Wimbo wa Taifa urekebishwe!!!

Wimbo wa Taifa urekebishwe!!!

Mafisadi nani kayaweka madarakani? Viongozi mburula wana akisi (reflect) umburula wa wananchi waliowaweka madarakani. kwa mfano ELow.asa tunajuwa ni mwizi, tapeli,fisadi lakini haitoshangaza wananchi ambao wengi si wajuzi wa mambo kadha wa kadha wakimchagua kuwa kiongozi.

nadhani hata sisi wananchi tu matapeli na mafisadi ndio maana tunawachagua viongozi wa hovyo na kisha tunawaombea baraka kupitia wimbo wa taifa

capital
 
Kwanza inaonyesha tangu utotoni hadi leo hujui wimbo wa taifa ulikuwa unaimba wrong lyrics hakuna sehemu tunayoimba "wabariki viongozi wote".
 
Mm wimbo wa Taifa hata siujui tangia niache kuuimba miaka ya 80, ukizingatia nilikuwa nakaa msitari nyuma hata kuimba nilikuwa naiga tu wala hata haukukaa kichwani kabisa.

Tukueleweje?uliimba miaka ya 80 au ya 90?bado unasoma?
 
Tubadilishe na neno " Tanzania" tuweke neno " Tanganyika"

Mungu ibariki Tanganyika,
Wabariki watanganyika wote,
Dumisha umoja na amani,
Hizi ni ngao zetu,
Tanganyika na watu wake,
Ibariki............ Tanganyika
Tubariki Tanganyika na watu wake

Inapendeza.
 
Tatizo ni la watanzania wenyewe, viongozi wake wote wanatakiwa kubarikiwa. Ila sisi tunawaweka viongozi wabovu! Fikiria kama tungeweka viongozi wazuri, hii nyuzi isingekuwa na mashiko. Tatizo sio wimbo, kwanza si 'wabariki viongozi wote' bali ni 'wabariki viongozi wake'.
 
Wakuu wa mikoa,walaya,wakurugenzi, wakuu wa majeshi nk. ni nani anawaweka?
 
Back
Top Bottom