Wizara ya Afya: Mloganzila si karantini ya wagonjwa wa corona, Tanzania hakuna mgonjwa wa virusi hivyo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mloga 2.jpg

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema Hospitali ya Mloganzila haijatengwa kuwa karantini ya wagonjwa watakaobainika kuwa na virusi vya corona na kwamba hadi sasa nchini hakuna mgonjwa wa virusi hivyo.

Akizungumza na Mtanzania Digital, kuhusu ujumbe uliosambaa mitandaoni kuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameiteua hospitali hiyo kuwa karantini ya wagonjwa hao, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Serikali wa wizara hiyo, Idara Kuu ya Afya, Gerald Chami, amesema ni uzushi.

“Hakuna kitu kama hicho. Hakuna mgonjwa wa corona si Mloganzila tu bali nchini kwa ujumla.

“Waziri amezungumzia kuhusu corona kuwa watu wawe na ufahamu na wachukue tahadhari, lakini hajazungumzia Mloganzila wala wagonjwa wawili wa corona kama inavyosemekana.

“Amezungumzia kuwa kila halmashauri itenge maeneo kwa ajili hiyo kama tahadhari ikitokea kuna tatizo kama hilo, ingawa hadi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa corona nchini,” amesema Chami.

Chanzo: Mtanzania
 
Hiyo link Mbona haipo?

Kiukweli ni gonjwa linalowaandama zaidi wazee especially kuanzia miaka 70, pamoja na wale wenye matatizo katika mfumo wa upumuaji nk.

Tanzania inaweza isifikie kubaya sana kwasababu wengi wa raia(nadhani zaidi 90%), ni vijana wa kati ya miaka 18-30 kama sikosei.

Kwa upande wa marekani, population yao kubwa ni wazee(baby boomers), na ndiyo maana waathirika wako wengi zaidi especially kwenye nursing homes ambazo zinakuwa special kwa wazee nk. Idadi kubwa ya waliopeteza maisha walikuwa nursing home iliyoko Washington.

Halafu kuna wale wanaoamini kuwa waafrika tuko immune! Ndo maana kuna wanaoulizia endapo hao wawili waliokutwa na covid19 kama ni weusi ama wahindi au wachina. Nadhani huu ni uzushi, hivyo usijidanye kwasababu wewe ni mweusi basi utapata corona. Ni vyema kufuata ushauri wote.

Cha muhimu usiguse uso wako baada ya mizunguko, hakikisha unanawa kwa maji na sabuni si chini ya sekunde ishirini. Kama unashindwa kufahamu sekunde ishirini zinavyopita, unaweza kuimba wimbo wa alphabet(a, b, c, d...z) hadi mwisho sekunde ishirini zitakuwa zimeisha.
 
Naona wameamua kufunguka, ila hatugopi COVID-19, we are better than that!!!
 
Sitashanagaa hilo likitokea kwani tumeacha watu woteke na kuingia nchini kama hakuna tishio la huu ugonjwa duniani.

Hata hivyo,hii inaweza kuwa ni mbinu ya kuhamisha attention kuhusu issue ya viongozi wa CHADEMA waliokamatwa na wanaoendelea kukamatwa.
 
Tunatishana sana au ni Njia ya kututoa kwenye kujadili suala la Viongozi wa CHADEMA.

Fanya haya ili usikupate au kuongeza kinga yako.

1. Kunywa maji mengi ila siyo ya baridi.

2. Kula vitu vyenye Vitamini A kwa wingi kama Matunda

3. Epuka msongamano, kushikana na watu na pia kushika sehemu hovyo hovyo

Hizi ni baadhi tu.
 
dawa yao ni kuwakimbiza kimbiza tuu hao mburukenge, maana hawajui majukumu yao
 
Back
Top Bottom