Mara nyingi ndivyo ilivyo, kuwa unalipia kodi ya chumba/nyumba, biashrara umemfungulia, gari umemnunulia lakini bado kuna Msaidizi wako. Hapo wala usiwe mkali, endelea naye tu maana hata wewe ni mwizi hapo, huenda aliye kuwemo ndani ndiye mume mtarajiwa naye analipia hicho chumba na biashara kamfungulia.
Mkuu umeongea pointi maana sasa hivi pesa ni ngumu sana halafu michepuko inazingua ila nimejifunza kitu kupitia hii issue mkuu.Mwizi anapoibiwa....!!
Mkuu nadhani kinachokuuma sio kugongewa ila ni jinsi pesa ilivyo ngumu afu mchepuko anaitumbua apendavywo
Mkuu nahisi kwa sababu mimi ndiye ninayemlipia hela na ya ile pango katika nyumba anayoishi na biashara ya duka nimefungulia .Lakini bado analeta kidume kwenye hiyo nyumba na kitanda nilichonunua mimi nahisi ndio kitu kinachoniuma roho.Unamuonea wivu mchepuko kwa lipi labda?au wameisha?sijawai kumuonea mchepuko wivu wala kujiona mjinga..!
nyie mnatulia??Ndo malipo hayo... Tulieni na wake zenu
Mkuu umenongea pointi nitajitathimini tena nijue wapi nilikosea ili nianze upya.Duuuhh kazi kweli kweli, mtenda akitendewa.
Kinachokuuma ni kile ulichowekeza kwa huyo mchepuko. Lakini pia ni dhana uliyojijengea kwa mchepuko, na dhana hiyo ni "kwa mchepuko wako ni free stress zone".
Hata hivyo ni Muda muafaka wa wewe kujitathimini. Je, kama wewe umeumia kiasi hicho na mkeo akijua una "spare tire" bila ridhaa yake ataumia kiasi gani.
NB : Pumzika au Acha mechi za mchangani.
msingi kiuno atapata mwingine.......Hapo ndio nimeshajipiga chini mkuu sirudi nyuma sijui kwa ile biashara kama ataweza kulipa kodi ya nyumba ikiisha.
Ni kweli mkuu, hawa wawili wote ni wezi, inabidi wawe wadogo kwa muda. Wayamalize kiutu uzimaMara nyingi ndivyo ilivyo, kuwa unalipia kodi ya chumba/nyumba, biashrara umemfungulia, gari umemnunulia lakini bado kuna Msaidizi wako. Hapo wala usiwe mkali, endelea naye tu maana hata wewe ni mwizi hapo, huenda aliye kuwemo ndani ndiye mume mtarajiwa naye analipia hicho chumba na biashara kamfungulia.