Wimbo wa Kombe la Dunia 2026 ni mbaya; hauna hadhi ya michuano hiyo, umekaa kama Kwaya ya kanisani

Wimbo wa Kombe la Dunia 2026 ni mbaya; hauna hadhi ya michuano hiyo, umekaa kama Kwaya ya kanisani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Bado siku 79 hadi mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. Mechi ya ufunguzi itachezwa Alhamisi, 11 Juni 2026 mjini Mexico, na ratiba ya FIFA inaonyesha mchezo huo ni Mexico dhidi ya Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana (The Boys in Zulu).

1774333046923.png

Tayari Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) limeachia wimbo rasmi wa michuano hiyo unaitwa 'Lighter' umeimbwa na Jelly Roll kwa ushirikiano na Carín León chini ya FIFA Sound.

1774333406709.png
Muda mfupi baada ya wimbo huo kuachiwa, baadhi ya wadau wa Soka wameuponda sana, wanasema haukidhi matarajio waliyozoea kwenye nyimbo za mashindano haya, na kwamba hauna vibe ya World Cup.

Mashabiki wamezoea nyimbo kama Waka Waka (2010), Dreamer (2022), Colors (2018) We Are One (2014) na nyingine ambazo zina mchanganyiko wa Afro/Latin na beat za kuchezeka, za kuaamsha, ambazo si rahisi mashabiki kusinzia Uwanjani. Huu wao wanaona umekaa kama wimbo wa simulizi ya huzuni, soundtrack au Kwaya 😅

Pia hata wasanii walioimba, baadhi wanajiuliza kama Jelly Roll ana hata connection kweli na soka; collabo yake na Karín León kwa wengi imeonekana kama imeharibu zaidi kuliko kuvutia.

Baadhi ya nyimbo maarufu za Kombe la Dunia ambazo zilibamba;

2010 – Waka Waka (This Time for Africa) — Shakira ft. Freshlyground
2010 – Wavin' Flag
- K'naan
2014 – We Are One
(Ole Ola) — Pitbull, Jennifer Lopez & Claudia Leitte
2014 – La La La
Shakira
1998 – La Copa de la Vida
– Ricky Martin
2018
Colors Jason Derulo
2022
Dreamer — South Korean singer Jung Kook ft. Fahad Al Kubaisi

Soma zaidi kuhusu Kombe la Dunia;

 
Back
Top Bottom