Will the Greying Obama end up like Johnson (LBJ)? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Will the Greying Obama end up like Johnson (LBJ)?

Discussion in 'International Forum' started by m_kishuri, Jul 19, 2010.

 1. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  [​IMG]


  [​IMG]

  Takriban wiki tatu zilizopita nilishangazwa kidogo nilipomuona Kaka Raisi Baraka Obama akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano wa G8 mjini Toronto-Canada......Labda ni macho yangu, lakini nimethibitisha yale yanayosemwa na wengi kwamba UZEE unamnyatia kwa kasi sana. Mvi zimeongeka kichwani tofauti na alivyoingia madarakani mwaka moja uliopita. Lakini baada ya kutafakari kwa kina, nikakiri kwamba mitihani aliyonayo imekuwa mingi sana. Kwa mfano:
  · Karithi vita mbili 1/. Iraq 2/. Afghanistan
  · Kaingia madarakani na kukutana na hali mbaya ya kiuchumi ambayo Dunia haijawahi kushuhudia tangu the Great Depression ya 1939.
  · Hivi karibuni imemlazimu amuondoe Gen. Macrystal kwa ukosefu wa nidhamu na imani kwa wakubwa zake katika vita vya Afghanistan
  · Uongozi wake umeonekana unawalakini kwa jinsi alivyoshughulikia suala Gulf Coast ((Haswa baada ya kushuhudia yaliyomkuta Kichaka Bush wakati wa Katrina). Sasa hivi mambo yameanza kuwa mazuri huko Luouisiana Coast.
  · Ukosefu wa kazi (Unemployment 9.5) umeendelea kuvuruga vichwa vya Wamarekani. Kwa mujubu wa taarifa hivi karibuni, watu 125, 000 wamepoteza kazi, huku sekta binafsi ikwa imeajiri wat 80,000 tu. Wamarekani milioni 14.6 hawana kazi kulinganisha na 15. 3 April (http://www.bls.gov/)
  · Wamarekan weusi, ambao wengi hawana kazi kulinganisha na Wazungui (14- 17%) wanazidi kulalamika kwa jinsi Obama alivyowasahau (96% walimchaguwa)
  · Spanish nao wanalalamika kutokana na tatizo la Immigration Reform
  · Gay, Lesbians and Transgendered nao vilevile wanalalamika kuhusu haki yao jeshini (Don’t ask, Don’t Tell) n.k
  · Oh, nilitaka kusahau deficit! Mpaka leo asubuhi ilikuwa imefikia 13, 252, 218, 476, 300.36 (http://www.brillig.com/debt_clock/)

  Lakini kivumbi alichonacho kama raisi wa 44, ni kuepuka kumaliza uraisi wake kama President Lyndon B. Johnson, ambaye baada ya term moja tu, akabwaga manyanga kutokana na Vita vya Vietnam. Sasa brother Obama anavita mbili mikononi mwake: Vita vya Afghanistan, na ambayo inonekana kama Fiasco, na Vita vya Iraq ambavyo bado mustakabali wake haujajulikana.

  LBJ baada ya kurithi kiti cha uraisi baada ya kifo cha John F. Kennedy, alianzisha mabadiliko makubwa sana ya kijamii (Social Reforms) kama vile The Civil Rights Act of 1964 (Ambayo iliwapa Black Americans haki sawa na Wazungu) na Medicare kwa wazee na Medicaid kwa maskini. Lindon Johnson angeweza kufanya mabadiliko mengi zaidi kama isingekuwa vita vya Vietnam (1963-1975).

  Kwa mujibu wa Bloomberg News;
  “Obama’s record is comparable to what Lyndon Johnson, another Democrat, achieved in 1965 with his “Great Society” programs. That agenda, the most ambitious since Franklin Roosevelt’s New Deal, included the Voting Rights Act of 1965, the creation of Medicare and Medicaid, and a national beautification program. It also entailed a major escalation of U.S involvement in the Vietnam War, which ultimately destroyed Johnson’s” (Bloomberg.com March 9, 2009).

  Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ile vita ya Vietnam na vita vya sasa vya Aghanistan vinavyonazidi kushabihiana. Taliban wameonyesha mbinu zilezile za kubadilika kutokana na mazingira kama walivyokuwa Waviet-cong. Maaman lazma ajuwe kwamba itakuwa vigumu sana kwa Marekani kushinda hii vita hata kama ataongeza wanajeshi (sasa hivi kuna 94,000 U.S Personnel in Afghanistan). Kadri siku zinavyokwenda ndio vita hii inavyozidi kuwa unpopular.

  Kama alivyosema gwiji wa habari Tom Friedman, katika makala yake What’s Second Price? (http://www.nytimes.com/2010/06/23/opinion/23friedman.html?_r=1&ref=thomaslfriedman)
  Kwamba “Your only real choices are lose early, lose late, lose big, or lose small.”

  Katika historia ya dunia, vita imechangia kwa kiasi kikubwa kuanguka kwa Empires nyingi duaniani. Kwa mfano, Empire kubwa kama vile Sparta, Roman, Mongol, British, na hata German ziliangushwa na vita. Kwa upande wa Marekani, vita mbili (Afghanistan na Iraq) changanya na hali ya kiuchumi sasa hivi iliyosababishwa na Big Banks imongeza mambo kuwa magumu

  Kashehse ni je what other alternative does he have ili kuwaridhisha Wamarekani? Akiondoa majeshi ya Marekani kutoka Afghanistan, halafu kuwe na shambulio lolote la kigaidi Marekani, The Republican wameula. Na kwa kadri anavyoendelea kujikita kwenye hii vita, ndivyo mustakabali wa uongozi wake unavyozodi kuwa mgumu. If thing goes wrong (kwa kila kitu) Obama gets blamed.

  NB: Ahmed Rashad wa ESPN, katika moja ya mahojiano na channel hiyo katika kumbukumbu za pambano la Mohamed Ali na Joe Fraser la 1971, ambalo Ali alishindwa, alisema kwamba kushindwa kwa Ali kuliwaliza watu wengi sana, haswa Blacks . Akaongeza kwamba kilichowaliza sana sio kwa sababu ya kushindwa pambano hilo, bali ni kama vile kila kitu ambacho Mohamed Ali stood for (yaani Equal rights, freedom of religion, kupinga vita vya Vietnam, na Racism) vilikuwa navyo vimeshindwa. Natumaini kwamba hali hii haitatukuta wakatu huu wa Kaka Obama. Kwani kuchaguliwa kwake kumeleta faraja kubwa kwa maskini, wahamiaji, na colored people dunia nzima.

  N.B: Kwa taarifa zaidi kuhusu vita vya Afghanistan, soma makala ya Richard Haas kwenye Newsweek toleo la wiki ijayo : Rethink Afghanistan Because Nation Building Is Not Working And We A re Not Winning.
  http://blogs.reuters.com/pakistan/2010/07/18/richard-haass-on-afghanistan-time-to-scale-down-u-s-ambitions/
   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  God bless president Obama.
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Sioni issue ya hizi wars ikimwangusha Obama maana Majeshi yote yatakuwa yameondoka kabla ya 2012,lakini hawa Americans wengi ni nyoko tuu hata uwafanyie nini na ndio maana walimchagua dubya twice na ali wa screw kisawasawa,acha wawarudishe Republican waje na mafia policy zao labda second time watajifunza,i really dont care acha republican washinde watakao suffer ni hao hao wazungu maskini tuu wanaowapigia kura.
   
 4. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Freedom without limits+Lazy american young generation=Fall of USA.
   
 5. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  You mean will the greying Obama be ended by a Johnson?
   
 6. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  I meant Lindon B. Johnson, who served as the 36th of the United States from 1963 to 1969.
  [​IMG]
   
 7. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,086
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  I like that...kama tunavyo sema waswahili bwana
  "mtoto akililia wembe acha umkate" waache
  wachague mmafia mwingine ili baba wa watu
  apumzike na kulea mabinti zake. Kama historia
  alishaiweka.
   
Loading...