William Kusila aitabiria kifo CCM

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
8,310
11,152
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma, William Kusila amesema kuwa Tanzania inaelekea kuzimu na kwamba hakuna namna tena ya kukifanya chama hicho kikawa na heshima.

Kusila ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, alishindwa kutetea nafasi yake baada ya kuambulia kura 216 dhidi ya mpinzani wake, Adam Kimbisa aliyezoa kura 948.

Akizungumza kwa simu kutoka kijijini kwake Mtitaa, Dodoma, Kusila ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Bahi, alisema moyo wake umepata kunyanzi na chama hicho licha ya kuwa ataendelea kuwa mwaminifu na mtiifu kwacho.

"Kwanza naililia nchi yangu, pili nakililia chama changu cha Mapinduzi ambacho daima dumu nitabaki kuwa mwanachama mwaminifu kwake, lakini siogopi kusema hadharani kuwa nchi hii sasa inaelekea mochwari na chama ndicho kinaelekea mwisho, '' alisema Kusila na kuongeza:

"Watu wanatumia hela nyingi sana kununua kura, huku vyombo vya dola vikiangalia utadhani havipo au havioni. Jambo hili linaniuma sana, nikiitazama nchi yangu ikiyumba mbele ya macho yangu naumia kwa kiasi kikubwa lakini basi."

Hata hivyo, Kusila alisema kuwa licha ya kuendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa chama hicho lakini anadhani kuwa CCM kimeyeyuka moyoni mwake na kwamba kilichobaki ni mapenzi ya juu-juu na ushabiki kama ilivyo kwa wengine.

Alisema Watanzania wanatakiwa kuililia na kuiombea nchi yao na hasa chama chao ambacho ndicho chenye dhamana ya kuiongoza nchi na ndicho kilichoshika dola.

Alipotakiwa kueleza juu ya makundi ndani ya CCM alisema hajui lakini anachofahamu ni juu ya kuwapo wenye fedha ambao hawana malengo yoyote ndani ya chama hicho zaidi ya kuonyesha utajiri wao.

Alipoulizwa kama maneno hayo yanatokana na hasira za kushindwa Kusila alisema: "Kama wanasema kuwa ni maneno ya mfamaji eti tunasema kwa sababu ya kushindwa nafasi zetu, acha waseme maana hata Sumaye alisema lakini sijui wanayachukuliaje…Nami leo nimesema na niko tayari kwa lolote kama watasema kwa nini nilisema hivyo."

Iringa wachaguana
Kada wa CCM na Mkurugenzi wa Shule za Star International, Jesca Msambatavangu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Iringa baada ya kumshinda mpinzani wake, Joseph Muhumba.

Jesca ameshinda kiti hicho baada ya uchaguzi huo uliokuwa ukisimamiwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima kurudiwa kutokana na kutopatikana mshindi kwa mujibu wa taratibu za chaguzi za chama hicho.

Katika uchaguzi huo, Jesca alipata kura 387 akifuatiwa na Muhumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo aliyepata kura 235.

Katika awamu ya kwanza iliyoamua kurudiwa kwa uchaguzi huo, Jesca aliongoza kwa kura 271, Muhumba kura 201 na Godfrey Mosha alitupwa nje baada ya kupata kura 183.

Kivumbi Mwanza leo
CCM Mkoa wa Mwanza leo kitapata viongozi wake katika uchaguzi unaotarajiwa kuwa na mchuano mkali. Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Clement Mabina anatetea nafasi hiyo huku akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Ilemela na Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo.

Wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo ni Mwenyekiti wa zamani wa Mkoa wa Mwanza, Joseph Yaredi, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Athuman Zebedayo pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Hussein Mashimba.

Wachunguzi wa masuala ya siasa wanaeleza kwamba iwapo nguvu za Diallo na Mabina zitalingana, zinaweza kuwa ahueni kwa Zebedayo na Mashimba ambao wanaonekana kuwa na kasi inayoweza kutoa matokeo yasiyotarajiwa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga alisema uchaguzi huo utafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba... "Ni imani yetu uchaguzi utafuata misingi ya kidemokrasia na wagombea watapata nafasi ya kujieleza kwa wajumbe wao kisha kuomba kura."

Joto lapanda Kilimanjaro
Homa ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kilimanjaro inazidi kupanda huku mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Thomas Ngawaiya akibatizwa jina la ‘Kunguru hafugiki' ili kumchafua.

Mchuano mkali katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Alhamisi unatajwa kuwa kati ya Ngawaiya na Meneja Rasilimali Watu wa zamani wa Kiwanda cha Sukari TPC, Idd Juma.

Wengine wanaowania nafasi hiyo ni Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, James Kombe na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa anayemaliza muda wake, Midred Kisamo.

Imedaiwa kwamba sababu za Ngawaiya kupewa jina hilo ni kutokana na kuhamahama vyama. Kabla ya kuhamia CCM, Ngawaiya alikuwa Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) na kabla ya hapo alikuwa na wadhifa kama huo NCCR -Mageuzi, chama ambacho kilitikisa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995.

Habari zinadai tangu awali, Ngawaiya hakupewa alama za kuwa miongoni mwa wagombea watatu na kwamba jina lake lilirejeshwa na Halmashauri Kuu ya CCM (Nec).

Akizungumzia madai hayo, Ngawaiya alisema siku zote mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe... "Sifugiki kivipi wakati hao wanaosema hawajafanya kazi kuliko nilizofanya na zote nimezifanya ndani ya CCM." Alisema kampeni hizo chafu zinamjenga zaidi kuliko kumchafua.

Guninita akubali matokeo
Akizungumza kwa simu jana, Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam aliyeshindwa, John Guninita alikubaliana na matokeo akisema: "Asiyekubali kushindwa si mshindani."

"Katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, nakubali nimeshindwa sikuona tatizo lolote, uchaguzi ulikuwa huru na haki."

Katika uchaguzi huo Guninita alipata kura 214 na kuangushwa na Ramadhani Madabida aliyepata kura 310 huku Madson Chizii akipata kura 52.

Source: Gazeti la Mwananchi

My take:
Watu wengine wakisema wanadai watasubiri sana kifo cha CCM, vipi kuhusu hawa makada wao?? Well one can say, wana uchungu wa kushindwa, lakini there is something very wrong. Wote wanalalamikia matumizi mabaya ya fedha katika chaguzi. Mbona hili CCM hawataki kulizungumzia?
 
Ina maana hawa jamaa wanaotafuta madaraka ndani ya CCM huwa hawaijui ilivyo mpaka wanapokosa madaraka? Nakumbuka ile CCM iliyotupiwa baharini huko Zanzibar ilikuwa na msemo wa "CHEO NI DHAMANA" inaonekana umeshasahaulika.
 
Naye Kusila haeleweki, anakiri kuwa chama kinaelekea kuzimu na yeye anasema kamwe hataondoka katika chama mfu basi naye ni mfu, kwi kwi kwi kwi. Kumbe mojawapo ya sifa kubwa za kuwa mwana CCM ni kuwa mnafiki.
 
Huyu Kusila vipi? Anasema chama cha mapinduzi lazima kife, halafu hapo hapo anasema ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM maisha yake yote!!
 
Sawa mzee, kabana na tai yako shingoni ili Historia ije iwahukumu vizuri.
 
Hii inapaswa kusomwa na MUKAMA

Kusila ni wewe unayeongea maneno haya leo? si ulimrithi Ndejembi wewe? umesahau zile fitna? si ni wewe ulieimalizia ngome ya kina Chigwiye misi baada ya Ndejembi? Kwa muda wote wa ubunge pale Bahi umefanya nini zaidi ya pombe kwa makanda, mifegi na vinyaso? oh mla huliwa, mbaya zaidi (si kwa nia mbaya lakini Dodoma ni ya wagogo) wewe leo umepeleka kiti kwa warangi? ha ha ha, ni fitna kweli? ni rushwa? au ni underperformance na kushindwa kumeet expectations za watu? ni mawazo tu wala usimaindi kwanza umezeeka sana, nenda kasimamie miradi yako ya kilimo uliyoianzisha, tena ina tija zaidi na impact kwa wananchi coz wanajifunza kitu kwa vitendo.
 
Huyu James Kombe kadi ameikata lini, ikiwa polisi hawaruhusiwi kuwa makada wa chama chochote? Kumbe kweli huwezi kupanda cheo bila kuwa kada wa CCM!
 
Naichukia hii style ya kupigwa chini ndio unakosoa... alikuwa wapi kuyasema haya? na Style ya kuwa na vyeo vitano vitano mtu mmoja, Huyo kimbisa si ni Mbunge wa EA sasa huo Uenyekiti wa nini?
 
Hivi haya mambo ya rushwa na matumizi ya pesa huwa hawayaoni kabla ya uchaguzi au ni vipi
Maana inaelekea wakishamwagwa kwenye uchaguzi ndo wanakuja na story za kuwa kuna rushwa na matumizi mabaya ya fedha
Je kabla ya kugombea na kwenye kampeni mpaka kura zinahesabiwa walikuwa hawayaoni
Tungetarajia kabla ya uchaguzi mwenye ujasiri atoke asimamishe uchaguzi kwa kuwa ameona matumizi makubwa ya pesa au rushwa inatembea kwa sana
Ila hayo huwa hawayaoni wakishaangushwa wanaanza kubwabwaja na kusema kuna rushwa
Mhhh Kombe yale yale ya Alfred Tibaigana
Kumbe ni wana magamba dam damu hata wakiwa kwenye kazi zao ila wanaficha kadi zao wakiwa wamevaa zile kofia na magwanda yao
 
William Kusila anashangaza kulalamikia rushwa leo baada ya yeye kuwa ameshindwa uchaguzi kwa njia ya rushwa. Inashangaza sana tena sana kumsikia akisema yuko tayari kuendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM licha ya kuwa anaona chama hicho kinaipeleka nchi kuzimu na chenyewe kinaelekea kuzimu. Nilitegemea sasa anyanyuke na kuusema ukweli na kuwaambia wana wa nchi hii kinachoendelea ndani ya ccm ili kuiepusha nchii hii kwenda kuzimu. Kwa kutofanya hivyo,ameonesha udhaifu mkubwa sana tena sana kwa nchi hii. Kuwa na wazee wasio na tija kama Kusila ni laana kabisa. Poor Kusila
 
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma, William Kusila amesema kuwa Tanzania inaelekea kuzimu na kwamba hakuna namna tena ya kukifanya chama hicho kikawa na heshima.

Kusila ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, alishindwa kutetea nafasi yake baada ya kuambulia kura 216 dhidi ya mpinzani wake, Adam Kimbisa aliyezoa kura 948.

Akizungumza kwa simu kutoka kijijini kwake Mtitaa, Dodoma, Kusila ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Bahi, alisema moyo wake umepata kunyanzi na chama hicho licha ya kuwa ataendelea kuwa mwaminifu na mtiifu kwacho.

"Kwanza naililia nchi yangu, pili nakililia chama changu cha Mapinduzi ambacho daima dumu nitabaki kuwa mwanachama mwaminifu kwake, lakini siogopi kusema hadharani kuwa nchi hii sasa inaelekea mochwari na chama ndicho kinaelekea mwisho, '' alisema Kusila na kuongeza:

"Watu wanatumia hela nyingi sana kununua kura, huku vyombo vya dola vikiangalia utadhani havipo au havioni. Jambo hili linaniuma sana, nikiitazama nchi yangu ikiyumba mbele ya macho yangu naumia kwa kiasi kikubwa lakini basi."

Hata hivyo, Kusila alisema kuwa licha ya kuendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa chama hicho lakini anadhani kuwa CCM kimeyeyuka moyoni mwake na kwamba kilichobaki ni mapenzi ya juu-juu na ushabiki kama ilivyo kwa wengine.

Alisema Watanzania wanatakiwa kuililia na kuiombea nchi yao na hasa chama chao ambacho ndicho chenye dhamana ya kuiongoza nchi na ndicho kilichoshika dola.

Alipotakiwa kueleza juu ya makundi ndani ya CCM alisema hajui lakini anachofahamu ni juu ya kuwapo wenye fedha ambao hawana malengo yoyote ndani ya chama hicho zaidi ya kuonyesha utajiri wao.

Alipoulizwa kama maneno hayo yanatokana na hasira za kushindwa Kusila alisema: "Kama wanasema kuwa ni maneno ya mfamaji eti tunasema kwa sababu ya kushindwa nafasi zetu, acha waseme maana hata Sumaye alisema lakini sijui wanayachukuliaje…Nami leo nimesema na niko tayari kwa lolote kama watasema kwa nini nilisema hivyo."

Iringa wachaguana
Kada wa CCM na Mkurugenzi wa Shule za Star International, Jesca Msambatavangu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Iringa baada ya kumshinda mpinzani wake, Joseph Muhumba.

Jesca ameshinda kiti hicho baada ya uchaguzi huo uliokuwa ukisimamiwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima kurudiwa kutokana na kutopatikana mshindi kwa mujibu wa taratibu za chaguzi za chama hicho.

Katika uchaguzi huo, Jesca alipata kura 387 akifuatiwa na Muhumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo aliyepata kura 235.

Katika awamu ya kwanza iliyoamua kurudiwa kwa uchaguzi huo, Jesca aliongoza kwa kura 271, Muhumba kura 201 na Godfrey Mosha alitupwa nje baada ya kupata kura 183.

Kivumbi Mwanza leo
CCM Mkoa wa Mwanza leo kitapata viongozi wake katika uchaguzi unaotarajiwa kuwa na mchuano mkali. Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Clement Mabina anatetea nafasi hiyo huku akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Ilemela na Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo.

Wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo ni Mwenyekiti wa zamani wa Mkoa wa Mwanza, Joseph Yaredi, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Athuman Zebedayo pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Hussein Mashimba.

Wachunguzi wa masuala ya siasa wanaeleza kwamba iwapo nguvu za Diallo na Mabina zitalingana, zinaweza kuwa ahueni kwa Zebedayo na Mashimba ambao wanaonekana kuwa na kasi inayoweza kutoa matokeo yasiyotarajiwa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga alisema uchaguzi huo utafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba... "Ni imani yetu uchaguzi utafuata misingi ya kidemokrasia na wagombea watapata nafasi ya kujieleza kwa wajumbe wao kisha kuomba kura."

Joto lapanda Kilimanjaro
Homa ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kilimanjaro inazidi kupanda huku mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Thomas Ngawaiya akibatizwa jina la ‘Kunguru hafugiki' ili kumchafua.

Mchuano mkali katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Alhamisi unatajwa kuwa kati ya Ngawaiya na Meneja Rasilimali Watu wa zamani wa Kiwanda cha Sukari TPC, Idd Juma.

Wengine wanaowania nafasi hiyo ni Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, James Kombe na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa anayemaliza muda wake, Midred Kisamo.

Imedaiwa kwamba sababu za Ngawaiya kupewa jina hilo ni kutokana na kuhamahama vyama. Kabla ya kuhamia CCM, Ngawaiya alikuwa Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) na kabla ya hapo alikuwa na wadhifa kama huo NCCR -Mageuzi, chama ambacho kilitikisa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995.

Habari zinadai tangu awali, Ngawaiya hakupewa alama za kuwa miongoni mwa wagombea watatu na kwamba jina lake lilirejeshwa na Halmashauri Kuu ya CCM (Nec).

Akizungumzia madai hayo, Ngawaiya alisema siku zote mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe... "Sifugiki kivipi wakati hao wanaosema hawajafanya kazi kuliko nilizofanya na zote nimezifanya ndani ya CCM." Alisema kampeni hizo chafu zinamjenga zaidi kuliko kumchafua.

Guninita akubali matokeo
Akizungumza kwa simu jana, Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam aliyeshindwa, John Guninita alikubaliana na matokeo akisema: "Asiyekubali kushindwa si mshindani."

"Katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, nakubali nimeshindwa sikuona tatizo lolote, uchaguzi ulikuwa huru na haki."

Katika uchaguzi huo Guninita alipata kura 214 na kuangushwa na Ramadhani Madabida aliyepata kura 310 huku Madson Chizii akipata kura 52.

Source: Gazeti la Mwananchi

My take:
Watu wengine wakisema wanadai watasubiri sana kifo cha CCM, vipi kuhusu hawa makada wao?? Well one can say, wana uchungu wa kushindwa, lakini there is something very wrong. Wote wanalalamikia matumizi mabaya ya fedha katika chaguzi. Mbona hili CCM hawataki kulizungumzia?

Hii sasa imekuwa kama sera, kila anayeshindwa uchaguzi.
 
Baba wa Taifa alisema CCM si mama yangu wala baba yangu, akimaanisha kwamba kutoka kwake halitakuwa jambo la ajabu. Na nina imani kuwa kama Mwalimu Nyerere angekuwepo mpaka sasa asingekuwa ndani ya CCM. Sasa Kusilla yeye anataka kufia ndani ya CCM inayokufa? Hii nayo ni ajabu ya mwaka.

Wito wangu kwa Kusilla na wengine wa namna yake, tokeni acheni woga wa kijinga. Msikubali kuwa wafu ndani ya CCM mfu.

Mimi siombi CCM ife ila naomba kiwe chama makini cha upinzani baada ya uchaguzi 2015
 
Huyu Kusila vipi? Anasema chama cha mapinduzi lazima kife, halafu hapo hapo anasema ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM maisha yake yote!!

Naona blai Kusila amechanganyikiwa baada ya kushindwa; hajui sasa mshiko wake utatoka wapi!!
 
Usikubali kudanganyika, Hakuna mtu anayeshinda ucahguzi CCM bila rushwa. Kusila kama mwenyekiti anayemaliza muda wake na yeye alishinda kwa rushwa sema sasa amepata wa kumzidi ndio maana analalamika.
Narudia, CCM hakuna mtu anayeshinda uchaguzi bila rushwa.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom