingi bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Semkiwa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

Akizungumza Mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi hiyo Waziri Ndalichako amesema suala la nchi kuwa na shule au vyumba vya madarasa vya nyasi litabaki kuwa historia kwa kuwa serikali ya awamu ya Tano inahitaji wanafunzi wapate Elimu bora inayoenda sambamba na uboreshaji wa miundombinu na hicho ndicho kinachofanyika hivi sasa.

Akizindua bweni moja la wasichana katika shule ya Sekondari Semkiwa waziri Ndalichako ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ili bweni hilo lianze kutumika mara moja.

Pia amewataka watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa namna anavyojitoa katika kuwatumikia Wananchi wanyonge kwa lengo la kuliletea Taifa Maendeleo.

Ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa,na vyoo umetekelezwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa Lipa kulingana na matokeo, (EP4R).
 
IMG-20171013-WA0015.jpg
 
Uyo alievaa suti huyo ni mwanaume....mwanaume kwa maana ya mwanaume kweli...ni Mkuu wa wilaya anaejua nini maana ya Ukuu wa wilaya...pamoja na Siasa za mkorogano za mji wa korogwe lakini bado mwanaume anatoboa kama SpiderMan vile.
 
hongera sana mkurugenzi wa korogwe na mkuu w korogwe mna speed ya maendeleo hasa katika ujenzi wa madarasa , wana korogwe tumepata viongozi wachapa kazi
 
sijui kama haya madarasa yatasaidiakama maslai ya walimu yataendelea kuwa hivi yalivyo.

Ikumbukwe hata mwalimu Nyerere Era wanafunzi walimudu stadi za KKK wanafunzi wakiwa bush school chini ya miti

Walimu tunaumia mwaka wa sita daraja lile lile hamna posho wala rikizo wala uhamisho wala elimu za kujiendeleza kama masters au PhD hazitambuliwi kwa walimu wa kawaida.

Hongereni kwa ujenzi ila kiukweli hatuwezi kwenda mbele kielimu kwa kujenga madarasa
 
Back
Top Bottom