Wizara ya elimu: Ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa katika gazeti la nipashe la tarehe 05 agosti

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,761
5,877
Katika gazeti la Nipashe la leo Jumatatu tarehe 5 Agosti, 2013 toleo Namba 057834 ukurasa wa mbele na wa nne kuna habari inayosomeka "Elimu: Aibu, aibu". Katika habari hii mwandishi anaelezea kwamba kuna Madudu zaidi yamebainika katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, baada ya kuwapanga baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano kwenye shule ambazo hazina masomo ya michepuo yao.

Habari hiyo imenukuliwa kimakosa kutoka katika Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo imepotosha ukweli wa Taarifa husika. Usahihi wa Taarifa yenyewe ni kwamba wanafunzi waliobadilishiwa shule ni wale walioomba wenyewe kubadilishiwa michepuo (combination) na si kwamba walibadilishwa kutokana na kukosa michepuo waliyopangiwa awali katika shule hizo.

Aidha, wanafunzi wengine waliobadilishiwa shule ni wale waliopangwa mbali kutoka sehemu wanazoishi, walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali na walioomba kupangwa katika shule za kutwa kutokana na sababu za kiuchumi.

Wizara huwapanga wanafunzi wa Kidato cha tano kwa kufuata Taarifa zilizojazwa na wanafunzi wenyewe kwenye Selection Form (SEL Form) ambapo wanafunzi wanajaza machaguo yao kulingana na matarajio yao.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya kupangwa Kidato cha 5 wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2012 tarehe 10 Julai, 2013. Baada ya tangazo hilo, Wizara ilipokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kubadili shule au machaguo (combinations) walizopangwa kwa sababu mbalimbali. Wizara ilitafakari maombi hayo na kufanya mabadiliko ya shule/ machaguo.

Imetolewa na:
Ntambi Bunyazu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano

Moja ya sifa ya kufanya kazi serikalini ni KUKANUSHA UKWELI." Baada Policcm kuua mfanyabiashara na kuiba pesa zake, wananchi tuliona na kusema, Kova alikanusha. Baada ya muda tukasikia wale policcm wameshitakiwa. Baada ya Mh JK kusaini sharia ya Uchaguzi, Dr. Slaa akasema amechomekewa. Werema alikuja kanusha, mwisho wa siku lisheria lenyewe likatupiliwa mbali. Serikali imekosa uaminifu na wengi wa watumishi wake sio waaminifu
 
Hakika Serikali imekosa uaminifu, kilichoko kwenye tovuti ya wizara hicho hapo. Sasa gazeti limedanganya nini?

ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO WALIOBADILISHIWA SHULE/MACHAGUO-2013

| Print |
MABADILIKO YA SHULE NA MACHAGUO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA 5 MWAKA 2013

Tarehe 10 Julai 2013, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya kupangwa Kidato cha 5 wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2012. Katika tangazo hilo Wizara iliwahimiza wanafunzi kuripoti katika shule zao walizopangwa kabla ya tarehe 29 Julai 2013. Baada ya tangazo hilo, Wizara imepokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kubadili shule au machaguo (combinations) walizopangwa kwa sababu mbalimbali. Wizara imetafakari maombi hayo na kufanya mabadiliko ya shule/machaguo kwa wanafunzi wenye sababu zifuatazo:
Waliopangwa shule za kutwa mahali ambapo hawana pa kuishi;

  • Waliopangwa mbali sana kutoka sehemu wanazoishi;
  • Walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali;
  • Walioomba kuhamia shule za kutwa kwa sababu za kiuchumi;
  • Walioomba kubadili ‘combinations' ambazo hazipo katika shule walizopangwa awali
Wakuu wa shule wanaelekezwa kuwapokea wanafunzi hawa katika shule hizo mpya na kuwasiliana na wakuu wa shule walizopangwa awali ili wawatumie ‘Sel form' za wanafunzi hawa. Aidha, mnatakiwa kuhakiki uhalali wa kila mwanafunzi mnayempokea kwa kutumia orodha ya majina yaliyomo katika tovuti pamoja na Result Slip za wanafunzi hao.

Wizara inawaagiza wanafunzi wote waliokubaliwa kubadilishiwa shule/combinations ambao taarifa zao zipo kwenye tovuti waripoti mara moja katika shule hizo. Wizara haitatoa barua kwa mwanafunzi yeyote. Aidha kuanzia sasa Wizara haitapokea maombi yoyote ya kubadilisha shule/combinations. Endapo yatakuwepo maombi yo yote yafuate utaratibu wa kawaida wa uhamisho kupitia kwa wakuu wa shule.

Imetolewa na
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
 
Wanafikiri bado wana deal na kizazi cha S.L.P na tele.. Money Order.
 
Thanx Mkuu, tumeshawazoea hao walipwa mishahara kwa kukanusha ukweli hawana tofauti sana na wale wa Buku 7 (Lumumba guys)
 
Hawa jamaa hawajajipanga kabisa. Kama waliamua kusingizia kuwa mwandishi ndiyo kachemka kaandika uongo, kwa nini wasingeondoa kwanza hilo tangazo lao ambalo ndio alilinukuu mwandishi?
 
walioomba kubadili combinations ambazo hazipo katika shule walizopangiwa awali

Walichomaanisha hapo wizara ni kwamba wale wanafunzi walioomba kupangiwa combinations mpya na ambazo hazipo kwenye shule walizopangiwa mwanzoni, wamehamishiwa kwenye shule mpya ambazo zina hayo masomo wanavyotaka kusoma sasa. Kwa mfano mwanafunzi A alichaguliwa kusoma PCB shule B. Lakini sasa anataka kusoma EGM ambayo haipo kwenye shule B basi kahamishiwa shule C ambayo ina mchepuo huo.

Kwa Mwandishi yeyote makini angeliweza ku counter check kirahisi sana kwa kulinganisha tangazo la awali la waliochaguliwa kuingia kidato cha tano na hili la sasa. Kwa mfano kama mwanafunzi A alipangwa shule B basi angechecki kama kweli hiyo shule B haina mchepuo huo.

Unavyokosoa uzembe wa mtu mwingine ni vizuri mno ujiridhishe na taarifa unayotumia. Hilo tangazo la wizara ni ambiguous na linaweza kuwa na maana nyingi. Lakini kwasababu Mwandishi aliamua kukosoa basi angejiridhisha na source nyingine na sio kukurupuka tu.
 
Hilo tangazo la wizara ni ambiguous na linaweza kuwa na maana nyingi.

Naunga mkono hoja na ndiyo maana hata gazeti liliandika vizuri kabisa ELIMU AIBU AIBU. Hata nami nasema ni aibu sana kama wizara yenye jukumu la kuelimisha vijana wetu linashindwa hata kutoa tangazo tu ambalo halina utata. Suala la kusema kuwa awali walipangiwa shule ambazo hazina michepuo waliyoomba na sasa wamebadilishiwa, hiyo ndiyo tinasema ni AIBU, AIBU. Kwani wakati wanapanga hawakuwa na orodha ya shule inayoonesha michepuo iliyopo katika hizo shule?

Kulikuwa na haja gani ya kushirikisha Wakuu wa shule kama upangaji wa wanafunzi kidato cha tano ilikuwa ni holela tu bila kujali kama wanachopanga kipo au hakipo? Hakika ELIMU AIBU, AIBU
 
Mkuu Kokomili,
Inaelekea hapo juu hujanielewa nilichoandikana pia hujalielewa hilo tangazo la wizara.

Kutokulielewa hilo tangazo ni sahihi kabisa maana tangazo linachanganya. Ila kwa mwandishi wa habari kabla ya kuandika hiyo habari ningetegemea ajiridhishe kwanza kwa kutumia facts mbalimbali zilipo.

Mimi nilivyoelewa hilo tangazo la wizara ni kwamba: Hakuna wanafunzi waliopangiwa shule ambazo hazina michepuo waliyopangiwa. Kwahiyo ukienda kwenye tangazo lao la kuchagua wanafunza kuingia kidato cha tano utakuta kila mwanafunzi amepangiwa shule ambayo ina mchepuo ule aliochaguliwa kujiunga nao.

Sasa, kwasababu mbalimbali baadhi ya wanafunzi wameomba kubadilishiwa michepuo. Kwa mfano kijana alipangiwa PCB Kibaha. Anagundua kuna tatizo na sasa anataka asome EGM. Nafikiri walichofanya wizara ni kwamba kama hiyo EGM haipo hapo Kibaha basi wamemhamisha huyo kijana aende shule ambayo ina EGM anayotaka kusoma. Kama EGM nayo sawa na PCB ipo Kibaha basi wanamwacha hapo hapo ila mchepuo ndio anabadilisha.

Kwahiyo sio kweli kwamba kuna vijana walipangiwa combinations ambazo hazipo kwenye shule walizopangiwa. Hivyo ndivyo nilivyoelewa mimi. Ninaweza kuwa wrong, ndio maana ni muhimu hasa kwa gazeti ku check facts zote.

Kosa hapa kwanza liko kwa mtoa taarifa wa wizara. Ameandika taarifa ambayo bila mtu kuchunguza unaweza kuielewa tofauti.

Lakini pia kwa gazeti mpaka kuandika makala kama hiyo ya kuikosoa wizara, ilitakiwa wafanye uchunguzi wao binafsi ili kujiridhisha. Inaelekea hawakufanya hicho kitu na hapo ndio wamekurupuka. Mwananchi wa kawaida nitaelewa akilalamika lakini kwa gazeti kwa kweli ningelitegemea wafanye uchunguzi wao na kujiridhisha na facts zilizopo.

Kwasababu hawakufanya, tafsiri waliyoitoa kwenye hilo tangazo sio sahihi na facts zilizopo zinapingana na hiyo tafsiri yao.
 
Hakika Serikali imekosa uaminifu, kilichoko kwenye tovuti ya wizara hicho hapo. Sasa gazeti limedanganya nini?

ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO WALIOBADILISHIWA SHULE/MACHAGUO-2013
ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO WALIOBADILISHIWA SHULE/MACHAGUO-2013 | Print |
MABADILIKO YA SHULE NA MACHAGUO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA 5 MWAKA 2013

Tarehe 10 Julai 2013, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya kupangwa Kidato cha 5 wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2012. Katika tangazo hilo Wizara iliwahimiza wanafunzi kuripoti katika shule zao walizopangwa kabla ya tarehe 29 Julai 2013. Baada ya tangazo hilo, Wizara imepokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kubadili shule au machaguo (combinations) walizopangwa kwa sababu mbalimbali. Wizara imetafakari maombi hayo na kufanya mabadiliko ya shule/machaguo kwa wanafunzi wenye sababu zifuatazo:
Waliopangwa shule za kutwa mahali ambapo hawana pa kuishi;

  • Waliopangwa mbali sana kutoka sehemu wanazoishi;
  • Walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali;
  • Walioomba kuhamia shule za kutwa kwa sababu za kiuchumi;
  • Walioomba kubadili ‘combinations’ ambazo hazipo katika shule walizopangwa awali
Wakuu wa shule wanaelekezwa kuwapokea wanafunzi hawa katika shule hizo mpya na kuwasiliana na wakuu wa shule walizopangwa awali ili wawatumie ‘Sel form’ za wanafunzi hawa. Aidha, mnatakiwa kuhakiki uhalali wa kila mwanafunzi mnayempokea kwa kutumia orodha ya majina yaliyomo katika tovuti pamoja na Result Slip za wanafunzi hao.

Wizara inawaagiza wanafunzi wote waliokubaliwa kubadilishiwa shule/combinations ambao taarifa zao zipo kwenye tovuti waripoti mara moja katika shule hizo. Wizara haitatoa barua kwa mwanafunzi yeyote. Aidha kuanzia sasa Wizara haitapokea maombi yoyote ya kubadilisha shule/combinations. Endapo yatakuwepo maombi yo yote yafuate utaratibu wa kawaida wa uhamisho kupitia kwa wakuu wa shule.

Imetolewa na
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
mkuu rudia kusoma hiyo habari.hujaielewa.
 
Kwa kweli mkuu alikurupuka katika kumjibu mwandishi wa gazeti la nipashe.Na yeye ndiye mkuu wa idara ya mawasiliano,sasa inaonesha kuwa hakushirikishwa wakati wa kulitoa tangazo hilo na amejibia kitu kisichomhusu.Pengine Katibu mkuu ndiye pekee anayejua kilichomo katika hilo tangazo kwa uhakika zaidi au mkuu ameamua kusafisha hali ya hewa hata angali akijua kilichoko katika tangazo.
Hakika Serikali imekosa uaminifu, kilichoko kwenye tovuti ya wizara hicho hapo. Sasa gazeti limedanganya nini?

ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO WALIOBADILISHIWA SHULE/MACHAGUO-2013
ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO WALIOBADILISHIWA SHULE/MACHAGUO-2013 | Print |
MABADILIKO YA SHULE NA MACHAGUO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA 5 MWAKA 2013

Tarehe 10 Julai 2013, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya kupangwa Kidato cha 5 wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2012. Katika tangazo hilo Wizara iliwahimiza wanafunzi kuripoti katika shule zao walizopangwa kabla ya tarehe 29 Julai 2013. Baada ya tangazo hilo, Wizara imepokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kubadili shule au machaguo (combinations) walizopangwa kwa sababu mbalimbali. Wizara imetafakari maombi hayo na kufanya mabadiliko ya shule/machaguo kwa wanafunzi wenye sababu zifuatazo:
Waliopangwa shule za kutwa mahali ambapo hawana pa kuishi;

  • Waliopangwa mbali sana kutoka sehemu wanazoishi;
  • Walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali;
  • Walioomba kuhamia shule za kutwa kwa sababu za kiuchumi;
  • Walioomba kubadili ‘combinations’ ambazo hazipo katika shule walizopangwa awali
Wakuu wa shule wanaelekezwa kuwapokea wanafunzi hawa katika shule hizo mpya na kuwasiliana na wakuu wa shule walizopangwa awali ili wawatumie ‘Sel form’ za wanafunzi hawa. Aidha, mnatakiwa kuhakiki uhalali wa kila mwanafunzi mnayempokea kwa kutumia orodha ya majina yaliyomo katika tovuti pamoja na Result Slip za wanafunzi hao.

Wizara inawaagiza wanafunzi wote waliokubaliwa kubadilishiwa shule/combinations ambao taarifa zao zipo kwenye tovuti waripoti mara moja katika shule hizo. Wizara haitatoa barua kwa mwanafunzi yeyote. Aidha kuanzia sasa Wizara haitapokea maombi yoyote ya kubadilisha shule/combinations. Endapo yatakuwepo maombi yo yote yafuate utaratibu wa kawaida wa uhamisho kupitia kwa wakuu wa shule.

Imetolewa na
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
 
Umakini katika Wizara ya elimu imekuwa ni kitu adimu sana kuboronga ndiyo mtindo wa kisasa
 
Back
Top Bottom