Wither Tanzania? Dalili hizi zinaashiria nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wither Tanzania? Dalili hizi zinaashiria nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tausi Mzalendo, Feb 5, 2012.

 1. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Huenda kuna jambo linataka kutokea Tanzania for the better or worse!
  Kwanini Taifa lina kila dalili ya kumeguka?
  Migogoro na mitafaruku ya kila aina:
  Kwa uchache nitaorodhesha michache na wasomaji mnaweza kuongezea :

  • Wananchi wanyonge dhidi ya watawala wenye nguvu na unafuu wa maisha ( migogoro wa wananchi dhidi ya wabunge, mgogoro wa madaktari dhidi ya serikali)

  • Mitafaruku inayojikita kwenye imani na dini za watu ( kutwa kuchwa waislam dhidi ya wakristo.Hakuna jambo linafanywa na wakristo hata kwa nia njema likapokelewa na waislam, Ni kupinga mwanzo mwisho).

  • Mitafaruku ya kisiasa ( vyama vya upinzani dhidi ya Chama tawala, Chama tawala dhidi ya vyama vya upinzani hata pale upinzani unapoleta hoja nzito zenye mashiko na maslahi ya watanzania kwa ujumla wao

  • Migogoro ya kifamilia( wake dhidi ya waume na waume dhidi ya wake, watoto dhidi ya wazazi)
  • Migogoro ndani ya jamii ( uonevu wa wenye nacho dhidi ya wale wasiokuwa nacho, mogogoro ya kugombea rasilimali)
  • Migogoro mingine ya kisiasa ( Zanzibar kupinga mambo yanayofanywa na bara hata kwa nia njema kama hili la Makubaliano ya kuongezewa ukanda wa bahari; matamko ya kushutumiana hasa kuwashutumu baadhi ya viongozi hata pale ambapo hakuna haja ya shutuma; kuwa na makundi na mitandao ndani ya serikali na hata vyama)
  Na mingine mingi.
  Kuna jambo linataka kutokea Tanzania.Haiwezekani kwamba ni jambo la kawaida tu au ni dynamics za kawaida katika jamii! Migogoro hii inalenga ama kulimega au kulisambaratisha Taifa hili au kuliimarisha?
   
 2. Rah_sputin

  Rah_sputin Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wamechoka amani Tausi.
  Wamebweteka, wamejidanganya muda mrefu kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani.
  Wanadhani tunakula amani!
  Ngoja tuone kitakachotokea
  A hungry man is an angry man.
  Love and Peace!
   
 3. m

  moshingi JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna haja ya tahamaki...
  Jamii inayoendelea haiwezi kutulia kama maji ya mtungi...
  Ni dhahiri katika maendeleo yeyote ya kidemokrasia, kijamii, na uchumi
  mambo kama hayo yanayoashiria misuguano lazima yajitokeze...
  Labda wengine wataona ajabu, kutokana na mazowea ya mbinyo wa demokrasia ya chama
  kimoja, na utovu wa uhuru wa vyombo vya habari wakati ule.(gazeti uhuru/mzalendo/daily news + redio tanzania)
  mambo haya yalikuwepo tangu zamani lakini hayakuwa yakiripotiwa/ hapakuwepo na uwazi.
  Tusiogope haya ni mafanikio ya uhuru wa habari na uwepo wa demokrasia.
   
 4. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Inapofikia hatu ya kukosekana nidhamu kwa wazi kama tulivyoshuhudia hapa karibuni( mkanganyiko baina ya viongozi wenyewe),
  kukosekana kwa woga hata kwa vitu visivyohitaji kuvaa miwani kuona ni vibaya ( wabunge kutokuwakilisha wananchi na badala yhake kujiwakilisha wenyewe..huoni tunaelekea kwenye hatari? Huko nyuma mbinyo wa uhuru wa habari ulikuwepo sambamba na watu kuwa na "nidhamu" hata kama ni ya woga.
   
 5. m

  moshingi JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati ule (zama za giza) dhana ya nidhamu ilitumika makusudi
  kuyafutilia mbali mawazo m-mbadala(zidumu fikra za mwenyekiti), labda kwa wakati ule yalisaidia kutokana na mazingira,
  maana tuliuruka mfumo mmoja muhimu sana katika maendeleo ya jamii nao ni "Ubepari"...
  tulitakiwa tuupitie kabla ya ujamaa(ambao ulituaminisha kuwa binadamu wote ni sawa, kumbe...!)
  lakini tuliuruka kwa kuwa ulikuwa ni wakoloni(maadui zetu)
  Jamii yenye afya lazima iwe na uhuru wa mawazo, hata ndani ya chama au serikalini...
   
 6. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani sasa tuko mfumo upi?
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Tuko mfumo wa kuchanganyana!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  tupo katikati
  tunaanza miaka 50 mingine ambayo itaamua the fate of this nation
  and it doesnt look good to be honest
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna tabia moja ya pressure mahali popote pale; lazima itoke somewhere! Tunachoshuhudia ni kuzidi kuongezeka kwa pressure na tension katika nchini na hii ni lazima ipate mahali pa kutokea ili kurudisha hali katika hali ya kawaida. Ninaamini hili litatokea:

  a. Lazima zitokee vurugu za kidini kwanza - hili lazima litokee ili kupunguza pressure kwenye mambo ya kidini na likitokea litatusumbua for few weeks hivi na watu watapoteza maisha, vitu vitaharibiwa na watawala watatafuta kila namna ya kusuluhisha bila kufanikiwa hadi wananchi wenyewe watakapoona imetosha liishe.

  b. Lazima zitokee vurugu za kisiasa kuachilia pressure ya kisiasa ambayo imejengeka na inazidi kujengeka. Hili litatokea vile vile hasa kwa sababu ya kuwa na hizi chaguzi ndogo ndogo za mara kwa mara na serikali kujaribu kuzuia sana watu kujiexpress kisiasa. Hofu yangu kubwa ni kwamba kiongozi maarufu wa upinzani anaweza kuuawa - na kusiwe na shaka kuwa ameuawa na dola - na hilo litafumua hiyo pressure nchini.

  c. Lazima zitokee vurugu za mahali pa kazi au zinahusiana na ajira kwani mfanyakazi ana uwezo wa kuvumilia kwa kiasi fulani lakini itakapofika kuwa uchaguzi ni kulalamika au kufa na njaa, kudai au kuishi katika dhiki wafanyakazi watasimama pamoja. Mgogoro wa madaktari ni sehemu ndogo sana ya mgogoro huo unaokuja. Kama ndani ya mwezi mmoja hivi serikali itakuwa haijapata suluhisho la madaia na madeni ya wafanyakazi mgogoro mkubwa utakuwa mbele yetu. Huu utasababishwa zaidi na hali mbaya ya kiuchumi!

  Sasa, hofia kama hayo matatu yana converge into one crisis!

  Uzuri pekee ni kuwa Tanzania haiwezekani kutokea mgogoro wa kikabila ambao unaweza kugusa taifa zima kwani huo ndio mara zote ni catalyst ya hayo mengine yote na ndiyo mafuta pekee yaliyokosekana nchini kuweza kulipua hiyo migogoro mingine.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  hiyo trend ni kwa nchi zoote?
  hii ni inevitable????/

  sidhani.....

  hii ni matokeo ya fundamental mistakes za siku nyingi.....
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tausi, haya unayoyasema tumekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 20, hakika tangia demokrasia iliporuhusiwa mikanganyiko ya aina hiyo imekuwa sehemu ya maisha. Sana sana mie naona wabongo wasahaulifu sana, likitokea jambo kubwa kwenye jamii watu wote wanafuata mkumbo na hadi habari hiyo inapofifia ni wachache watakaokumbuka agenda zao.
  Mie nasema hii migogoro mnayoiona ni bandia na si ajabu ni watawala wenyewe au kuna kikundi cha watu wana-sponsor hizi propaganda na kuzitangaza sana kupoteza mwelekeo wa jamii kwa maslahi wanayoyajua wao wenyewe. Sie wote ni wahanga wa michezo ya kisiasa.
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Vita vya kidini ndio vipo karibu zaidi kutokea kwa sasa.
   
 13. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mzee mwanakijiji siku hizi umekuwa sheikh yahya au tb joshua???. Maneno uliyosema ni mazito sana. Napiga magoti kuomba yasitokee kwa jina la Yesu Kristo aliye hai jana,leo,kesho na hata milele!
   
 14. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi, huduma za afya siyo kipaumbele cha Serikali?
  Taifa la wagonjwa litasimama?
   
 15. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba watu wengi wanaamini kwamba hii nchi imekuwa tulivu na itabaki kuwa hivyo siku zote, hata ukisikia sala na maombi, mengi yamejaa msukumo wa kuombea hali ibaki kuwa shwari.
  Jambo la muhimu na la kukumbuka wakati wote ni kwamba Tanzania si kisiwa na wala haina tofauti na nchi nyingine yoyote kwa sababu nayo inakaliwa na binadamu walewale ambao leo ni kondoo na kesho ni mbweha. Kwa hiyo uwezekano wa watu kutwangana upo kutokana na kuwepo kwa hali zile zile ambazo nchi zingine zilisababisha machafuko. Kwa bahati mbaya hakuonekani juhudi zozote za kukwepa msala huu kwa sababu serikali hakuna na vyombo vya dola na ulinzi vimegeuka magenge ya wapiga dili.
   
 16. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kusikia nchi ambapo wagonjwa wanakuwa "dismissed" kutoka hospitali! Huwa tumezoea wanapata discharge kwa vile hali zao ni nzuri, au referral kwenda kupata matibabu zaidi kwenye hospital iliyo na uwezo zaidi. Jana niliskiliza Wagonjwa waliopewa dismissal wakiambiwa waende makwao au kwa wale waliotoka mikoani watafute pa kwenda! Sikuamini maskio yangu maana sikuweza kupata picha ni vipi mgonjwa mahututi ataweza kujikongoja .............atoke hospitali! Wengine hata kuongea walikuwa wanaongea kwa shida.SERIKALI YETU INATUPELEKA WAPI?
   
 17. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi naamini ndio dalili moja wapo tena muhimu kabisa ya manadiliko kutoka leftist politics and social relations to rightist. Tanzania bado ipo kwenye mabadiliko ya kimfumo wa maisha kutoka kwenye mfumo tuliouzoea toka enzi za Mwalimu wa serikali kuwa kama mama wa raia, ikiwa na maana ya kuwalea huku tukiipa jukumu la kukusanya kodi, kwenda kwenye mfumo wa kibepari, ambapo kila mtu anakuwa anajitegema. Mfumo huu wa Kibepari ndio hasa unaotawala dunia kwa sasa baada ya vita baridi. Tunaweza kuona Nyerere hakupenda mfumo huu na baada ya kuona kazidiwa na nguvu zake akaamua kung'atuka. Mwinyi alichofanya ni kuufungulia milango kwa kukubali policy za IMF na WB ambazo ndizo hasa propagators institutions za mfumo huo. Mkapa alichofanya ni kujenda mifumo ya ndani ili mfumo ufanye kazi vizuri huku na yeye personally akijiandaa na mfumo kwa kumega mtaji wa kutosha. Kikwete sasa ndio yupo katika critical stage ambapo mfumo sasa umeanza kugusa moja kwa moja mtu mmoja mmoja, hasa masikini.
  Mwalimu alikuwa na slogan kwamba ubepari ni unyama, watu wengi hawakumuelewa kwa kipindi kile. In fact in this system most poor people will perish out of the globe huku watu wanaangalia. Dalili ndio hizo, wagonjwa maskini ambao wanalazwa hospital za serikali watakufa sana huu ni mwanzo tu. Nchi za Ulaya mashariki watu sasa wanakufa kwa snow (freezing), huku kuna mtu jirani tu anaspace kubwa yenye heater ndani kwake. Inasigitisha nchi kama Ujeruman ina pet dogs 6-8million huku ikiwa na homeless 860,000. Hao ni Mbwa tu ambao wanaishi vizuri, wanakula vyakula kama binadamu kutoka supermarkets huku watu wanakufaa njaa katika upande mwingine wa dunia.
  Wanasiasa wa CCM baada ya kupitisha azimia la Zanzibar walichofanya ni kuchuma kilikuwapo kwa nguvu zote kabla mfumo haujakomaa na sasa wapo katika safe side kwani wameza kujibadili kuwa capitalist mwenyewe, kutoka kuwa makada wa chama wakati wa ujamaa.
  Tunakokwenda ni kubaya zaidi kwa mtu maskini, watu maskini wengi watakufa, na bado huu ni mwanzo tutegemee maasi zaidi miaka ijayo.Vijiji alivyoanzisha Mwalimu vitakufa, ardhi inauzwa kwa wenye mtaji, tumeshudia ranchi zote za Taifa zimeuzwa, sehemu zenye utata wa ardhi kama maeneo wanaishi wakimbizi yanauzwa (Mfano Mishamo na Katumba Rukwa), baada ya hapo yatakuja maeneo ya vijijini. Watu wengi zaidi watahamia mijini kuwa wamachinga, uhalifu utaongezeka zaidi. Huo ndio Ubepari.
  Kibaya zaidi watu watazidi kupoint dini, kabila, au ukanda kuwa ndio adui yao. Watu maskini watakufa sana
  Kwa kifupi ubepari hautoi nafasi ya mtu maskini kuishi duniani, kadri watu maskini wakavyokuwa wanakufa ndio ubepari utakuwa unashusha thamani ya mtu mwenye kipato cha kati na kumpeleka maskini, kwa sababu ili mfumo uendelee kuwepo lazima kuwe na tajiri na maskini.
  Mgogoro wa Madaktari wa sasa, utaleta mabadiliko makubwa ya sekta ya afya Tanzania, hata hizo posho zikiongezeka itakuwa kidogo na wengi wataenda sector binafsi na ndio kifo halisi cha hospital za serikali.
   
 18. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tulipofika ni bapaya. Ila bahati iliyopo sasa, mkosaji bado hajakuwa mmoja. Watu wengine wanadhani ni bunge, wengine wanalaumi madaktari, wengine Pinda, na wengine Raisi. Sasa, mwanga ukatoka na wote wakasema ni serikali, basi ndio safari hiyo.

  Ewe JK, kama unadhani iwe basi yatatimia.
   
Loading...