jembelamkono
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 2,733
- 2,011
Waheshimiwa wakuu sana nawaombeni muangalie upya hili mnalotufanyia raia huku mitaani,
Hali imekua ngumu kuliko maelezo,yaani kuzidi kipindi kile cha Ukapa,
Wanaume tunafedheheka kupita maelezo,Mifukoni tunatembea na ma chenji (Coins),Noti ya alfu kumi kuipata imekua kama kupata dola alfu moja,
Narudia tena wanaume tunafedheheka hapa mjini,Majumbani huko tumekua watu wa sound kila kukicha,nyumba tunazikimbia alfajiri kabla jogoo hajawika,Kurudi usiku wa manane kama mwanga.
Tunaogopa kukutana hata na watoto mezani,Baba unaombwa pesa ya vitumbua asubuhi inakua mtihani mkubwa kwako.
Mchana tunabadili gia angani juu kwa juu,(mlo wa mchana imekua sinema),
Jamani hata kama ni kauli mbiu ya "hapa kazi tuu,sijui kutumbua majipu,lakini sio kwa namna hii...
Narudia tena familia ziko mbioni kusambaratika,Watu wana discuss mamna ya kulikimbia jiji,nauli tu ndio imekua mtihani.
Huku kwa Mangi hatuaminiki tena ,daftari tumekopa mpaka aibu sasa,tunajikaza kiume lakini hatujui hatma yetu lini,
Kama hii keki ya taifa ni yetu sote,japo mtukumbuke kwa makombo.
Makontena waliiba wachache wenye pesa zao,iweje kibano kitupate hata sisi makabwela,walala hoi!!??
Walah hali ikiendelea hivi,nina mpango wa kwenda kuwatelekeza watoto nyumbani kwa waziri wa fedha au kwa Magu kabisa,Nimevurugwa kwelikweli.