Wito kwa wateule wa Rais kuyaishi maono haya ya Hayati Mwalimu Nyerere

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
243
100
Mimi mtanisamehe maana bado ni muumini wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Jk Nyerere.

Nakumbuka enzi za uhai wake aliwahi kutaja mambo manne muhimu ambayo yeye binafsi aliamini tulitakiwa (na mimi bado naamini) kuyazingatia katika kusaka maendeleo yetu.

Ili tuendlee kama Taifa na hata kwa mtu mmoja mmoja tunatakiwa tuwe na Watu,Ardhi ,Siasa safi na Uongozi bora.

Kwa mkutadha wa mada hii,leo sitaongelea Watu na Ardhi japo navyo vinahitaji mjadala.

Leo nitajikita kwenye masuala ya Siasa safi na Uongozi bora.

Na haya ndio mambo ya msingi ambayo Wateule wanatakiwa kuyazingatia.

Kwa muda mrefu sasa Watanzania tumekuwa tukiendesha nchi yetu chini ya mfumo wa siasa ya demokrasia ya vyama vingi .

Aina hii ya siasa kwa kweli haijafanikiwa sana katika kuleta utulivu kwa nchi, kwani kumekuwa na makandokando mengi yaliyosababisha hata utekelezaji wa majukumu ya wanasiasa (viongozi) wenyewe kutoelewana vizuri.

Kadhalika, upatikanaji wa viongozi bora umekuwa na changamoto nyingi zilizosababishwa, kwa kiasi kikubwa, na mfumo mbaya wa namna ya upatikanaji wa viongozi katika ngazi mbali mbali.

Yote haya, kama hayatawekwa sawa,tutashindwa kuendelea kwa kasi inayotakiwa.

Nichukue nafasi hii kuwaasa Wateule hawa kuyaishi maono haya ya Mwalimu kwa kusimamia kupatikana kwa mifumo sahihi ya kuendesha nchi (siasa safi) na namna bora ya kupatikana viongozi bora.

Nachelea kusema kuwa, suala la upatikanaji wa Katiba mpya haliepukiki.

Pengine mchakato wa kupata Katiba mpya iliyo bora unaweza kuchukua muda mrefu.

Lakini jambo la kutengeneza mfumo bora wa namna ya kupata. Viongozi bora likiwemo swala la upatikanaji wa Tume huru ya uchaguzi linaweza lisichukue muda mrefu.

Ni matumaini yangu kwamba, , Wateule watakubalina na mimi kwamba, pamoja na mambo mengine, kazi kubwa waliyonayo ni kuwaletea maendeleo ya kweli Watanzania.

Juhudi zote watakazofanya, wanapaswa kufahamu kwamba bila SIASA SAFI na UONGOZI bora maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana.

Au ninasema uongo ndugu zangu?
 
Be serious kidogo na wewe. Usipomtaja Polepole wala hata hufurahi? If you judge his content unbiased, utaelewa kwamba anazungumza mora sense than all your fake politicians combined.

The guy is simply talented and dedicated.
Shule ya uongozi ya Polepole? Au iko nyingine?
 
The wise say that contempt brings ruin.

If our leaders were honest in their work and held national responsibility, we would not have leaders who care only about their own interests or corruption because the responsibility of the people would be their responsibility.

but we do not have those leaders.
 
Be serious kidogo na wewe. Usipomtaja Polepole wala hata hufurahi? If you judge his content unbiased, utaelewa kwamba anazungumza mora sense than all your fake politicians combined...

Mimi sijamdhihaki Polepole wala nia yangu haikuwa kumdharau bali nimeuliza tu kujua kama kuna shule nyingine zaidi ya darasa alilokuwa anafundisha Polepole! I have no problem with his talent and dedication.
 
The wise say that contempt brings ruin.

If our leaders were honest in their work and held national responsibility, we would not have leaders who care only about their own interests or corruption because the responsibility of the people would be their responsibility.

but we do not have those leaders.
Did you just say, ^leaders who care only about their interest or corruption^? Implication ni kwamba kama wangejali masuala ya wananchi, IN ADDITION TO ^their interest or corruption,^ mambo yangekuwa just fine! REALLY?

Kumbe corruption ni optional kwa kiongozi au mtumishi wa umma, as long as anatimiza kiaina maslahi mengine ya wananchi? I bet, your brain no longer cooperates with your inner self.
 
Back
Top Bottom