Wimbo wa Rayvany(natafuta kiki) ni mwigo. Haustahili sifa unazomwagiwa

gasto genaro

JF-Expert Member
Oct 15, 2014
780
554
Wimbo wa Ray Vany (Natafuta Kiki) ni MWIGO. Haustahili sifa unazomwagiwa.

Na: Gasto Di Genaro

Ray Vany ni msanii mchanga anaekuja kwa kasi sana kutoka kwa Lebo ya WCB.


Ray hadi wakati huu amesha achia Single mbili ambazo kwasasa zinafanya vizuri sokoni. Single yake ya kwanza ni ile iitwayo KWETU ambayo kusema kweli ni nzuri na inavutia. Na single yake ya pili ni ile iitwayo NATAFUTA KIKI.


Kimsingi watu wengi wamekua wakiisifu hii single(natafuta kiki) kuwa ni nzuri. Lakini single hii isingetakiwa imwagiwe sifa hizo zote kwani ni MWIGO wa nyimbo ya YOUNG KILLER.

Young Killer alishawahi kutoa wimbo wenye maudhui na style kama hiyo uitwao MISS SUPERSTAR Tofauti ya nyimbo hizo mbili ni Aina ya uimbaji.

Ray kamuiga Young Killer kutokana na ukweli kuwa, Young Killer alikua akizungumzia kuwatamani Warembo wa TZ ambao ni masuperstar, na ndicho alichokifanya Ray sema tu akabadilisha style ya uimbaji.


Hivyo basi, wimbo wa Ray hauna ubunifu zaidi ya mwigo na hauhitaji kupata sifa unazozipata.


Gasto Di Genaro
Shabiki wa kufa wa Man Utd
 
Back
Top Bottom