Wivu wa mapenzi: Je, ni sahihi wapenzi kufuatiliana mawasiliano ya simu?

Donkere91

Senior Member
May 28, 2016
185
155
Wadau naomba mawazo yenu ktk hili...

Je ni sahihi mpenzi wako kufuatilia kwa siri mawasiliano yako ya simu kupitia rafk yake mweny access hyo ktk ma kampuni ya mawasiliano...na je ukijua kafanya hvo uta chukua hatua gani??

Na kama je mpenzi wako ndio mweny hyo access na ukajua amekua akifuatilia mawasiliano yako utafanya nn!?


(Vp kama kitendo hiko kikapelekea mkaachana?)
Mawazo yenu plz.....
 
Hakuna kitu kizuri kama uhuru na kuaminiana.... Hakuna kitu kinachokera kuchafuana kukasirisha kama mnafuatiliana kwa style hiyo..

Maana yake kwamba hamuaminiani... Na binadamu hachungwi anajichunga mwenyewe...


Hapo uaminifu zero... Kamwe hamuwezi kudumu na ni kasoro mbaya sana...
 
Sio sahihi hata kidogo.
Lakiniiii unapohisi kitu tofauti kwa mda mrefu utalazimika kufanya hivyo maana mmmh!
Ukiona mwanaume hata chooni simu anayo kuwa makini chukua hatua.
 
We kama umeichoka amani anza kufuatilia mawasiliano ya mwenzako, kama siku nyingi hujaumwa walau presha fuatilia mawasiliano ya mwenzako.
Kama ni mwaminifu ni mwaminifu tuu na kama amekubuhu amekubuhu tuu
 
Kufuatiliwa pie, wapenzi wengine waongo waongo sana. Unaweza kuwa umejizatiti kwake kumbe yeye hana mpango anakufuja tu. Na kingine sioni ishu kama mpenzi wako akidukua mawasiliano yako ilihali huna la kuficha. Utachukulia poa tu!
 
Kama kweli wewe ni mwaminifu ya nini kificha au kutokubali kufatiliwa simu yako? Kama hauna figisu figisu hutokua na presha ata ukimwachia simu siku nzima.

Ni vizuri kumfatilia mpenzi wako kama una plan future nae so unakaa na mtu kumbe moyo wake upo kwa mwingine
 
Mmmh! Hapo pagumu. Badilisha mtandao mkuu ili ashindwe kukufatilia. Ila siri kwenye mapenzi za nini? Inatakiwa mtu uwe huru ata ukisahau simu nyumbani pressure isipae.
 
Kama hutaki kufuatiliwa basi ww si muaminifu,kama humpendi mwenzio muache aende usimpotezee muda,kuchunguza ni njia moja wapo ya kuongeza mapenzi kati yenu na kumtoa dukuduku mwenzio!! Inapendeza kila mmoja kuwa na uhakika na penzi la mwenzie na inaleta raha na kudumisha mapenzi ya kweli na kuyavunjilia mbali mapenzi ya uongo!! Mulika mwiziiii! in Kidumus voice
 
Back
Top Bottom