BabM
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 1,166
- 956
Katika hali isiyo ya kawaida katika chuo nnachosoma katika moja ya nchi zenye hewa safi profesa mmoja amemchinja mhadhiri mwandamizi kama kuku. Ilıvyokuwa: katika kitivo hicho kama miezi saba ilopita kampuni inayosimamia usafi chuoni hapo ilimleta mwanadada kama msimamizi wa wafanya usafi wote wa hapo kitivoni. Inasemakana kwamba mhadhiri alikuwa akirusha roho na dada huyo kwa wakati wake na profesa naye alikuwa akipata fungu lake la mapenzi kwa wakati wake. Profesa huyo ambaye ni mkuu wa kitengo pia alikuwa anafanya kazi na mkewe hapohapo kitivoni ambapo mke alikuwa ni mkuu wa kitivo. Inavyoonekana profesa alijua kwamba bwana mdogo ( mhadhiri mwandamizi anashare naye mchepuko) hasa baada ya mhadhiri huyo kumwacha mkewe baada tu ya msimamia usafi kutua kitivoni. Siku ya tukio bila kuonekana profesa aliingia ofisi ya mhadhiri mwandamizi na huko ndipo alipomkata shingo bila ya wafanyakazi wengine kujua. Baada ya mauaji alifunga mlango kwa nje na kuzika funguo. Siku hiyo jioni wakati anaenda nyumbani na mkewe(Mkuu wa kitivo) alishtuka kidogo kuona nguo za mume zina madoa kama ya damu ambapo alipohoji aliambiwa ni kemikali zimemwagikia. Inasemekana kufika nyumbani baada ya mke kuzidi kuhoji profesa alisusa nyumba na kwenda kukaa hotelini. Mwili wa marehemu uligunduliwa siku ya tatu baada ya tukio ukiwa umekata koo. Baada ya polisi kuwasili na kujaribu kuhoji waalimu na wafanyakazi profesa alianza kubabaika na kutetemeka jambo lililofanya akamatwe. HUko rupango profesa alikiri kuuua kwa sababu ya wivu wa mapenzi. Profesa huyo baada ya kuua alimpigia mchepuko wake ukamfuata hotel ambapo alimweleza kuwa keshaua na alikuwa anataka mchepuko umpe pesa kidogo kwani alikuwa ameishiwa na ndani ya muda waliodumu alikuwa ameshampa zaidi ya milioni 50 za tz. Mke wa profesa hakulaza damu wiki hıyohıyo akachukua talaka yake. Haifahamiki mara moja mume wa mchepuko/dada huyo atakuwa amechukua hatua ganı. Mchepuko huyo alikamatwa na polisi lakini baadaye aliachiwa baada ya kuonekana hana hatia kwani kutembea na mume wa mtu sio kosa katika nji hii. Kweli dunia imekwisha yaani mtu ana wivu mpaka na mke wa mtu. Magazeti yameminyana sana kupata picha ya binti huyo ili wajue ni mrembo wa kiasi ganı lkn polisi wamezuia kabisa jaribio la picha.