Wivu umeniponza

Wivu umeniponza

Duh, pole mkuu, mshukuru mungu kakuepushia na huyo shetani, wanawake wapo kibao, ila ili usimuwazie sana,tafuta mwingine and get close to her. Huyo utamsahau tu

invest what you are willing to lose
 
Lakini mkuu.....
Unajua nimejikuta nawaza sana baada ya kurudia soma huu uzi mara kadhaa.....
Nimegundua kwamba ulipaswa uandike heading kwamba, UJINGA UMENIPONZA badadala ya WIVU UMENIPONZA.
Ila pole sana mkuu...
Nimtazamo tu
 
Kila siku nasema siku zote wenye mapenz ya dhati huishia maumivu mapenz ya dhati yanatoka moyoni mwaaliekuridhia huyo alikutamani kwa maslahi yake ila Mungu yupo atakusaidia mapenz ya dhati sio pesa karibu chama cha u single team

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapenzi yakizidi hupunguza uwezo wa kufikiri ( quoted).....muulize hata mtoto wa miaka kumi atakupa jibu kua wewe ni makinikia ya akashia
 
Wadau wa JF jukwaa lililosheheni wajuvi wa mambo,

Niende kwenye mada,

Nina mpenzi wangu ambae hadi leo kaniacha ni miaka miwili na miezi sita sasa, tangu tufahamiane nilimpenda Bi dada huyu kwa mapenzi ya dhati, alikua akiishi kwao lakini nikamuwezesha kupanga chumba na kumfungulia biashara iliyokuwa na mtaji wa tsh 4.5m ili aweze kuendesha maisha yake na wanae alioachwa nao, niliweza kulipia chumba kwa mwaka.

Kila kodi ilipokwisha bili ya umeme na maji nilipia, chumba cha biashara pia kila kodi ilipokwisha nilihudumia, matibabu kwa mpenzi wangu na wanawe pale walipougua niliweza, kumpa fedha kwa ajili ya fanicha za ndani kwa kadiri ya mahitaji ya msingi bila kujali nilikua radhi kumgawia yeye nusu ya kipato changu ili akidhi mahitaji yake lakini wivu wangu kwake umeniponza.

Bidada huwa anapokasirika hachagui neno la kuniambia hata ikiwa yeye ndiye mkosaji anakasirika, hii inapelekea mimi kujishusha na kumuomba yeye radhi yaishe japo kosa ni la kwake, amekua hapendi kuulizwa maswali japo huwa namuuliza kwa upole na nia ni kulipa afya penzi letu, moja ya maswali yangu asiyo yapenda huwa napenda kila Mara kujua yuko wapi na anafanya nini nikiwa na wasiwasi nikitaka kujiridhisha hapo atanijibu kama huniamini achana na mimi mi najiamini na sio malaya, ni majibu ambayo ukweli huyatoa kwa ukali.

Hali ambayo imekua ikinisikitisha, kisa sasa cha kuachwa ni kodi ya nyumba imekwisha ya huu mwaka, nami hali yangu kiuchumi sio nzuri nikamuomba anivumilie nimtafutie lakini hakunielewa amepunguza mawasiliano kama ilivyokua kawaida yetu kupigiana simu Mara nne kwa siku kwani siishi nae huwa nikitaka kwenda kwake ni hadi nimpe taarifa.

Ndugu zake asilimia kubwa wananifahamu kuwa mi ndio namlea ndugu yao lakini Jana usiku nilimpigia simu baada ya kuwa nzima kupita bila mawasiliano nikiwa kuna mtu kanitonya kuwa bidada kakaa baa na mtu anakunywa bia mi kumpigia nikamsalimia nikamuuliza yuko wapi, akanidanganya nikakwambia vuka barabara tuonane akaniambia sawa, dk chache akanipigia mbona sikuoni nikakwambia sipo pale lakini kuna mtu akaniambia umekaa na mtu baa akaniuliza ninani sikumtaja akasema nikimjua atanitambua.

Kwani kukaa na mtu wa kiume ndio nikalale nae mimi najitambua nikakwambia naomba kukutana nawe, akaniambia kwa hasira hutanikuta wala sikuhitaji huna msaada kwangu wewe ukipigiwa simu na mtu unapaniki na kunihisi kama polisi, mimi sitaki huo ujinga na kama unadhani mimi ni malaya basi kuanzia leo futa namba yangu na usinitafute tena aniache na maisha yangu.Tangu nikuombe kodi umekuana visavisa kata mawasiliano na mimi.

Wana JF mimi sikumjibu lolote zaidi ya kusema asante, bidada nampenda sana uchumi wangu umeyumba lakini kwa maneno alionitamkia nimebaki njia panda biashara yake niliompa mtaji umekata.

Naomba ushauri wenu kwani nahisi kuchanganyikiwa jinsi nilivompenda lakini wivu wangu kwake umeniponza, nifanyeje wana JF nisaidie ushauri.
Hapo unapoteza Muda wako Bure masikini ya Mungu.

Achana na huyo Mwanamke.
Sio type yako.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakupendi hata kidogo hata chembe tena hayuko na wewe tu...mwache atakutafuta....ila kwa upendo hana
 
Kwanza pole sana lakini pili ni muhimu kujifunza, humu huwa kuna visa kibao tu vinaletwa hasa MAHUSIANO NA SINGLE MAZAZ lkn kwakuwa nyie vijana wa leo na wanaume ambao masikio yameziwa kwa nta ya uchafu wa masikio yenu hamsikii hiyo ndiyo dawa yenu, Why dating a single mother? why cant you find a simple lady, young and lovely and enjoy the life with her? au ndo ule msemo single mazaz hawawez fanya ujinga wanajua maisha maana walishapigika? Acha hizo jombaaaa Mistresiiii mnajitia wenyewe KUBALI MATOKEO kisha move on with your life nothing else. ALL THE Best bro
 
Ningependelea JF kile kitufe cha like kiwe na options nying ka fb hv....hapa badala ya kubofya like nltakiwa nbofye sad...nkupe pole mkuu kwa kupoteza muda wako adhimu na pesa zako kwa mwanamke asokupenda na kukuheshimu...
Mungu kakuepusha na majanga....pambana uweke mambo yako sawa (financially).
Move on with ya life bro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah aisee! Inavyoonekana wewe bado ni kijana.

Hakukupenda huyo ila hukumgundua mapema bila shaka ulimuingia kwa gia ya pesa,

ukajifanya unatoa sana hela akaona asipoteze nafasi alichokuwa anakifanya ni kukutumia tu.

Ndo akaamua kukupa hayo masharti na inawezekana hata papuchi ulikuwa unapata kwa ratiba.

Hakuwahi kukupenda ila ni kwa sababu ulijifanya una 'kiherehere' cha kutoa hela ndo akaamua akukubalie ili azile!

Na usingeyumba kiuchumi ungeipata pata!

Ni funzo hilo.

Thamani yako ni kubwa. Jithamini, mpotezee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee wewe jamaa umenisikitisha sana huduma zote hizo kwa mtu alieachwa??. Halafu bado unajilaumu huo haukua wivu ni haki yako kujua alipo eeeh.. Angalia mbele.

Xmass Boy.
 
Duuh we kweli zwazwa lol...ila pole.

Kosa ulilofanya ni kumpenda sana mtu ambae hana mapenzi na wewe SIO WIVU,unatakiwa kuwa makini kuhakikisha kwamba hilo penzi lenu lipo kote (mutual) sio upande mmoja tu,sasa ww ukakurupuka kuinvest pesa nyingi na muda wako kwa hyo kiumbe asie kupenda alafu mbaya zaidi mpka sahiv ulikuwa hujui kwamba hana time na ww kabsa kwa kufikiri kakuacha sababu ya wivu haha...

Achana na hyo mwanamke mzee alafu usipende kuwanyenyekea sana hawa viumbe unakuwa kama fala bwana,we kusanya kilicho chako sepa zako na number yake futa kabsa,wanawake wako kibao sana tafuta bi dada alie tulia,anaekupenda na kukuheshimu, maisha yatakunyookea fresh tu!
 
suala la uchumi halijawahi muacha mtu salama. Wale ma don wa jk leo wanapigwa chini. Ngoja nijipange na ka vitz kangu nkamng'oe anti

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Back
Top Bottom