Watoto wa viongozi hawawezi kuleta mabadiliko yenye tija kwa Taifa.Sidhani kama watawachukulia hatua wazazi wao walioshiriki kwenye ufisadi.Sana sana wataendeleza ufisadi kwa kutumia mbinu mpya.Shida si kutawala,bali kutaka kuendelea kuwa madarakani by any means neccessary.
Kama tutakubali kufuata sheria hili la watoto wa vigogo ama vijiti halitakuwepo kwani si mtoto wa kigogo au kijiti mwenye kuwajibisha ama ku promote bali utawala wa sheria na pale panapotokea mgongano wa kimaslahi ni wazi anayehusika kuliweka wazi hilo. Tatizo letu viongozi wetu waliamua kuiweka sheria kando na kutumia hisia zao kuongoza nchi. Hili lilisababisha mambo yaliyokuwa ya aibu kuwa halali na kuathiri maadili ya watanzania kiasi kwamba majambazi ndiyo sasa wanaonekana mashujaa na wakitoa sauti watu wote wana nyamaza. Niwe mkweli kiongozi kama rais asipokuwa mfano wa kuigwa kiutawala wa sheria na kimaadili walio chini yake huiga kwa haraka sana na hatimaye kusababisha kujenga utamaduni huo kwa kasi usiyoweza kutegemea.
Wengine tulipata kazi bila kupeleka vimemo ofisini kwa mtu yeyote Lakini sikuhizi watoto wetu ndiyo wanaotoa instruction kwa mwajiri na kumwelekeza sehemu anayotaka kufanya kazi na kazi zipi azifanye kisa mimi baba/mama/shangazi/mjomba/shemeji ndiye mkubwa. Matokeo ni kuwa taifa lina watu ambao wapo kwenye nafasi wasizo stahili kiasi kwamba wana underperform na wakikosolewa wao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho hivyo kuamua kuwawajibisha hao wanaowakosoa badala ya kukubali kuwa hizo nafasi hawa stahili kwa faida yao wenyewe na kwa taifa.
Pia kuna tabia imejitokeza ya kufanya cartel kwenye biashara hasa kwakutoa information kwa clout fulani hivi ya politicians na ndugu zao huku raia wengine wenye ujuzi pengine na capacity wakiachwa nje na kusababisha biashara zao zishindwe kuhimili na hivyo kujikuta zikifa. Athari inayotokea ni kuwa hizo biashara zilitoa ajira kwa group kubwa la raia hivyo zinaposhindwa kuendelea inaleta impact kwa raia wengi. Hizi zingine kwakuwa haziendeshwi kitaalamu na pia zinakuwa highly subsidized indirectly na hivyo ile labour inayotakiwa pengine iwe provided na raia zinafanywa na machine ambazo ukizifanyia financial na economic analysis haziko viable ila kwakuwa zinapata indirect subidies hili haliwezi kuonekana mpaka huo mrija utakapokatwa huyo kigogo akipata kwamfano ajali ya kisiasa na kutoka kwenye hiyo nafasi basi utaona hizo biashara zinajifia na hivyo kutoa picha halisi kuwa ilikuwa si biashara bali mrija wakupitishia pesa za kifisadi na spending ya hizo pesa ni kwenye foreign goods so hakuna reinvestment. Hili tusipolikemea tax base yetu itaendelea kusinyaa na hata ukusanye vipi kodi bado itakuwa haitoshi maana walaji ni wengi kuliko wazalishaji.
Kwaujumla taifa limeingia kwenye tabia ambayo bila kuja na sheria kali zenye kumaanisha si rahisi kurekebisha hii tabia. Maadili hayaji bila kuwepo na sheria zenye kurekebisha tabia za watu ndiyo maana tunasema Azimio la Arusha ni muhimu sasa kuliko wakati mwingine wowote.