Wise Quotes by Mwalimu Nyerere: And not so Wise by Others...

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,194
1,355
Wise Quotes from Mwalimu
Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni"
***********************

'Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana' 01/5/1995
***********************

'Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!' 01/5/1995
***********************

“Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika” –MwalimuNyerere (Januari, 1966)
***********************

"Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais ambaye atalitambua hilo na ataichukia rushwa hata ukimuangalia anaonyesha kweli anaiichukia rushwa, sio rais ambaye anayesema kweli rushwa ni adui wa haki....lakini ukimuangalia usoni unashangaa na kusema.... aaaah kweli huyu?
***********************

"Poverty is not the real problem of the modern world. For we have the knowledge and resources which could enable us to overcome poverty. The real problem--the thing which causes misery, wars, and hatred among men--is the division of mankind into rich and poor."
***********************

Not So Sure kama kweli alisema haya na wapi…. lakini inasemekana Source inapatikana kwenye hiki kitabu
Reflections On Leadership in Africa' VUB University Press, 2000.

Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?
***********************

Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
***********************

Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.
***********************

Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu.
***********************

Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe....
***********************

Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili.
***********************

And Not so Wise by Others.., Kwa kweli mpaka sasa siamini kama ni kweli alisema au alisingiziwa

"Kina mama pia endeleeni kuzaa wasichana wazuri kwani katika miaka hii miwili hata kwenye mashindano ya urembo duniani tumetamba." -- Jakaya Kikwete
***********************

Ikiwa tutaruhusu wasichana waliojifungua kurudi mashuleni matiti yao yatakuwa yakichirizika maziwa darasani" --- J.M.Kikwete
***********************

"Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi" J. K. akimtetea mbunge Chitalilo aliyegundulika kuwa kughushi vyeti vya elimu yake.
***********************

"Nafikiri imefika wakati Tuwaombe Rafiki zetu wa Scandinavia,Watufundishe kuandika na Kusoma Mikataba haswa ya MADINI,kwani sie hatuna wataalamu hao" - JK Kikwete May'2007

Nadhani hakuna atakaekataa Hekima zilizojaa katika maneno aliyoyatoa Baba wa Taifa...

Wakuu tukumbushane Wise and Unwise qoutes kutoka kwa viongozi wetu.....
 
Zile nukuu za jk mod turudishien pliz na naomba iwekwe kwenye Sticky hadi 2015 atapomalza kipnd chake.
Hivi hizo hapo juu kuhusu wanawake na maziwa na kuzaa watoto wazuri ni kweli alisema au amesingiziwa...? alafu ile nyingine ya kwamba angekuwa na uwezo angeleta wingu na kunyesha Mtera...? duh kaazi kweli kweli nadhani sometimes ni bora kukaa kimya kuliko kuongea
 
Kweli tunakukumbuka mzee wetu...; na wosia wako utaishi milele na tukiufata utatufikisha mbali
 
"If a door is shut, attempts should be made to open it; if it is ajar, it should be pushed until it is wide open. In neither case should the door be blown up at the expense of those inside."
Julius Kambarage Nyerere, from his Stability and Change in Africa speech given to the University of Toronto, Canada, 2 October 1969.
 
Jamani hii statement kweli JK aliisema manake simaini mtu anaweza kuongea haya majambo

"Ikiwatutaruhusu wasichana waliojifungua kurudi mashuleni matiti yao yatakuwayakichirizika maziwa darasani" --- J.M.Kikwete
 
Hivi hizo hapo juu kuhusu wanawake na maziwa na kuzaa watoto wazuri ni kweli alisema au amesingiziwa...? alafu ile nyingine ya kwamba angekuwa na uwezo angeleta wingu na kunyesha Mtera...? duh kaazi kweli kweli nadhani sometimes ni bora kukaa kimya kuliko kuongea

...ngachoka!!
 
Nyerere utamchukia machoni (kwa wale wanaoigiza kumchukia) ila moyoni utampenda
Tutampendea nini? Kutuulia EAMWA na kutuanzishia BAKWATA,kuwaua wanaharakati wa uhuru wa nchi hii, katika moja ya maelezo yake amewahi kusema wakati wa harakati za uhuru aliwahi kusema kuwa Alifunga na WAISLAMU pamoja siku 3 vile vile wanaharakati wa uhuru waliokua wakimzunguka wote walikua waislmu hivyo hakua na budi kufuata taratibu za uislamu wakati huo mbona HAMYAZUNGUMZII HAYA?
 
nyerere alisema,

" upumbavu ni kama kipaji.....watu
wanakuwa na vipaji vikubwa hivi".....
 
Jamani hii statement kweli JK aliisema manake simaini mtu anaweza kuongea haya majambo

"Ikiwatutaruhusu wasichana waliojifungua kurudi mashuleni matiti yao yatakuwayakichirizika maziwa darasani" --- J.M.Kikwete

Mkuu nakudai hela ya matibabu nimevunjika mbavu tatu kwa kicheko, unitumie kwenye tiGO pesa... kwi kwi kwi teh teh teh......!!!!
 
Tutampendea nini? Kutuulia EAMWA na kutuanzishia BAKWATA,kuwaua wanaharakati wa uhuru wa nchi hii, katika moja ya maelezo yake amewahi kusema wakati wa harakati za uhuru aliwahi kusema kuwa Alifunga na WAISLAMU pamoja siku 3 vile vile wanaharakati wa uhuru waliokua wakimzunguka wote walikua waislmu hivyo hakua na budi kufuata taratibu za uislamu wakati huo mbona HAMYAZUNGUMZII HAYA?

Hayo tumekuachia wewe uyazungumzie kwani inaonyesha yanakulipa... ,
 
Tutampendea nini? Kutuulia EAMWA na kutuanzishia BAKWATA,kuwaua wanaharakati wa uhuru wa nchi hii, katika moja ya maelezo yake amewahi kusema wakati wa harakati za uhuru aliwahi kusema kuwa Alifunga na WAISLAMU pamoja siku 3 vile vile wanaharakati wa uhuru waliokua wakimzunguka wote walikua waislmu hivyo hakua na budi kufuata taratibu za uislamu wakati huo mbona HAMYAZUNGUMZII HAYA?

sikulaumu sana....tatizo umetawaliwa na akili za mafisadi...
 
Back
Top Bottom