Wizara ya Elimu ihakiki matokeo ya wanachuo Mzumbe Mbeya mwaka 2015 kurudi nyuma

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Habari wapendwa,

Jana kuna barua ilikuwa humu JF kuhusu Abdi Mruma kufutiwa shahada yake ya sheria baada ya kugundulika alikuwa akighushi alama alizokuwa akipata.

Huu mchezo wa kughushi matokeo upo sana na ulikuwa ukifanywa na idara ya ICT, kuna mmoja ndio alikuwa kinara ila kwa sasa hayupo tena Mzumbe.

Ipo hivi, Wakati wa kujaza matokeo alikuwa anakutafuta au unamtafuta na kufanya maelewano ya pesa. Kama umepata C utajaziwa B+ au A.

Mruma amesoma chuo cha Uongozi wa mahakama, akasoma shahada ya sheria Mbeya kampasi ya Mzumbe na sasa amemaliza pale Law School na tayari ana mhuri wa uhakimu.

Huyu Mruma baada ya kumaliza shahada yake ya sheria, alirudi Mzumbe kufundisha wanafunzi wa stashahada ya sheria.Sasa kama mtu aliyegushi na kupata ufahulu mzuri mpaka akaaminiwa kufundisha wadogo zetu.

Wahitimu aina ya Mruma wapo wengi sana Mzumbe kampasi ya mbeya.
 
Back
Top Bottom