Wizara kutumia mfumo wa kidigitali kuondoa migogoro ya Ardhi nchini

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
WAZIRI wa ,Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Dkt Anjelina Mabura, amesema wizara hiyo itatumia mfumo wa Digitali katika kuondoa migogoro ya ardhi nchini ili kuimarisha mfumo wa usimazi na kuwepo Ufanisi wa utendaji

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili cha watendaji wa wizara hiyo,makamishina wa ardhi nchini na maafisa ardhi wa mikoa na akawataka wakurugenzi wa wizara hiya kufuatilia utendaji kwenye halmashauri ili kuwepo na mfumo sahihi wa upatikaji wa taatifa

Amewataka wataalamu wa wizara hiyo kuhakikisha Kwamba miji yote inapangwa ili kuondoa ujenzi holela ambao unajitokeza kwenye miji yote inayochipua lengo urasimishaji usiendelee

Mabula,amesema ujenzi holela una mchukiza hivyo mipango miji wahakikishe kunakuwepo maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kupanga miji.hivyo akawataka wasimamie sheria ili kuondoa ujenzii holela na viwanja ambavyo havijaendelezwa wamilike wake waviendeleze

Amesema makampuni mengi yaliyoingia mikataba ya urasimishaji yameshindwa kuendelea kutokana na migogoro ya ardhi kuwa mingi hivyo wizara itashirikiana na halmashauri na kuagiza bodi ardhi kuchukua hatua ya kufuta usajili wa makampuni hayo yaliyoshindwa kufanya kazi kwa kuwa wananchi wametoa fedha zao kwa ajili ya urasimishaji lakini hawajapata hati

Amesema mpango wa urasimshaji ulikuwa wa miaka Kumi na unafikia mwisho mwaka 2023 hivyo wizara inashirikiana na benki za NMB,CRDBna TCB, kushiriki katika mpango wa urasimIshaji makazil lengo ifikapo mwaka 2023 urasimIshaji usiwepo nchini

Awali mkuu wa mkoa wa Arusha john Mongela,akitoa Naaaha zake amesema ardhi ndio msingi wa kila kitu na ni nyeti hivyo akaishauri kutengwa meaneo ya uewekezaji kwa kuwa kuna dalili kama yasipotengwa yatakuja kuwa na migogoro kwa kuwa kila sehemu wawekezaji wakifika watakuta ni meaneo ya watu

Katibu mkuu wa wizara ya Ardhi,Dkt Allan Kijazi,amesema hicho ni kikao kazi cha watendaji cha siku mbili ni mwendelezo wa vikao vya kila mwakaili kufanya tathimini ya utendaji wa wizara , mikoa na halmashsuri nakuweka mkakati ili kiongeza tija na uwajibikaji

Amesema changamoto iliyopo ni kutokufikiwa kwa malengo ya ukusanyaji wa mapato ya kodi ya ardhi ambapo ni mikoa 10 tu ndio imevuka ukusanyaji kwa 50

Ends..


IMG-20220225-WA0018.jpg
 
Cha kusikitisha ni kwamba hii Wizara hutoa matamko na mikakati mingi lakini hakuna lolote la maana linalotokea. Mwaka jana wakati wa kipindi cha Sherehe za Sabasaba wakazi wa Mkoa wa Dodoma walitoa maelezo yao kuhusu kero za masuala ya Ardhi.

Utitiri wa wafanyahazi wa Wizara hiyo walikuwepo hapo pamoja na vifaa vyao vya kidijitari, wakawapiga picha na kumpa namba kila aliyehudhuria na kuahidi kutatua kero hizo ndani ya mwezi mmoja.

Kauli mbiu yake maarufu ilikuwa "Dodoma bila kero za Ardhi inawezekana". Leo hii zaidi ya miezi sita ni asilimia chache sana ya waliohudhuria ambao wamepata suluhu ya yale waliyolalamikia.

Sana wanaishia kuletewa taarifa za kidijitari kwenye simu zao kila baada ya mwezi kwamba "Ndugu kero yako namba XYZ tumeipokea na tunaifanyia kazi". Kumbuka ni miezi zaidi ya sita na BADO wanalifanyia kazi!
 
Back
Top Bottom