Wizara ya Afya ikifanyie uchunguzi kipimo cha malaria mRDT

LIFE HELP

Senior Member
Nov 29, 2012
149
70
Ni mara yangu ya tatu sasa napimwa kwa kutumia hicho kipimo kipya cha haraka na kutoa majibu tofauti na baadae ukitumia cha zamani slides unapata ukweli,

Naiomba serikali kwa haraka zaidi ifuatilie jambo hili, kwani ni hatari sana unaweza kuambiwa huna malaria, kumbe unayo na hali ni mbaya kuhatarisha maisha.

vipimo hivi vipo kwa wingi sana Dar hata mikoani.

TANZANIA iliamua kutumia kipimo kipya cha kugundua vijidudu vya Malaria kwa haraka kijulikanacho kama Malaria Rapid Diagnostic Test (MRDT), na kuamua kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2013 kiwe kimesambaa nchi nzima. Kipimo hiki mara kadhaa kimeibua maswali ya muda mrefu yasiyo na majibu ikiwemo kifaa hicho kutofika katika maeneo mengi nchini.

Kumbukumbu za FikraPevu zinaonyesha kuwa awali Shirika la Afya Duniani, World Health Organization (WHO) lilipendekeza kuwepo kwa uthibitisho wa vipimo vya malaria kabla mgonjwa hajapewa tiba katika upimaji wa damu ili kubaini vidudu vya malaria badala ya kutumia kifaa cha darunini ambacho kinachukua muda mrefu kutoa majibu kwa kuhitaji mtaalamu anayeweza kutambua vijidudu hivyo kupitia mashine hiyo.

SWALI: Kipimo cha haraka cha kutambua malaria, maarufu kwa jina la kitaalam kama mRDT, ni kitu gani?

JIBU: mRDT ni kipimo cha haraka ambacho hutambua malaria kwa kutoa uthibitisho wa kuwepo kwa antijeni (visisimuzi fingo) za vimelea vya malaria kwenye damu kwa muda mfupi, ndani ya dakika kati ya 15 na 20.

SWALI: Kuna aina ngapi za kipimo cha mRDT?

JIBU: Kuna aina mbili kuu za kipimo cha mRDT zinazotambua uwepo wa antijen za vimelea vya Malaria. Aina ya kwanza, ni maalum kwa kutambua antijeni za vimelea vya P.falciparum peke yake. Mara nyingi, kipimo hiki huweza kuzitambua pia antijen za aina ya Histidine-rich protein 2 (HRP2). mRDT za kundi hili hujulikana zaidi kwa jina la P.falciparum mRDT (P.f mRDT) au HRP2 mRDT.

Aina ya pili ya mRDT, hutambua antijen za vimelea vya malaria zaidi ya aina moja. Kitaalamu hujulikana zaidi kwa jina la Pan mRDT. Aidha, majina mengine yanayotumika kutambulisha mRDT ni mahususi kwa shughuli za kibiashara na hutumiwa zaidi na makampuni au mawakala wa biashara.

SWALI: Kipimo cha mRDT kinaaminika kwa kiasi gani?

JIBU: Tafiti zilizofanywa nchini Tanzania na maeneo mengine ulimwenguni, zinaonyesha kwamba uwezo ((sensitivity) wa kipimo cha mRDT kugundua kuwepo kwa antijen za vimelea vya ugonjwa wa malaria, ni kati ya asilimia 88 na 99, na uwezo wa kugundua kuwa ugonjwa huu si malaria (specificity) ni asilimia kati ya 95 na 100 (Marx-2005, Mboera-2006, Ochola-2006 & Kamugisha-2008). Hii ina maana kwamba tunapaswa kuamini kabisa majibu yanayotolewa na kipimo cha mRDT.

SWALI: Je, inawezekana kutumia kitepe kimoja cha mRDT kumpima mgonjwa zaidi ya mmoja?

JIBU: Hapana. Kila kitepe cha mRDT kinapaswa kutumika kwa mgonjwa mmoja tu. Endapo mpimaji atapata majibu yasiyo sahihi (invalid results) kutoka katika kitepe, anashauriwa kufungua kitepe kingine kipya na kurudia tena kumpima mgonjwa huyo.

SWALI: Inawezekana kupata majibu ambayo ni chanya ikiwa mgonjwa hana malaria?

JIBU: Ndiyo. Kama mgonjwa amekwisha kupata matibabu ya malaria siku 14 za nyuma, mgonjwa huyo anaweza kuonekana chanya kwa baadhi ya vipimo vya haraka vya kutambua malaria.

Kipimo kinafanya kazi kwa kugundua antijen. Sumu inayotengenezwa na vimelea wa malaria na kupatikana kwenye damu na kubaki ndani ya mwili kwa muda hata kama vimelea vya malaria vitakuwa havionekani. Kwa kawaida, HRP2 antijen inabakia kwenye damu kwa muda wa majuma mawili au zaidi baada ya vimelea vya malaria kuuawa.

Kwa hiyo basi, kabla ya kutumia kipimo cha kutambua kwa haraka vimelea vya malaria kwa mgonjwa, ni lazima mgonjwa aulizwe kama amekwisha kupata matibabu ya ugonjwa huo katika majuma mawili yaliyopita. Kama hivyo ndivyo, mgonjwa anatakiwa apimwe kwa kutumia hadubini badala ya mRDT.

Lakini pia, jibu lolote la kipimo cha haraka cha utambuzi wa malaria, ni muhimu ikakumbukwa kuwa mgonjwa anaweza kuwa na ugonjwa mwingine zaidi ukijumuisha na malaria au ni ugonjwa mwingine tofauti na malaria.

SWALI: Itakuwaje kama majibu ya kipimo cha mRDT hakionyeshi kuwepo kwa vimelea vya ugonjwa wa malaria, lakini mgonjwa akawa anasisitiza bado kupewa tiba ya ugonjwa wa malaria?

Soma zaidi | =>Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu Malaria na Kipimo cha mRDT
 
Ni rahisi sn ku2mia mRDT kuliko hadubini. Ukichukua slides 100 zilioonyesha positive zikarudiwa kwa umakin utakuweza kuta ni 60 or 70 ndo zpo positive. Sema wakat mwngne wagonjwa 2naenda pale 2kiwa tayar na iman ya malaria ze2 kichwan ukiambiwa negative unaenda kwa mwngne unamwambia nime2mia mRDT sehemu imekataa czamini, yeye atatumia hadubin na atapenda kukupa majibu uyapendayo hususan kwa hosptal bnafsi.
 
mrdt is effective sema wagonjwa wengi wankuja hospitali tayari wakiwa wanaamini wana malaria.hizo dalili za malaria ni common kwa magonjwa mengi sio malaria tu.wataalam wa kutumia hadubini effectively ni wachache wengi wao wanaandika tu idadi ya parasites bila hata kuwaona
 
ZIPO TAFITI ZA MWAKA 2005 HADI 2006 ZILIZOONESHA MPAKA 95% za postive malarial blood slide zilikuwa false postive. Na hiyo ni moja ya sababu za kuleta mrdt.
 
mrdt is effective sema wagonjwa wengi wankuja hospitali tayari wakiwa wanaamini wana malaria.hizo dalili za malaria ni common kwa magonjwa mengi sio malaria tu.wataalam wa kutumia hadubini effectively ni wachache wengi wao wanaandika tu idadi ya parasites bila hata kuwaona

kuna wale wa malaria 2 kwa kila apimie
 
ZIPO TAFITI ZA MWAOA 2005 HADI 2006 ZILIZOONESHA MPAKA 95% za postive malarial blood slide zilikuwa false postive. Na hiyo ni moja ya sababu za kuleta mrdt.
 
Wapimaji hospitalini wengi hawapimi, hasa kubwa za serikali, wanakadiria tu mf. Watatu malaria, wawili typhod, mmoja kichocho, wanaanza upya.

Jaribu siku moja uende hospitalini chukua vipimo usinywe dawa, nenda hospali tatu tofauti, kila hospitali jifanye ni mara ya kwanza, nakuhakikishia kila hospitali watakwambia ugonjwa tofauti
 
MRDT ndo kipimo sahihi cha malaria...blood slide hakuna kitu...istoshe wataalamu wachache sana wanaoweza kutumia microscope kwa usahihi... utaishia kumeza dawa za malaria kumbe hata malaria hauna.....
 
Back
Top Bottom