Wingi wa Cherahani na matumizi ya neno Rambirambi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wingi wa Cherahani na matumizi ya neno Rambirambi

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Uloi nga Machi, Jan 4, 2012.

 1. U

  Uloi nga Machi Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukitazama kamuzi ya Kiswahili Sanifu, kwa kweli uwingi wa neno CHERAHANI ni MAREHANI na siyo VYERAHANI. Mpo hapo Waungwana! Pia kamusi hiyo ya Kiswahili Sanifu ya TUKI 1981, inafafanua kuwa Rambirambi pamoja na matumizi yake yanayofahamika na wengi, hutumika pia kuelezea salamu za heri apewazo mtu baada ya kufikwa na jambo jema au la furaha kama kufaulu mtihani, kushinda bahati nasibu, kuteuliwa kushika nafasi ya juu ya uongozi n.k. Inaeleweka Waungwana? Kiswahili ni bahari yenye maji male. Tuongelee na kuzamia kwa kuzitambua mantiki na balagha zake.
   
 2. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  .

  Wewe unatumia Kamusi gani wewe?! - una uhakika hiyo ni TUKI?
  Kwanza hiyo haiitwi Cherahani hiyo inaitwa Cherehani!


  Anyway, Kamusi ya TUKI inasema wingi wa Cherehani ni Vyerehani


  Tafsiri yake kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI ni hii hapa:


  cherehani[SUP]*[/SUP] nm vy- [ki-/vi-] sewing-machine. (Kaj)

  rambirambi* nm [zi-] condolences: Peleka ~send condo-lences. (Kar)


  .
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  kama unakumbuka mambo ya ngeli,
  wingi wa neno lolote linaloanzia na CH katika umoja, wingi wake lazima uanzie na V

  CHUPA-VYUPA
  CHOO-VYOO
  CHEUSI-VYEUSI
   
 4. Mukhabarat

  Mukhabarat Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Chupa haina wingi, wingi wa chupa ni chupa tusidanganyane
   
Loading...