Wimbo wa taifa uwe lazima mashuleni

Wimbo wa taifa uwe lazima mashuleni

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
312
Reaction score
614
Naandika kwa masikitiko makubwa, ni masikitiko makubwa sana, mtoto anarudi nyumbani kutoka shule amekariri nyimbo zote za kizazi kipya na hajui kabisa kama kuna wimbo wa taifa inasikitisha sana, ukienda kwenye mahafali ya shule za msingi watoto wanawekewa nyimbo za sasa ambazo nyingi zimetungwa kwa kutumia lugha chafu watoto wana kata viuno mbele ya walimu na wazazi wanachekelea..huwa najiuliza hili ni zoezi makusudi la kuuwa elimu? Kiukweli siyo sawa hata kidogo kwa sekta hii muhimu, mawaziri wenye dhamana ndio hao mwingine alisema Tanzania ni muunganiko wa Zimbabwe na Pemba, mwingine ndiye huyu “ you are going to stay inside” inatulazimu wazazii tutumie gharama kubwa sana kupeleka watoto shule zenye mitaala ya nje ya nchi inasikitisha sana, mpaka Mimi mwananchi wa kawaida nimetambua Hilo naamini kuna wadau wa sekta hii muhimu wanalijua hili ni **** anisha kwamba kuna jitihada za makusidi za kuua elimu
 
Dah aise watanzania kwa kulaumu hatujambo? Inawezekana una hoja nzuri lakini unashindwa kuiwasilisha!
Swala ni watoto kufundishwa wimbo wa taifa? Au ni kuimbishwa bongo fleva shuleni kwao? Kama wewe unaona shida mpeleke mwanao shule za dini ambazo hawaimbi au kuchezeshwa hayo ma bongo fleva!
Mbona kuna shule kwenye mahafali wanacheza hayo ma bongo fleva na kila mwaka zinafaulisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom