Wito kwa wanahabari: If you can't get what you want, just take what you get!

Pole Sana kwa Pikipiki ila ule ulikuwa ni mzigo na sio Bodaboda... Ule nadhani ulikuwa na uzito wa karibu kilo mia mbili kuumudu barabarani Hongera zako na Tatizo lako ulikuwa huvai helmet
 
Ninaposema wewe ni msaka chochote simahanishi kulipwa katiaka uandishi wako bali ninamaanisha kukumbukwa na bwanamkubwa.
Mkuu Musigaji, kwa taarifa tuu, nikienda Chato au Biharamulo, huwa nafikia kwake, tena ni kabila moja, hivyo ningetaka kukumbukwa, ningejipendekeza kwake na kujikombakomba ile mbaya! .

Paskali ni ile type ya full maukweli tuu. Ukiwa mkweli too much unakuwa adui wa wengi.

Paskali.
 
Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho kiko mubashara Star TV, asubuhi hii, kinazungumzia sheria hii mpya ya habari, kule Mwanza yuko Dotto Emmanuel Bulondo na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile na kwa Dar es Salaam, yuko Angalieni Mpendu, Pili Mtambalike wa MCT na Maggid Mjengwa.

Kiukweli wameitendea haki sheria hii, kwanza kwa kuikubali kuwa tayari ipo, hii inaitwa "accepting the reality", pili kitu cha kufanyika sasa ni kumsaidia Waziri wa Habari, kutunga kanuni bora.

Paskali
 
Sasa wanasemaje kuhusu upande wa pili kwa maana ya kuwakandamiza nyie na wamejiandaaje kukabiliana na changamoto hizo........tudokeze kidogo mkuu wengine tuko mbali na tv!
 
Sasa wanasemaje kuhusu upande wa pili kwa maana ya kuwakandamiza nyie na wamejiandaaje kukabiliana na changamoto hizo........tudokeze kidogo mkuu wengine tuko mbali na tv!
Mkuu Kaufman, baada ya kusainiwa kwa sheria mpya ya habari ambayo bado ina baadhi ya vipengele kandamizi, njia iliyobakia ni kutengeneza kanuni bora.

Paskali
 
Mkuu Kaufman, baada ya kusainiwa kwa sheria mpya ya habari ambayo bado ina baadhi ya vipengele kandamizi, njia iliyobakia ni kutengeneza kanuni bora.

Paskali
Mi naitwa Kafman si Kaufman
Sasa kanuni bora zinaweza badili dhana ya sheria na hata huko Mahakamani kwa mfano watahukumu kwa kutumia hizo kanuni? Mi siijui sheria mkuu.....
 
Kuna aina mbalimbali za Mapambano. But fighting from within ndio the most effective way.
Paskali
Ngosha Pascal,
Kwanza ni kweli wasukuma si waoga kama ulivyosema nakuunga mkono 100% ila ni peace makers...Hili la kwenu sasa "waandishi wa habari" ni tatizo kubwa mno,maana kwanza mmekuwa na matabaka sana. Kuna waandishi wachumia tumbo,kuna wasaka uongozi, wasaka hongo na waandishi wachache sana ni waandishi wenye weledi.
Kwa nini nasema hivi, hivi bungeni kuna wanahabari wangapi hata tukichukulia tu upande mmoja wa chama tawala? Je, ni kweli hawakuona muswaada huo kuwa ulikuwa haufai? Ndugu yangu Pascal au Pasi kama uitwavyo nyumbani, hiyo Fighting from within...yes naikubari kinadharia lakini kivitendo hiyo tayari ilishafeli...who gonna fight from within? Personally simuoni kaka.
ulichoongea nahisi umetumia msemo wa wasukuma wa " Kaya ya Ng'obha nayo kaya" nashindwa kuistranslate vizuri kwa kiswahili ili wanaJF wote tuwe sawa.
Kiwezekanacho leo na kisingoje kesho....
 
Ningekuwa mwalimu wako ningekulima 0%. Viboko vya kutosha na suspension juu. Uwe unajiongeza basi.
Ungenilima 0% sababu na wewe umo katika list ya waliotuangusha na kutufikisha hapa tulipo kaka. Lakini nikiona zaidi humaanishi ulichokiandika ila unakubaliana na nilichokiandika maana hakuna asiyejua kuwa Wanamageuzi wetu walituzuga kutuonyesha walikua wanataka kutuletea katiba mpya kumbe hamu yao ilikua kuingia Ikulu.
 
Ngosha Pascal,
Kwanza ni kweli wasukuma si waoga kama ulivyosema nakuunga mkuyyono 100% ila ni peace makers...Hili la kwenu sasa "waandishi wa habari" ni tatizo kubwa mno,maana kwanza mmekuwa na matabaka sana. Kuna waandishi wachumia tumbo,kuna wasaka uongozi, wasaka hongo na waandishi wachache sana ni waandishi wenye weledi.
Kwa nini nasema hivi, hivi bungeni kuna wanahabari wangapi hata tukichukulia tu upande mmoja wa chama tawala? Je, ni kweli hawakuona muswaada huo kuwa ulikuwa haufai? Ndugu yangu Pascal au Pasi kama uitwavyo nyumbani, hiyo Fighting from within...yes naikubari kinadharia lakini kivitendo hiyo tayari ilishafeli...who gonna fight from within? Personally simuoni kaka.
ulichoongea nahisi umetumia msemo wa wasukuma wa " Kaya ya Ng'obha nayo kaya" nashindwa kuistranslate vizuri kwa kiswahili ili wanaJF wote tuwe sawa.
Kiwezekanacho leo na kisingoje kesho....
Mkuu Kandawe, kwanza nakubaliana na wewe kabisa kuwa kwenye tasnia ya uandishi wa habari kuna tatizo. Fani imevamiwa na makanjanja, wasakatonge, wachumiatumbo, na wasaka uteuzi hivyo kutufanya sisi sote tulio humu kuonekana ndio wale wale kwa kanuni ya Samaki mmoja akioza, wote kuonekana tumeoza, ila kiukweli bado tunao baadhi ya waandishi ambao ni weledi, ila nakiri ni wachache.

Pamoja na matatizo mengine yote, kumeibuka kwa mtindo mwingine wa uandishi unaoitwa "petty cash journalism" ambapo lazima utoe bahasha, ndipo habari yako itoke. Hili nimelizungumzia hapa

Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco wa JF!

https://www.jamiiforums.com/threads...kipindi-cha-mavuno-jee-bahasha-hizi-ni-halali.

Paskali
 
Ngosha Pascal,
Kwanza ni kweli wasukuma si waoga kama ulivyosema nakuunga mkono 100% ila ni peace makers...Hili la kwenu sasa "waandishi wa habari" ni tatizo kubwa mno,maana kwanza mmekuwa na matabaka sana. Kuna waandishi wachumia tumbo,kuna wasaka uongozi, wasaka hongo na waandishi wachache sana ni waandishi wenye weledi.
Kwa nini nasema hivi, hivi bungeni kuna wanahabari wangapi hata tukichukulia tu upande mmoja wa chama tawala? Je, ni kweli hawakuona muswaada huo kuwa ulikuwa haufai? Ndugu yangu Pascal au Pasi kama uitwavyo nyumbani, hiyo Fighting from within...yes naikubari kinadharia lakini kivitendo hiyo tayari ilishafeli...who gonna fight from within? Personally simuoni kaka.
ulichoongea nahisi umetumia msemo wa wasukuma wa " Kaya ya Ng'obha nayo kaya" nashindwa kuistranslate vizuri kwa kiswahili ili wanaJF wote tuwe sawa.
Kiwezekanacho leo na kisingoje kesho....
100% upo sahihi na ulichoandika, siwezi kumjibia Mayalla nini alimaanisha aliposema fighting within bali nahisi alimaanisha waukubali huu mswada kama ulivyo halafu wajitahidi kuwashawisha wenzao ambao wapo katika nafasi ya kufanya marekebisho maana umeshakuwa sheria hakuna tena jinsi. Kuhusu wachumia tumbo hapo ni pagumu sana maana kwasasa ni vigumu kumuona nani si mchumia tumbo mpaka akipata nafasi afanye vile tunavyotegemea. Sitashangaa hata huyu Ngosha wetu hapa Pasi akipata nafasi naye akajiunga na wenzake japo siamini kama itatokea lakini huwezi jua. Mnamfahamu mtu aliyejulikana kama mtetezi wa wanyonge na msema kweli ndugu Humphrey Polepole??? Kaadhibiwa na Mwenyezi Mungu kwa kupewa cheo kilekile alichosema hakina nafasi kwa wakati huu, nini alifanya alikataa?? Thubutuuuu huyo kajinyamazia na U DC wake huko Ubungo. Ushauri wangu kwa watu kama kina Pascal Mayalla pale mkuu wa nchi anapowapatia nafasi kama hizi za umma wakiona kuwa zitapingana na dhamira yao nzuri ya kutetea wanyonge ni bora wakazikaa ama wakiona kuwa hawatakuwa watu wa kutumiwa kama rubber stumps basi wazikubali.
 
Mayala stop that. Lakini hakuna watu waoga kama wasukuma. Just keep quiet kama huwezi kujenga hoja nzuri. Nilitegemea kama mwanasheria (unavyojinasibu, I know you have LLB but never practiced any law) useme WE SHOULD MAKE HEADWAY TO CHALLENGE ITS CONSTITUTIONALITY, sio tuikubali, tuipokee, tuitekeleze kwa roho safi.
Pasco alikimbilia mno hii ID baada ya kupata promo ya ikulu sasa hawezi kurudi kule alikokua....

Amechagua fungu bovu kati ya mema!! Ndio shida ya waafrika!! Sasa hawezi simama tena tetea misimamo kama ya aliyojaribu cheza siku ile ikulu!!

Ameuza vyote sasa anatetea watawala kwakuwa hayupo kizani!! Ameuza ujasiri na hiki afanyacho hakipaswi kukushangaza!!!
 
Mkuu Kandawe, kwanza nakubaliana na wewe kabisa kuwa kwenye tasnia ya uandishi wa habari kuna tatizo. Fani imevamiwa na makanjanja, wasakatonge, wachumiatumbo, na wasaka uteuzi hivyo kutufanya sisi sote tulio humu kuonekana ndio wale wale kwa kanuni ya Samaki mmoja akioza, wote kuonekana tumeoza, ila kiukweli bado tunao baadhi ya waandishi ambao ni weledi, ila nakiri ni wachache.

Pamoja na matatizo mengine yote, kumeibuka kwa mtindo mwingine wa uandishi unaoitwa "petty cash journalism" ambapo lazima utoe bahasha, ndipo habari yako itoke. Hili nimelizungumzia hapa

Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco wa JF!

https://www.jamiiforums.com/threads...kipindi-cha-mavuno-jee-bahasha-hizi-ni-halali.

Paskali
Basi kwa hali hiyo, ngoja tuvumilie tena miaka kumi....kwa vile nchi yetu hatuna VISION ila tunalazimisha kuwa na MISSION baada ya miaka kumi tena tuone ajaye atakuwa na mission gani nasi tuenende humo humo.....uandishi wa habari kwa sasa ni JIPU...!!!!
 
Hiki kilichotokea kwa media za utangazaji kuadhibiwa na TCRA ni matokeo ya madhaifu katika sharia yetu ya habari, niliyazungumza humu, huwezi kuwa vyombo vya habari, vikatawaliwa na sharia mbili tofauti, chini ya wizara mbili tofauti.

Licha ya sheria ya habari kuvihusu vyombo vyote vya habari, lakini sharia hiyo inahusu Zaidi print media, wakati vyombo vya utangazaji vinaratibiwa na sharia ya utangazaji, broascasting act, iliyoko chini ya TCRA, iliyochini ya wizara ya mawasiliano.

Paskali
 
I quote: "Nawaombeni sana tusimlaumu rais Magufuli kuusaini huo muswada kwa haraka, kwa sababu uharaka huo ni uthibitisho wa kutoingilia mhimili wa Bunge, maadam wabunge ambao ndio wawakilishi wetu Wameridhia na kuipitisha hiyo sheria, who is he, asiisaini? !."

Hapa ndio nimechoka kabisa... yani kwamba raisi amebanwa na bunge!!!! na kwamba huu sasa ni uthibitisho tosha kwamba raisi haingilii bunge! na tunatakiwa tuamini hivyo?! Kweli Tanzania ngumu sana aisee!

...alafu 'pascal' huyu inaonyesha ndie yule pasco mwingine... Siku za karibuni naona yule aliyekuwa anaitwa 'pasco' hayupo tena ila huyu 'pascal' kidogo kidogo anakuwa more and more kama 'pasco' yule.
Leo Paskali huyo huyo anaizungumzia sheria hii hii kwa mtizamo tofauti kabisa na huu! Kulikoni Bwana Paskali?
 
Leo Paskali huyo huyo anaizungumzia sheria hii hii kwa mtizamo tofauti kabisa na huu! Kulikoni Bwana Paskali?
Mkuu KUTATABHETAKULE, utanisaidia sana na kulisaidia jukwaa kama utaonyesha the contrast ya mtazamo wa mwanzo na mtazamo wa sasa.

Paskali
 
Wanabodi, japo tukio hili waandishi tumedhalilishwa, haya ndio mambo niliyoyasema kwenye bandiko hili, sasa every Tom, Dick and Harry anaweza kuwa mwandishi, matokeo yake, makanjanja ambao hawakupita shule yoyote ya habari, hawajui maadili, wanatupiwa pesa kama mbwa na kuanza kugombania, hivyo kutuaibisha waandishi wote tuonekane ni watu wa hovyo, hatuna maana!..
P.
 
Mkuu pascal,

Could you let me know if the journalists have got their board that regulates their conducts & setting various standards?
 
Wanabodi,

Huu ni wito kwa wana tasnia ya habari, "Moja shika sii kumi nenda rudi " and "if you can't get what you want, then just take what you get", baada ya kusainiwa kwa sheria mpya ya habari, sasa tuzivunje kambi zote pingamizi, tutoe ushirikiano kwa utekelezaji wa sheria hii mpya.

Tumpe ushirikiano wa kutosha waziri wa Habari, atengeneze kanuni bora, aunde Baraza bora la ithibati ya waandishi, tuunde Baraza huru la habari litakalo shehenezwa manguli wa tasnia hii, halafu yale yote yenye ukakasi, yatachomolewa moja baada ya jingine na yale mazuri yatachomekwa moja baada ya jingine kupitia marekebisho ya sheria hii.

Nawaombeni sana tusimlaumu rais Magufuli kuusaini huo muswada kwa haraka, kwa sababu uharaka huo ni uthibitisho wa kutoingilia mhimili wa Bunge, maadam wabunge ambao ndio wawakilishi wetu Wameridhia na kuipitisha hiyo sheria, who is he, asiisaini? !.

Sii wengi wanaoujua kuwa kuwa iwapo bunge limetunga sheria, Rais ni lazima aisaini, na asipo isaini basi anapaswa au kulipigia magoti bunge lirekebishe kile rais anachotaka, Bunge likingomea, rais anakuwa hana jinsi bali anapaswa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu mpya wa wabunge tuu! .

Sasa ukiangalia jinsi wananchi walivyopigika kwa ukata, njaa na msoto, ukijumlisha na umasikini wetu uliotopea, hili bunge la chama dola lukivunjwa leo na uchaguzi kuitishwa, no one is sure to return, sasa nani yuko tayari kwa bura yangu njema kubadili kwa rehani, au kuchezea shilingi chooni?!, bora alivyosaini.

Sheria hii mpya ya habari ni kama tuu katiba mpya, Watanzania walitaka katiba bora, lakini wakapatiwa bora katiba. Ndivyo hivi kwa miaka 20, waandishi tumelilia sheria bora ya habari, tumeletewa bora sheria, tuikubali, tuipokee, tuitekeleze kwa roho safi.

Hata wewe kama kuna kitu fulani kizuri ulikihitaji lakini ukakikosa, ukafanikiwa kupata kingine kidogo, kibaya, then kukubali tuu hicho kidogo na uwe na shukrani kwa kidogo ili upatiwe kikubwa.

Mfano mzuri ni mimi mwenyewe, nilitamani sana kuendesha Range Sport, lakini kwa mishahara ya sisi watangazaji wa zamani enzi za RTD, uwezo wetu ni kumiliki boda boda, nilinunua boda boda na ndio usafiri wangu siku zote mpaka boda boda iliponifanya vibaya, sasa niko kwenye bajaj, ila kila nikipishana na Range Sport, naitazamaa na kusmile kimoyo moyo huku nikijisemea gari kipenzi changu, halafu nashukuru kwa bajaj yangu, vivyo hivyo waandishi tushukuru kwa sheria hii.
Maoni yangu yanafuata.

Paskali:
Mwandishi ni mwandishi/mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea.

Mkuu sina hakika kama nimekuelewa kisawasawa.

Kikwetu kama mtu hukubaliani na kitu au jambo (tena kwa sababu zenye maslahi mapana zaidi ya ya kwako), na pia kwa sababu linaenda kinyume na convictions zako au certain universal principles, unasema dhahiri kwamba hukubaliani nacho/nalo.

Kusema kwamba jambo hilo liendelee huku ukifanya reference ya kitisho (i.e. kuvunjwa bunge), mbona kama ni kitendo sawa na cha kulikubali pamoja na au kuli-promote jambo hilo?

Pia kusema kwamba if you can't beat them then join them, huoni kwamba umeshaegemea upande fulani kwa mtu anayejinasibu "sina upande wowote"?
 
Back
Top Bottom