Wito kwa Watanzania: Tusimame sote, tutashinda

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,494
1,874
Mshairi mwandamizi na mbobezi, Mohammed K. Ghassani, katika Diwani yake iitwayo KURASA MPYA ukurasa wa 7, ni kama vile anamhakikishia Rais wa Awamu ya 6, Samia Suluhu Hassan kuwa hakika "TUTASHINDA"

Anaandika kama ifuatavyo:

[Tutashinda, tusimame sote tufunge ubinda (kamba au mkanda wa kufunga kiunoni tayari kwa kupigana)

Tuyahame, maumivu tulonayo ya kidonda (iwe kufiwa na Magufuli, kufiwa na Maalim Seif au ufisadi uliokithiri BoT, bandarini na kwingineko)

Irindime, furaha yanyooke yalopinda]

Angalizo: yote ya kwenye mabano ndani ni nyongeza yangu binafsi.

Na kwa kusema hivyo, ili Rais Samia Suluhu Hassan ashinde, inabidi tusimame sote pamoja naye ndiposa tutashinda pamoja naye. Asiwepo wa kukaa kitako huku akiangalia wengine wanasonga mbele. Ataachwa njiani, maana hatupaswi kurudi nyuma au kusimama tu bila kusonga mbele.

Natamani japo ubeti huo tu, umfikie Samia Suluhu Hassan na Hussein Ali Mwinyi, wayahame maumivu tuliyopata na kuyanyoosha yaliyopinda!
 
Back
Top Bottom