Windows 10 kutolewa bure kwa watumiaji wa windows 7 na 8

Windows 10 kutolewa bure kwa watumiaji wa windows 7 na 8

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,253
Reaction score
44,363
kwa wale wataalamu wa ku activate windows Kuna habari mbaya leo microsoft sasa hivi ametangaza itakuwa ni buree, ukiwa na pc yenye windows 7 au 8

B749N8qIIAAjnW-.jpg

​

kuieka hii habari vizuri zaidi ni kwamba utaweza ku update bure mwaka huu toka windows 8/7 kwenda windows 10, kwa wale walio na pc mpya itabidi wanunue windows kwao haitakuwa bure.

-pia microsoft wamezindua cortana kwenye pc. huyu atakuwa ni msaidizi wako kwa ajili ya kumtuma akufanyie vitu kwenye pc mfano unaweza sema "hey cortana play my music" basi ataplay miziki yako

kwa wale wa windows phone ukiupdate kwenda windows 10 utaweza kumove keyboard kuipeleka popote pale
B75Doa1IUAAr1vq.jpg

​

pia microsoft wameonesha universal app ambazo zitakuwa zinafanya kazi kwenye pc na simu kama vile office, gallery, calendar
B75GSJECMAEBdM4.jpg

​

-microsoft wanatengeneza browser mpya ambayo code name yake ni spartan itakuja na windows 10, hii browser itakuja na reading mode ambayo ukiiactivate inatoa mambo yasiyo na maana kama sidebar na matangazo na kukuachia article yenyewe tu (hi google), pia cortana itakuwa ndani ya hii browser hivyo unaweza fanya mambo mengi kwa sauti bila kuandika tu.

-microsoft wameelezea direct x 12 kuwa itasave power hadi asilimia 50 na pia itaongeza asilimia 50 ya perfomance kwenye same hardware. ina maana kama una gpu inayosuport direct x12 tegemea perfomance boost kama hio.

-kwa wale wa windows phone update ya developer preview itakuja february

-microsoft pia wamezindua surface hub tv yenye computer ndani na kioo cha inch 84. kwa wale watangaza mipira, mikutano, na wafanyabiashara wanaoproject vitu hii ni tv yao
B75OBu_IgAEaHVX.jpg

​

and the next big thing ni windows holographic, microsoft wamezindua virtual reality yao.
B75QOihIEAE49rU.jpg

​
kuona hii virtual reality itabidi uvae kifaa hiki ambacho microsoft wanakiita HOLO LENS
B75RsVsIYAExiJ1.jpg

​

pia microsft wamezindua na studio ya hologram ambayo mtu kama mimi na wewe tunaweza tukatengeneza holo zetu, ikumbukwe vifaa vyote vya windows 10 vinaweza kurun hii hologram bila kujali bei au power hata kisimu kama lumia 520 kinaweza
habari zaidi zinakuja
 
Good news kwa wale wote watumiaj wa friend user wa OS ya windows
 
wow this is so amazing, ngoja tupate hizo holo lens maana tushachoka kutembea na simu kubwa hapa itakua mwendo wa kuswipe vitu hewani hewani
 
Sijui na samsung nae atakuja na nini kipya????
 
Good news,,,aisee hii nimeipenda,,big up kwa microsoft,,
 
Microsoft anataka arudi kama zamani.
Universal apps zitasaidia sana
 
Free? Gharama za production anazirudishaje?
Bila kupata jibu la hili swali nadhani inaweza kuwa "trap" 🙂
 
So now window 10 ipo sokoni o bado haijaanza kuuzwa! Na kama ipo bingo unainstall kwa sh ngapi msaadacolz
 
Wenye ma-PC ya kizamani kwetu ni msiba tu hata windows 8 kwetu ni ishu. Wacha nivutie upepo mini laptop najua hapo windows 10 ita-Run.
 
Free? Gharama za production anazirudishaje?
Bila kupata jibu la hili swali nadhani inaweza kuwa "trap" 🙂

1. ni free kwa mwaka mmoja baada ya mwaka ikiwa huja update utalipia.
2.ni kwa wenye windows 7 na 8 ambao wana genuine windows kwa lugha nyengine walishalipia winndows, wenye vista na xp watabidi wanunue.
3.computer mpya zinaendelea kulipiwa kama kawaida hio free ni kwa sisi tunao upgrade.

pia ujue wateja wakubwa wa ms ni enterprise na makampuni huwa hayana haraka ya ku update hadi bugs ziishe hivyo huwenda wakaanza ku update baada ya huo mwaka, hii free tumeekewa kina sisi tunaopiga kelele kuhusu bure.
 
So now window 10 ipo sokoni o bado haijaanza kuuzwa! Na kama ipo bingo unainstall kwa sh ngapi msaadacolz

sasa hivi kuna preview tu kwa wale wanaotaka kuitest ila yenyewe bado itatoka mwezi wa 4 au wa 9/10
 
Back
Top Bottom