Wimbi la uvaaji wa nguo fupi kuongezeka

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
15,836
22,948
Wadau,

Nimeona nilete jamvini hii mada ili tuijadili. Miaka kadhaa ya nyuma serikali ilikuwa ikitoa matamko na makaripio makali juu ya uvaaji wa nguo fupi kwa wanawake lakini nimegundua wimbi la uvaaji wa nguo fupi kuongezeka siku za hivi karibuni na naona serikali iko kimya kwenye hili.

Sikatai kuwa wanapendeza lakini tukiwa katika wakati huu ambapo tunapambana na ugonjwa wa UKIMWI serikali haioni kwamba vita hii haitakuwa na mwisho zaidi ya kutumia pesa nyingi kwenye mapambano ya huu ugonjwa kwani ni jambo lisilofichika kuwa baadhi ya sehemu ya miili ya wanawake inapoachwa wazi huvuta hisia za mapenzi kwa kushawishi tendo la ndoa kwa wanaume.

Nawasilisha.
 
Wadau nimeona nilete jamvini hii mada ili tuijadili.Miaka kadhaa ya nyuma serikali ilikuwa ikitoa matamko na makaripio makali juu ya uvaaji wa nguo fupi kwa wanawake lakini nimegundua wimbi la uvaaji wa nguo fupi kuongezeka siku za hivi karibuni na naona serikali iko kimya kwenye hili.Sikatai kuwa wanapendeza lakini tukiwa katika wakati huu ambapo tunapambana na ugonjwa wa UKIMWI serikali haioni kwamba vita hii haitakuwa na mwisho zaidi ya kutumia pesa nyingi kwenye mapambano ya huu ugonjwa kwani ni jambo lisilofichika kuwa baadhi ya sehemu ya miili ya wanawake inapoachwa wazi huvuta hisia za mapenzi kwa kushawishi tendo la ndoa kwa wanaume,nawasilisha.
Vipi kuhusu sigara mzee? Huoni kuwa kuna haja ya kufunga kiwanda cha uzalishaji?
 
Kuhusu swala la joto Bonesmen sidhani kama Dar kuna joto zaidi ya Saudi Arabia,Ethiopia,Somalia n.k ambako pamoja na kuwa na joto kali vazi la hijabu linavaliwa na kuhusu sheria juu ya dress code zipo ila hazifuatwi,karibu kwenye mjadala.
 
Hata kama ni uhuru wa mtu kuvaa apendavyo ila vinguo vingine ni kukosa tu maadili...Kisketi kiko juu ya magoti yeye mwenyewe ukimkuta kwenye daladala hayuko komfotabo kabisa ni kujifunika tu na kipochi hapo kati...Akitembea sasa anavyojirusha rusha..Ndiyo maana kuna maeneo Arusha ukipita umevaa vaa kizembe hivyo sijui sketi fup ama wanaume kata K unakamatwa unakula viboko 70 unaachwa uende zako...
 
Ahhahhahahaahaha Mwanamke wa Dunia ya sasa na Mwanaume wa Dunia ya Kale, hapo mbona balaa. Mkuu vumilia tuu ifanye kama kawaida, ukimuona kavaa nguo fupi fumba macho na chukulia kavaa hijab. Serikali haiwezi kwa sasa kuingilia issues za dress code kwa wananchi wake, ishachelewa. Hii inafanana na biashara ya ukahaba Duniani kote ambapo hakuna nchi inayojivunia kumaliza ukahaba.
 
Labda tujiulize hili swali dogo tu,

nini "Lengo" kuu au "Sababu kuu" inayopelekea mwanamke kuvaa nguo fupi?
 
Haipendez hasa nnguo ikiwa fupi kupitiliza...Thamani ya mwanamke mbele ya jamii inaongezwa pia kwa kujistir
Btw hakuna la kuwafanya wavae japo gauni iguse magoti..wakipita lbarqbarani tunawaangalia tu then tunaendelea na yetu..Kamshindwa mzazi wake utaweza we jirani?
 
Back
Top Bottom