Wito: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kibadilishiwe matumizi

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Mwanzo nilidhani mzaha Prof. Kabudi ambaye alikuwa mwalimu wa chuo kikuu Dar essalaam alipoteuliwa na Magufuli kuwa Waziri alisema anamshukuru rais kwa kumtoa ktk jalala. Wenye Akili tulistuka kwa maneno yale kwa kudhani kuwa chuo kikuu ni sehemu nyeti ktk nchi sasa imekuwaje kuwa jalala ghafla. Ila kwa hali inavyo one onekana huenda Kabudi alikuwa sahihi.

Juzi Profesa Mkumbo kutoka chuo hicho icho ambaye alikuwa Mwalimu, Mkumbo anae jiita mbunge bila kuchaguliwa akiwa bungeni alisema anataka sura ya raisi Samia iwekwe ktk fedha.
Yaani ktk nchi iliyofanywa kuwa Maskini watu wanalala barabarani kwa ubovu wa barabara, wajawazito wanakufa kwa huduma mbovu, Elimu mbovu, wafanyakazi maslahi Dunipace, wakulima wapo hoi, huku majizi ya ccm na malaika zake yakibaka fedha za walala hoi Mawazo ya Profesa Bungeni ni kuweka sura ya Rais ktk fedha.

Hata yule jamaa muasisi wa mauaji, utekaji,utesaji na watu wasio julikana nasikia ni hapo hapo alitunikiwa shahada tena shahada ya udaktari wa philosophy mpka wananzengo wakawa wanahoji uhalali wa yeye kupata hiyo shahada uchwara akawa anauna na wengine kuwapoteza.

Ni maprofesa kutoka chuo hiki hiki walituletea ripoti ya urongo kuwa Watanzania tunadai fedha nyingi Kampuni ya madini ya ACCACIA na tutalipwa kodi ambayo kila mtu atakuwa na Noah yake.Tundu Lissu alisema Bungeni kuwa ile ripoti ilikuwa ni Proffeserial Rubish!! Yaani ni taarifa takataka iliyo andaliwa na maprofesa wa hovyooo.

Ni mtu mmoja tuu Prof. Mkandala toka chuo hiki aliwahi kusema ukweli ktk utafiti wake wa Kisayansi kupitia shirika la REDET kuwa CCM inapendwa na watu ambao mijinga au Nyerere huwa anayaita Mazuzu.

Nyerere ktk moja ya hotuba zake anasema Elimu ya chuo kikuu inapaswa kuwa chemchem ya Fikra chanya ambazo chanzo chake sio utumwa.
Nyerere anasema utumwa ni ile hali ya mtu kuambiwa mawazo ya watu fulani na yeye kuwa tayari kuyapigania bila kujali kuwa jambo hilo linaweza kushusha hadhi yake au chuo alicho soma.
Maendeleo hayana chamaa.
 
Back
Top Bottom