Wizara ya elimu imewawajibisha wahusika wangapi wa wizi wa mitihani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya elimu imewawajibisha wahusika wangapi wa wizi wa mitihani?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by FADHILIEJ, Jan 10, 2012.

 1. FADHILIEJ

  FADHILIEJ Senior Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa najitahidi sana kufuatilia habari hizi za wizi wa mitihani ya std vii,ni kweli kuna wanafunzi wamefutiwa matokeo yao na pia kuna taarifa kuwa watapata nafasi ya kurudia mitihani.
  NAOMBA MWENYE TAARIFA HIZI ATUJUZE HAPA JUKWAANI.SWALI LANGU LA MSINGI NI KWAMBA,HADI HIVI SASA
  1. NI MAOFISA WANGAPI WALIOHUSIKA NA KASHFA HIYO WAMETAMBULIKA?(Wakuu wa shule,askari waliokuwa wakilinda mitihani,Maderva waliosafirisha,wasimamizi wa mitihani nk)
  2. JE WANGAPI WAMEWAJIBISHWA ANGALAU KWA KUSIMAMISHWA KAZI?
  3. WANGAPI WAMEPEWA ONYO.
  4. NA NINI KINAENDELEA KUFANYIKA ILI KUHAKIKISHA KASHFA HII INAKUWA HISTORIA?
  NADHANI NIKIPATA MAJIBU HAYA TAWEZA KUTOA MAONI KWA WIZARA YETU YA ELIMU.

  NAWASILISHA.
   
 2. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu acha siasa katika jambo hili. Hivi maafisa elimu, madereva, walinzi wanahusikaje na wizi wa mtihani? Mitihani yenyewe ya std vii ni ya kuchagua kuanzia hesabu na masomo mengine. sasa mtoto ambaye hata hajui hesabu anawea kupata ufaulu mzuri kwa kukisia majibu.

  Kwa taarifa yako baraza la mitihani wanataka kujikosha kuwa wanafanya kazi kwa kuwafutia watoto mitihani kisa majibu yamefanana. hivi kwa majibu ya kuchagua kwanini majibu yasifanane?

  Pia hakuna ushahidi wa kuwaweka hatiani wote uliowataja, serikali inajua ikithubutu kuwa wafukuza ijue iwe tayari kulipa mamilioni ya fidia kwani watashinda kesi.

  Baraza la mitihani waache uhuni wa kunyanyasa watoto, hebu wabadilike walete mtihani wa kujieleza na maswali ya kujaza majibu sio kama ilivyo sasa
   
 3. FADHILIEJ

  FADHILIEJ Senior Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  MKONDAKAIYE,

  Hili jambo limeniudhi sana,na hapa siongelei siasa ninachosema ni kuwa hadi kufanyike wizi wa mitihani lazima kuna waliohusika,linapokuja suala la kuwaadhibu wanafunzi hapo ndo ninaumia zaidi,sasa kama ni adhabu wa kwanza ni waliohusika na wizi huo,ambapo lazima wakuu wa shule,askari wanaolinda lazima waone ni nini kinachoendelea,

  suala la kubadili mfumo wa mitihani ni zuri lakini kwa SUALA HILI HAKIKA WAMEWAONEO WANAFUNZI.
   
 4. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kwa hali hii serikali inaendelea kulea watendakazi wabovu,ndo maana mi naona bado hatujapata serikali ya kutatua matizo yetu,bila hata aibu serikali inakiri kufanyika kwa udanganyifu katika mitihani. Huu ni upumbavu,kwa kawada mitihani hii huwa ninasimamiwa kwa umakini hadi ulinzi wa polisi unakuwepo.Serikali ya JK bomu.
   
 5. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu hao uliowataja hapo juu wanahusika tena sana,wewe unataka tumuulize nani mtihani umevujaje? Wewe kama hujui pole sana,mtihani unavuja kwa hawa jamaa kuhongwa na kuachia mtihani sanasana wasimamizi na askari. Sidhani kama unachokisema ni kweli,mtihani ulikuwa wa kuchagua kila kitu?? Lazima kulikuwa na sehemu ya maelezo. Kama ingekuwa hvyo wizi usingetambulika.
   
 6. N

  Ninliy Senior Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  serikali yetu haipo serious na ndiyo maana hatupati maendeleo,hao hawawezi kuwajibishwa hii serikali ni ya uonevu!!!
   
Loading...