Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 38,856
- 90,333
WITO KWA VIONGOZI WENGINE NA WATANZANIA KWA UJUMLA
Na, Rpbert Heriel
Kwanza namshukuru Mungu, yeye aliyemuweza wa yote, mwenye mamlaka atupaye mamlaka, mwenye nguvu atupaye nguvu, mwenye elimu atupaye elimu, Huyo mwenye kila sifa njema ndiye namshukuru.
Baada ya hapo, niwape pole wote mlioguswa moja kwa moja na msiba huu ambao kimsingi ni mzito kama tutazingatia utawala wa nchi. Mungu awaape faraja ya kweli katika kipindi hiki kigumu, pia niwape pole watanzania wote kwa kuondokewa na kiongozi ambaye mlikuwa mkimpenda na nafikiri hata yeye alikuwa akiwapenda. Nafahamu pole hii haitawahusu baadhi ya watanzania kwani kikawaida kwenye hii dunia sio kila mmoja huomboleza kwenye misiba ya namna hii bali wapo wengine ambao hufurahia.
Ninaandika andiko hili nikiwa nazidi kujifunza, na kukubali kuwa sisi ni mali ya Mungu na hakika kama tulizaliwa basi hakika siku moja tutakufa. Ikiwa ni hivyo, basi andiko hili lihesabike kuwa sehemu muhimu ya kutukumbusha wajibu wetu kwa Mola wetu na jamii tulizowekwa kwazo.
Kama nitasema kweli, na kweli ingali ndani yangu nafsi yangu ikinishuhudia, hakika hakukuwa na sababu ya kuficha mahali alipo Rais kwa kipindi chote hiki. Unajua penye wengi kuna mengi na kamwe hapaharibiki kitu, sasa kuwaficha wengi ni kujiepusha na mengi, ni kutaka kuharibu mambo.
Wakati fulani kwenye tawala za zamani zikiwemo tawala za Ashuru enzi za kale, mambo yanapokuwa mabaya kwenye utawala kama Mfalme kupatwa na ugonjwa fulani au tatizo fulani, basi tangazo maalumu lilitolewa kwa makundi muhimu ya watu, makundi maalumu yaliitwa mathalani madaktari bingwa, manabii, waganga na waganguzi, wakaldayo, wanajimu, na watu wote wenye akili, huitwa ili kutatua ugongwa wa mfalme, na hakika ugonjwa huo lazima upate suluhu, lazima tatizo liondoke.
Lau kama tatizo bado lingalipo mbali na makundi hayo maalumu kuitwa, basi mbiu ya mgambo hupulizwa kisha wananchi wote hupewa taarifa kuwa Mfalme wenu yu aumwa kusudi mwenye tiba ajitokeze kwa maana yafahamika kwamba wapo watu wanaujuzi wa mambo lakini hawana umashuhuri yaani hawafahamiki na wakubwa. Hivyo kupigwa kwa Mbiu hiyo ndio lengo lake. Tenaa wakati mwingine mpaka dau huwekwa kwa atakayefanikiwa kupata suluhu ya afya ya Mfalme. Lakini hiyo pia haikufanyika.
Mwisho kabisa, tangazo hutolewa kuwa kila mwananchi aombe kwa Mungu wake kumuombea mfalme ili apone, hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Binafsi naamini, moja ya watu iliyowasaidia kuepa kifo kutokana na maombi ya watu ni pamoja na Tundu Lisu alipokoswa koswa na Mtoa roho. Watu walimuombea, siamini kama madaktari pekee yao ndio walifanikisha lile zoezi bali pamoja na maombi ya watu.
Kuficha Afya ya Rais kulilenga nini hasa?
Waliotaka watu wasijue afya ya Rais wao walitaka wananchi wasimuombee Rais wao huenda Mungu angesikia?
Au mlichukulia rahisi/ mazoea kuwa haina haja ya watu kuambiwa atapona kama kawaida?
Huu sio muda wa kulaumiana lakini lazima watu wawajibike baada ya zoezi la kumpumzisha Kiongozi wetu.
Mtu anatuambia Rais ni mzima anachapa kazi wala haumwi kumbe mtu anaumwa, aisee! Hii ajabu sana, kwamba sisi watoto tunaona ni jambo kubwa au lisilowezekana kwa kiongozi mkuu wa nchi? Pengine angesema anaumwa watu wangehangaika kumuombea wale waliokuwa wanampenda, sasa unnficha ili iwe nini?
Watu wanadai Rais anaumwa ati mnawatishia wengine mmewasweka ndani, jamani jamani! hivi ilishindikana nini kusema ni kweli Rais anaumwa, watu wamuombee, mbona rahisi hivyo.
Tusiwe hivyo ndugu zanguni, mambo hayaendi hivyo. Mnatishia watu ili iwe nini sasa, waogope au wafanyaje. Tubadilike jamani.
Hii ni funzo kwangu, na kwa watu wengine, tusifiche haya mambo, ni hatari kuliko tunavyodhani na wote tumeona. Kwani ulikuwa ni ugonjwa wa aibu?
Ati mimi niumwe hapa alafu ndugu zangu wasitoe taarifa kwa watu, kwa kweli nitawahesabia hatia.
Dunia inawatu wengi, sema tatizo lako hauwezi jua msaada utatoka wapi.
Nimesikitika kweli, wanaohusika wote wawajibike, msipowajibika wakuwawajibisha yupo. Nanyi mnamjua.
Na wale mnaofurahia tukio hili, hongereni kwa sababu kila mtu huvuna alichokipanda. Tenda wema nawe utavuna wema, ukitenda mabaya utalipwa mabaya.
Mwisho, tujitahidi kupendana, elimu, uzuri, pesa, cheo, mamlaka sio kitu wala sio chochote, ukijihadaa vikakuendesha na kupelekesha viumbe vya Mungu jua utalipwa maradufu. Maana kuna watu wakipata vyeo na pesa wanakuwa vichaa na wapumbavu.
Utofauti wetu ndio ukuu wa Mungu, haimaanishi tuumizane bali tunapaswa tuombe hekima ya kuelewana.
Mungu awabariki wote.
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam