Wizara ya Afya inafanya nini kuhusu maradhi haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Afya inafanya nini kuhusu maradhi haya?

Discussion in 'JF Doctor' started by Wamnetu, May 21, 2012.

 1. W

  Wamnetu Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo naomba nitoe dukuduku langu kuhusu Wizara ya Afya. Ninaamini kuwa tulio wengi tumeshafiwa na ndugu na jamaa kutokana na maradhi ya Kisukari na/au Shinikizo la damu (Blood pressure), na watu wengi wanaendelea kupoteza maisha. Ndio maana nimeona niulize kama wizara husika inafahamu tatizo hili na kama inafahamu, ni mikakati gani inayobuniwa kupambana na maradhi haya?
  Nimeona katika nchi nyingine mara tu mgonjwa anapofika kwenye zahanati/kituo cha afya, miongoni mwa huduma ya awali anayopata ni kuhojiwa kama ana tatizo linalohusiana na maradhi haya (Diabetes or Blood sugar). Baada ya hapo mhudumu mhusika/muuguzi atachukua vifaa vyake na kukupima kabla ya kuonwa na mganga (hii wenyewe wanaita screening). Sasa hapa kwetu tunashindwa nini kufanya hivyo na misaada tunapata teletele? Je, kuna elimu gani inayotolewa kwa umma kuhusu magonjwa haya ambayo wataalam wanayaita 'silent killers?'
  Ni kweli kuwa nyama ya mbuzi/ng'ombe iliyonona ya kuchoma ni tamu sana mdomoni, lakini je, madhara yake mwilini tunayajua? Ni kawaida mtu akienda kwenye bucha kuwa atachagua nyama iliyonona kama kidari au nundu, nk., lakini je mtu huyo aneelimishwa kuwa hiyo mboga aliyochagua inaweza kumsababishia cholesteral mwilini asingeweza kufanya uamuzi utakaomsaidia yeye na familia yake kuishi maisha bora (healthy Life style)? Inasikitisha kuwa tuna taasisi ya chakula na lisha na idara mbalimbali katika wizara ya afya lakini hakuna maendeleo katika kuelimisha umma! Bado utakuta jamaa zetu Wachagga wakipika mtori ni lazima uwekwe "futa!"
  Tufanyeje ili wizara yetu iweze kutupatia huduma tunazostahili?
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye kuchagua nundu na kidari uwiiiiiiiiiiiiiiiii umenigusa
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu unaomba jamvi msibani.Nakupa pole.Kama unajua visababishi vya magonjwa uliyoyataja utagundua kwamba yanazuilika.Lakini visababishi hivyo ndizo biashara za wakubwa.Sasa wizara ya afya ina ubavu wa kusindana na wakubwa.Surely no.Kwa hiyo tunaendelea kufa pole pole.Tena sio magonjwa hayo tu,na mengine mengi.
   
 4. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Kwa hakika. Magonjwa aliyoyataja hayapaswi kuwa kabisa ni magonjwa yanayotesa watu wengi kiasi hicho, lakini kama ulivyosema, suluhu ya magonjwa hayo na mengine mengi kama ulivyosema na hata ukimwi wenyewe, ni dogo sana. NI ELIMU TU. Lakini kama ulivyokiri, ni vigumu sana UKWELI KUIZIDI HELA (money is more stronger than the truth). Kwa sababu hiyo niliamua kutengeneza tovuti, http://maajabuyamaji.net/ inayoeleza ni namna gani kwa kutumia maji tu ya kunywa, unaweza kujitibu na kujikinga na magonjwa karibu yote, shukrani kwa dr.F.Batmanghelidj! Sasa tutafanyaje? Mungu mwenyewe ndiyo anajuwa. Hela bana!
   
Loading...