ninakubaliana na comment ya jamaa mmoja that "inabidi kuwe na malipo kwa kila anayetaka kuweka post hapa JF"..hivi huyu jamaa anasahau kuwa hata wakati wa kudai uhuru hali ilikuwa hivihivi?
lazima kieleweke sijiondoi chadema ngo, nilisabikia ccm toka enzi za Tanu sasa hivi zamu ya chadema, ndugu yangu hebu jaribu kufikiri ndoka miaka hamsini ya uhuru mpaka leo no changes tukipe chama cha upinzani support kiweze kuchukua dola ili tuone changamoto zake maana hata kama umefunga ndoa na mkeo ipo siku utapiga nje kuonja radha tofauti.
Imekuwa kawaida sasa kwa vijana wengi kushabikia mno CHADEMA.Hii inapelekea hata kusahau pale chama hiki kinapo boronga,wao hufumba macho na kutanguliza ushabiki mbele.
Jambo hili ni baya kwa mustakabali wa taifa letu,kwani pale ambapo CHADEMA itafanikiwa kuchukua dola,itakumbana na wakati mgumu kwani imezoea kujiona sahihi wakati wote.
Mbaya zaidi wengi wa mashabiki ni wale wasio hata na kadi ya chama,nao wanajiita wana CHADEMA.
Jambo la msingi kukumbushana ni kuwa sisi ni watanzania.Nawasihi mashabiki wa CHADEMA ni bora wakajiondoa CHADEMA na kujiona kama watanzania neutral ambao watashabikia maslahi ya taifa,na chama kinacho yatekeleza ndicho kiungwe mkono.
Hii itawawezesha kuikosoa chadema pale inapo kosea,na hivyo CHADEMA itakuwa imara na kupata nguvu zaidi.
TANZANIA:Nakupenda sana.
Mkuu tegemea matusi na kashfa nyingi sana kutoka kwa hawa pro-chadema na bado watakutukana hawa si unajua unakuta mmoja anamiliki account kumi kwa wakati mmoja hapa JF ndivyo sera za mtaa wa UFIPA zinavyosema MATUSI mbele
mkuu,ushabiki kwa vyama ulio pitiliza ni hatari kwa vyama vyenyewe,na kwa mustakabali wa taifa kwani unajenga vyama vipofu visivyoweza kujikosoa na kujisahihisha.
kuna mtu aliniquote niliposema sina chama, ukweli ukiwa neutral ndipo unapoweza kushaui na kukosoa vizuri kuliko ukiwa mwanachama.
nahimiza ushabiki wenye kutazama uzuri wa chama na kuusifu bila kusahau kukosoa ubovu pale unapo jitokeza.
This same applies kwa mashabiki wa vyama vingine.
Mkuu ulilosema lina ukweli,lakini siyo kwa pro-chadema pekee hata uvccm kuna mashabiki wasiyoambilika akina Shimwela.Hawaonekani kusimamia maslahi ya taifa kwani hawaikosoi serikali inapofail bali wanaonekana tu pale ambapo upinzani wanakosea.Na hii ni vema tukaitazama kwa jicho la tatu pasi na kunyosheana vidole eti CHADEMA pekee.Sisi vijana wa CHADEMA tukubali kukosolewa lakini tusikubali kukosolewa tunapogundua mazingira ya ukosoaji yametengenezwa!
Acha mawazo mgando, hicho chama ulicho wewe, kiweke wazi tukifahamu. Na hapo kwenye red chunga sana, hatubahatishi this time.
ninakubaliana na comment ya jamaa mmoja that "inabidi kuwe na malipo kwa kila anayetaka kuweka post hapa JF"..hivi huyu jamaa anasahau kuwa hata wakati wa kudai uhuru hali ilikuwa hivihivi?
Aliyekudanganya kuwa vijana hawana kadi za CDM amekudanganya sana! Hivi inahitajika Shahada au Diploma kufahamu nia ya CDM kwa Taifa hili! Tunafahamu wote kuwa CDM inaundwa na Watanzania wale wale waliokuwa CCM, sasa kutegemea CDM ya Malaika hapa TZ ni sawa na wendawazimu!! Nia ya CDM ni kutoa watanzania tongotongo za imani kuwa wapo watawala wa kuzaliwa na wapo watawaliwa wa kuzaliwa. kila m2 ajue kuwa anayo haki ya kufahamu na kutetea maslahi yake binafsi na Taifa kwa ujumla. tunafanyaje katika hili!? ni kupitia njia za siasa ambapo moja ya njia hizo ni USHABIKI wa wakereketwa pamoja na kuhamasisha wa2 kujiunga. Tutajirekebisha pale CDM itakapokamilisha lengo hili muhimu kwa chama cha siasa.