pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 312
- 614
Hii Wizara ishakuwa kidonda ndugu, ubora wa elimu unashuka kila kukicha wahitimu tunaozalisha hawakidhi vigezo vya soko la ajira.
Shule zetu za umma uwiano wa wanafunzi kwa Mwalimu hauendani na uhalisia watoto wetu kila siku wanadaiwa hela na maelezo sahihi mwanangu wa Darasa la pili kila siku anatakiwa apeleke 500 bila hivyo anachapwa na kufelishwa inasikitisha.
Shule za binafsi ada haishikiki shule za umma elimu haikidhi, mashuleni hawaimbi tena nyimbo za taifa na za kizalendo badala yake wanawekewa nyimbo za kizazi kipya hata watoto wa kiume.
Hii sio sawa ikizingatiwa Wizara hii inaongozwa na msomi mwenye hadhi ya Uprofesa.