Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 1,699
- 3,350
Hapo miaka ya nyuma kulikuwa na juhudi kubwa na za wazi za kuelimisha kuhusu HIV/AIDS.
Lakini kadiri muda unavyozidi kusonga juhudi na jitihada hizi ni kama zimeendelea kufifia kwa spidi kubwa kama sio kutoweka kabisa, na kama juhudi bado zipo, basi hazijawa za uwazi na kina kama ilivyokuwa hapo nyuma.
Kwa sasa nafasi ya kuelimisha imeachwa kwa wanafamilia na wananzengo wenyewe kuonya vijana wao kuepuka tabia na mienendo hatarishi inayoweza kuwaingiza kwenye hatari ya maambukizi.
Nje ya familia elimu nyingi ipo huko mitandaoni kupitia waelimishaji binafsi. Kwa kupitia njia ya mitandao wahusika huwafikia watu wengi zaidi hasa vijana maana hao ndio watumiaji wakuu.
Lakini tukumbuke njia hizi za uelimishaji bado una ombwe kwa kuwa si lazima ufanywe na mtu mwenye utaalam wa mambo ya afya. Mtu yoyote tu anaweza akajirekodi akaposti kwenye mtandao. Kwa maana ingine, kama wizara imeona huu ndio mwelekeo sahihi, basi hapana budi kujenga uwezo wa wahusika ili elimu wanayotoa iweze kuwa uthabiti na isiyoacha shaka.
Kutokana hali hii watu walio wengi hasa hawa vijana mabarubaru wengi wao hawana elimu na ufahamu wa kutosha kuhusiana na ugonjwa huu kiasi cha wengi wao kuuchukulia poa kiasi cha kujiingiza kwenye mienendo hatarishi inayowaweka kwenye mazingira ya kupata maambukizi.
Kwa kiasi fulani hali hii inachangiwa na elimu hizi za mitandaoni zinazotolewa pasipo udhibiti. Elimu inayotolewa humfanya mhusika kuamini kuwa HIV/AIDS ni ugonjwa mwepesi tu na hata ikitokea amepata, basi atakunywa dawa atakuwa sawa!
Wizara husika iangalie vizuri eneo hili la elimu kuhusu HIV/AIDS kama kweli ina nia ya kunusuru taifa na vizazi.
Mnisamehe kwa gazeti.