WIzara ya afya haitaki madaktari....Sikia haya!

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
-Serikali inaomba kuajiri jumla ya wataalamu/wahudumu wa afya 9,391. Kati ya hao wote madaktari, bingwa na wale wa kawaida wanaohitajika ni kama 300 (3.2%) tu.

-Wilaya na manispaa nyingi hazijaonyesha uhitaji wowote wa madaktari, wanahitaji clinical officers na Assistant medical officers-AMOs wasiopungua
elfu mbili.

-Sokoni tuna madaktari wa tiba MD na meno wasiopungua 700 ambao hawana ajira bado wanazungushwa!

-Hawa wengine wote 400 waende wapi? Je ni kweli kuwa nchi hii haihitaji madaktari kihivyo??

-Vyuo vingi vimefunguliwa ili kupata madaktari wa kutosha waende kwenye hospitali za mikoa ambazo zimeitwa za rufaa..Sasa kila mwaka(kuanzaia mwaka jana) angalau madaktari 500-600 wanamaliza shule, Je waende wapi kama Wizara haitaki kuwaajiri??

TAFAKARI...CHUKUA HATUA!!
 
Hii serikali yetu inapenda sana cheap labor afu inawaweka watu wasio na uwezo wenye uwezo wanazunguka na bahasha mtaani, mm nilipo hapa Sina kazi na ni Dr Md nimemaliza intern sijui nitapata nafasi yenyewe kama nafasi zenyewe ni 300: any ngoja nijipe matumaini nitashinda.
 
halmashauri zina matatizo sana !utakuta halmashauri haina watumishi lakini hawaombi kuletewa watumishi kutoka central goverment matokeo yake wanajaza watumishi wasio na sifa stahili.miaka 50 ya uhuru ni aibu kukuta AMO katika hospitali ya mkoa jamani.
nashauri wizara ya afya ifanye ukaguzi wa watumishi walioko kwenye vituo vyake vya afya na imuajibishe RMO,DMO ambaye hana wataalamu wa afya halafu hajaomba kupatiwa.
 
halmashauri zina matatizo sana !utakuta halmashauri haina watumishi lakini hawaombi kuletewa watumishi kutoka central goverment matokeo yake wanajaza watumishi wasio na sifa stahili.miaka 50 ya uhuru ni aibu kukuta AMO katika hospitali ya mkoa jamani.
nashauri wizara ya afya ifanye ukaguzi wa watumishi walioko kwenye vituo vyake vya afya na imuajibishe RMO,DMO ambaye hana wataalamu wa afya halafu hajaomba kupatiwa.

RMO au DMO ataajiri kwa kulipa nini wakati Halmashauri haijatengewa Budget hiyo? Halimashauri huomba lakini kule Hazina hakuna kitu je wao RMO/DMO Watawalipa hao Doctors kutoka kwa......"Masauli" yao?

"Wilaya na manispaa nyingi hazijaonyesha uhitaji wowote wa madaktari, wanahitaji clinical officers na Assistant medical officers-AMOs wasiopungua
elfu mbili."

Kumbuka kuwa hao kwa utaratibu wa sasa wa Wizara ya Afya wanatakiwa wakahudumie Health Centres na Dispensary vijijini ambazo ni nyingi na namba hizo mlizoweka bado hawatatosha vijijini

 
safi kabisa. tatizo tukiwaajiri siku mbili tu wanakimbia acha wakae bench tu. sisi hatufi ngo labda ndege zisiruke tena kwenda nje? apo vip
 
tatizo haliko kwa wizara ya afya bali ni mamlaka za wilaya na mikoa hawataki watu wenye degree au masters si unajua wanaoshikilia vitengo ni dalasa la nne wa zamani
 
Back
Top Bottom