Wizara ya Afya yaandaa muswada wa kuvuna viungo vya watu, kama maini, figo, mapafu nk

Wakati Niko mdogo kwetu mtoto akilia alikuwa anatishiwa na story kuwa Kuna viumbe hatari wanaitwa makomanyuundo kazi yao viumbe hao nikuchukua viungo vya bin adamu haraka mtoto hunyamaza
Sasa kwa sheria hi mnafanya nione kuwa makomanyuundo wapo
 
  • Thanks
Reactions: _ID
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto imeanza kuandaa muswada wa sheria itakayosimamia uvunaji viungo vya binadamu zikiwemo figo, maini, moyo na mapafu ili vipandikizwe kwa wanaovihitaji.

Ofisa katika kitengo cha magonjwa yasiyoambikiza katika Idara ya Tiba kwenye wizara hiyo, Dk Linda Ezekiel alisema Dar es Salaam kuwa itatungwa sheria ya uvunaji na upandikizaji wa viungo vya binadamu kwa sababu huduma hiyo imeanza hivyo inahitaji sheria.

Daktari huyo bingwa wa magonjwa ya figo aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds kinachomilikiwa na Kampuni ya Clouds Media ya Dar es Salaam.

Alisema baadhi ya watu huenda wapo tayari wakifariki dunia viungo vyao vitolewe wapewe watu wengine lakini hakuna sheria kusimamia hilo.

Dk Linda alisema suala la kutoa kiungo au viungo kwenye mwili wa binadamu litakuwa la kisheria litakalowahusisha watoaji, familia zao, madaktari na wanasheria.
“Hakuna pesa yoyote inayopaswa kuwepo pale katika ule uchangiaji, ni haramu. Unaweza kuweka bei yoyote kwenye kiungo chochote? Huwezi, uhai unaweza kuweka bei yoyote? Unaona eeh, kutoa kwa kweli ni moyo,”alisema.

Kwa mujibu wa daktari huyo ambaye ni mratibu wa huduma za figo nchini, anatumaini hadi mwakani sheria hiyo itakuwa imetungwa ili kudhibiti na kusimamia uchangiaji viungo vya binadamu yakiwemo macho.

“Mchakato ulianza tangu mwaka juzi na mimi sasa hivi ndio kazi mojawapo ambazo nazisimamia. Tumeshamaliza mchakato wa ndani ya wizara sasa hivi tunakwenda kupata mawazo ya wananchi kujua na wao wanasemaje,”alisema Dk Linda.

Alisema makundi yakiwemo ya kidini, vijana na vyuo vikuu yatahusishwa kwenye mchakato huo ili kupata mawazo yao kuhusu uvunaji huo.
“Unapotoa figo ya mtu ambaye yupo hai sio kusema kwamba eti unamhatarishia misha yake kwa sababu kitu kimoja kizuri ni kwamba tuna figo mbili. Ukikata figo moja kwenye sehemu tatu ina maana una vipande vingapi kama una figo mbili, sita,” alisema Dk Linda na kuongeza:

“Tafiti zipo wazi kwamba, kwa ufanisi wako wewe mpaka unapoishi miaka sitini, themanini au tisini unahitaji kipande kimoja cha hivyo vipande sita kwa hiyo ina maana una vipande vya ziada vitano lakini sasa huwezi kukatakata ukatoa kipande kimoja kimoja kwa hiyo ina maana ile figo moja unapoitoa bado unamuachia reserve (akiba) ya vipande viwili”.

Pia alitoa mfano wa kijana mwenye umri wa miaka 18 aliyepata ajali lakini hakuwahi kuwa na matatizo yoyote yakiwemo ya moyo na kabla hajafariki dunia alielezwa kuhusu kuchukua viungo vyake na alikubali.

“Macho yanaweza yakaenda kusaidia mtu, moyo unaweza ukaenda kusaidia mtu, figo inaweza ikaenda kusaidia lakini hivyo tunahitaji sheria ndio sasa tunashughulikia. Tukishakuwa na sheria tunakuwa na chombo ambacho kinasimamia uvunaji,”alisema Dk Linda.

Alisema watu wanaohusika na tamaduni za Mtanzania watahusishwa kwenye maandalizi ya muswada huo na akatoa mfano wa nchi ya Croatia kuwa hakuna mtu anayepata kiungo kutoka kwa mtu aliye hai na kwamba, viungo vyote vinavyopandikizwa hutolewa kwa watu waliopoteza maisha au wagonjwa mahututi.

“Ajali imetokea Mtwara, mgonjwa yupo kwenye ICU Ligula, yule mgonjwa alishasema mimi siku ya siku ikifika kama limetokezea jamani vitu viende kusaidia. Kwa sababu tuseme ukweli tukizika vinakwenda ardhini, vinapotea. Hivi ni viungo vingewasaidia watu,”alisema Dk Linda.

Alisema mtu akiwa na akili timamu, baada ya kueleweshwa na akisaini kukubali kutoa kiungo chake hatakuwa na kisheria kukidai kiungo hicho baadaye.

“Sio kwamba mtu anasema leo nenda katoe, ni process (mchakato), unakwenda hospitali, unafanyiwa cancelling (unasihi), sio mara moja, mara mbili, mara tatu, unakwenda kwa daktari wa magonjwa ya akili naye anakutathmini kwamba huyu, kusudi sasa kusiwe na element yoyote ya influence (ushawishi)…una familia unakaa nao unawaeleza,”alisema.
Sualal uchangiaji viungo linafanyika duniani kote. Sisi tumechelewa sana. Watu wengi wanakufa kwa kukosa viungo mbadala kisa hakuna benki ya viungo. Nchi zilizoendelea wenye matatizo ya moyo, figo nk hupata viungo toka kwa watu waliojitolea. Hakuna maana yoyote ya kufa kisha ukazikwa na viungo vyako wakati vitu kama moyo vinaweza kusaidia wenzako wanaobaki duniani. Hiyo sadaka ni kubwa sana mbele ya Mungu.
 
Yaani mtu anywe mipombe huko, anywe midawa hovyo huko aharibu figo zake au moyo au ini lake au mapafu halafu mimi niyatunze yangu au ndugu yangu atunze yake mje kuyavuna......

Hiyo katu haitakuwa ubinadamu na itahatarisha usalama wa wagonjwa sababu kuna watu wanania mbaya wanaweza cheza michezo ya rafu na kuwamaliza watu wasio na hatia.

Hii michezo nimeifuatilia sana huko marekani na China, upumbavu mtupu.

Msije mkaruhusu huo uchafu. Mtu kama viungo vyake vimefeli ndugu zake watamsaidia, imeshindikana basi apambane na hali yake maisha ya kulazimisha huwa si mazuri.
 
Kama nina watoto na watalipwa basi sina pingamizi.

Kwa bure hapana, bora wakafaidi mchwa, tena maini yalivyo matamu
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Hili inabidi liwe la hiari au litazua balaa kubwa sana nchini. Kuna baadhi ya dini hili swala hawalikubali hata chembe. Madaktari wengi wa Bongo hawaamini watasema huyu mgonjwa ana mwezi mmoja tu wa kuishi hivyo ni bora tuanze uvunaji 😂 before it is too late na tumeshaangalia baadhi ya internal organs zake ziko vizuri.
Kuna watu ambao wamehukumiwa Kifo na Mahakama zetu je wataruhusiwa kuchukua "advance" ya fedha za uvunaji wa viungo vya?

Masikini ndio watakaovunwa zaidi na vigogo wa CCM na matajiri
 
Kwa upande wangu mimi nitaruhusu wanivune kihalali kusiwe na zengwe na atakaefaidika awe Masikini
 
sasa nikitolewa moyo, figo, maini na mapafu huko paradise nitaaishi vipi?
au
hakuna maisha tena baada ya kifo?
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Ni wazo zuri ila Siliungi mkono,
Hii Ni sawa na uhamasishaji wa biashara haramu ya viungo.
Mtasababisha watu waanze kutekana na kunyofoana viungo.

Najalibu TU kuwaza
Rushwa itetembea,
Wanafamilia watavuta mpunga kwa wenye mahitaji ya viungo,
Kisha utaandaliwa ushahidi wakihuni, wanasheria wahuni n.k

matokeo yake wale wenye wagonjwa yasiyotibika kam SARATANI n.k watauawa kwa lazima kwa manufaa ya waliobaki.

Hii biashara Ni mbaya Sana.
Tunajitolea damu bure na kila mahali kuna matangazo yanakataza kuuza damu sasa wewe nenda huko hospital kama huna hela uone kama utapewa damu. Hata hili utatoa viungo bure lakini mgonjwa lazima watamlipisha hawa

Hii program nimeifuatilia kwa muda mrefu ulaya na ninapenda kuwa donor ila kwa nchi za ulaya hapa bongo hapana utabambikiwa kesi umekufa au huponi na hapa inaonesha wanaweza kukutoa ukiwa hai mradi tu uwe ulisaini. imagine corona tu watu wanahonga hela mgonjwa mwingine anaenda kuchomolewa mtungi wa oxygen unawekewa mwenye nazo.
Kama huna ndugu usiende hospital peke yako
I can imagine wafungwa watakuwa wahanga
Kiranga una mawazo gani hapa
 
Muswada huo umechelewa sana, ungeletwa wakati bodaboda ndio zimeingia wangevuna mapafu, figo, moyo maini, bandama, kwa wingi sana maana bodaboda walikuwa wanjibamiza uvunguni mwa semi na vichwa vinasagika na viungo muhimu vibaki....sasa hivi wamekuwa hodari sana! (nimeandika muandiko wa jf)
 
Mmewasahau wanyonya damu miaka 90 kuendelea 94 ikakoma baada serikali kuweka mswada mpya was kujitolea damu ,wengi walikufa Sana hasa wakina mama na wadada na vijana mungu azilaze roho za marehemu mahalo pema peponi amen.
Kumbe hili jambo lilikuwa kweli? mwaka 83, 84 tulikimbilia sana polini kila tukiona gari lenye msalaba mwekundu!
 
Kuna wagonjwa wa ajali wengi wanapelekwa hospital zetu hizi.

Hawana ndugu Wala jamaa wa kuwauguza, wanaugulia hospitali miezi na miezi.

Hii biashara ikiruhusiwa,
Watu wengi wa Aina hii wengi watapotezwa maisha,

Matajiri wengi watatumia Nguvu ya pesa kupata viungo kutoka kwa ndugu zetu hawa wa bwelele.

Na hawatakua na mtetezi.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mmewasahau wanyonya damu miaka 90 kuendelea 94 ikakoma baada serikali kuweka mswada mpya was kujitolea damu ,wengi walikufa Sana hasa wakina mama na wadada na vijana mungu azilaze roho za marehemu mahalo pema peponi amen.
Duuuu nakumbuka hii.kumbe iliishiaga hivi
 
Back
Top Bottom