Wito: Kwa wanyiramba wote

Wito: Kwa wanyiramba wote

masanjasb

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
2,364
Reaction score
869
Wadau habari za jioni?

Nimesikia tangazo la wito toka kwa mh. Mwugulu akiwaita wanyiramba wote ndani ya ukumbi wa Urafiki pale Shekilango ili kujadili mstakabali wa iramba.

Nikiwa nawaza na kuwazua likaja swali kichwani mwangu nalo ni,wanaCHADEMA wanaotokea Iramba kama Dr. Kitila Mkumbo wanaweza jumuika pia?

Na kama kuna mwaliko wa barua na yeye kapewa? Nauliza hivyo nikijua kabisa huyu mtu ni myiramba original na pia anaweza kuwa na mchango mzuri sana akishirikiana na wanyiramba wengine kama akina Mwigulu Nchemba au atabaniwa kwa vile tu yupo chama kinachoongozwa na kiongozi anaechukiwa na mwandaaji wa shughuli hyo?
 
Asipo kwenda Kitila Mkumbo basi anajimaliza kisiasa,Mwigulu ni jembe sana,mbali ya siasa ameamua kuwakutanisha wadau wote kwa umoja wao kujadili hatima ya jimbo na wilaya yao.
 
Asipo kwenda Kitila Mkumbo basi anajimaliza kisiasa,Mwigulu ni jembe sana,mbali ya siasa ameamua kuwakutanisha wadau wote kwa umoja wao kujadili hatima ya jimbo na wilaya yao.

this is too low
 
Mkuu taswaira kama kweli mwigulu ni jembe kwa nini hapendi juhudi za mnyiramba mwenzake na mara kwa mara anambambikia kesi za hapa na pale ili kumshusha kisiasa?
 
Akili za kibavicha ni hasara tupu.

Guilt conscience inakusuta mpaka unashindwa hata kulitaja jina la huyo Dr. wako wa pale chuo kikuu.
Nikiwa nawaza na kuwazua likaja swali kichwani mwangu nalo ni,makamanda wanaotokea iramba kama dr(k.......m) wa pale chuo kikuu anaweza jumuika pia?

Wewe mwenyewe unasema wanyiramba WOTE wameitwa kujumuika na kujadili mstakabali wa Iramba, harafu unauliza tena kama na yeye ANAWEZA kujumuika. Is he really Mnyiramba.

Kwa angalizo lako unatufanya tuanze kufikiria kama huyo Dr. wako siyo Mnyiramba kwa sababu kama angekuwa ni Mnyiramba kusingekuwa na wasiwasi wa yeye kuhudhuria kwa vile tangazo linasomeka na kueleweka kwa watu wenye fikra pevu.

Bavicha ni janga la taifa.
 
Asipo kwenda Kitila Mkumbo basi anajimaliza kisiasa,Mwigulu ni jembe sana,mbali ya siasa ameamua kuwakutanisha wadau wote kwa umoja wao kujadili hatima ya jimbo na wilaya yao.

jimbo linafikia tamati hadi ikajadiliwe HATIMA
 
Kwa waliko dar ni vema wakahudhuria.

Kusiwe na uchama hata kwa mwandaaji mwigulu. Mwandaaji alete hoja na apokee msimamo wa wengine bila kuwahukumu kwa vyama vyao. Bila hivyo itakuwa ngoma ya watoto-tunajua haikeshi.

Na mwigulu ashauriwe kuacha siasa mbaya asimamie kweli na jimbo lake lipige hatua.

Kwangu mimi naona mwigulu ameanza kuona kitu.
 
Mtu maarufu akitajwa kwa jina la kwanza na la mwisho kwa mtu mwelevu utaelewa ni nani hasa anaeongelewa hapa,mfano nikisema jk kwa maono yako utasema nimeshindwa kutaja jina la boss wako vzr? Bandiko langu limebeba maana kubwa hasa kwa mhusika wa hucho kikao maana amekuwa kwenye msuguano kwa mda mrefu na dr km(kitila mkumbo) na kama nia nikujenga iramba kwa nini mwigulu na kitila wasiwe marafiki wa kweli na sio kama ilivyo leo?
 
Ni mahakama pekee unayoweza dhibiti kama unaemsema ni muuaji au la.....japo nayachukia maneno yake ila sijawahi kushuhudia matendo yako kwa hyo i cant judge him
 
Akili za kibavicha ni hasara tupu.

Guilt conscience inakusuta mpaka unashindwa hata kulitaja jina la huyo Dr. wako wa pale chuo kikuu.


Wewe mwenyewe unasema wanyiramba WOTE wameitwa kujumuika na kujadili mstakabali wa Iramba, harafu unauliza tena kama na yeye ANAWEZA kujumuika. Is he really Mnyiramba.

Kwa angalizo lako unatufanya tuanze kufikiria kama huyo Dr. wako siyo Mnyiramba kwa sababu kama angekuwa ni Mnyiramba kusingekuwa na wasiwasi wa yeye kuhudhuria kwa vile tangazo linasomeka na kueleweka kwa watu wenye fikra pevu.

Bavicha ni janga la taifa.

UNaipenda Bavicha mpaka utakapoingia kaburini lakini hufit kuwa mmoja wapo muulize LE MUTUZ UVCCM anasema imekufa kairevive hiyo achana na Bavicha sio size yako ha ha unaota ndoto
 
Ivi kuna mtu na akili yake timamu anaenda kumsikiliza mwigulu.......mtu kama huyu atakuongezea nini kwenye maisha.....namwona kama mshamba hana exposure.....he is blind though anaact kama anaona....watu wa philosophy wanajua nikisema mtu ni kipofu japo ana macho.....
 
Hicho ni kikao cha umbea,uzabizabina na ushekunaku. Kikao chochote kinachosimamiwa na mwigulu,hakiwezi kuwa na tija. Nachojua wanyiramba wa ukweli hawatahudhuria,na mimi napendekeza wanyiramba tusihudhurie ili atahayari.
 
Hive Iramba wanaishi wanyiramba pekee - au ndio siasa za ukabila?
 
Swali hilo labda ulipeleke moja kwa moja kwa mwenyekiti kwa vile kifungo chake kimeisha atakujibu
 
Hicho ni kikao cha umbea,uzabizabina na ushekunaku. Kikao chochote kinachosimamiwa na mwigulu,hakiwezi kuwa na tija. Nachojua wanyiramba wa ukweli hawatahudhuria,na mimi napendekeza wanyiramba tusihudhurie ili atahayari.


Kama wewe ni mnyiramba tafadhali hudhuria tu, toa uchama wako weka unyiramba wako mbele kamsikilize mnyiramba mwenzako mh mwigulu nchemba
 
Waheshimiwa kwa maoni yangu binafsi........ninadhani neno "wanyiramba" si busara kulitumia hasa pale maendeleo ya jimbo la Iramba inapokuwa agenda.....badala yake neno WANAIRAMBA lingetumika ili kuondoa dhana ya ubaguzi......kule Iramba kuna makabila mengi tu waliweka makazi yao vizazi na vizazi. Je siku nasi wazaramu wa ubungo tukijadili maendeleo ya jimbo letu mh Mnyika atahudhuria kweli???......."Dhambi ya ubaguzi haiishi" ~~ Mwl J K Nyerere (APP)
 
Kuwa Mnyiramba is one thing, lakini nani kaitisha mkutano is another thing. Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kuitwa na Mwigulu akaitika wito? Labda kama akiwa hana la kufanya.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom