Wilaya ya Rungwe na upungufu wa maji

Wilaya ya Rungwe na upungufu wa maji

queen of the jungle

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2017
Posts
228
Reaction score
430
Pamoja na kwamba Wilaya ya Rungwe ni miongoni mwa wilaya zenye mvua nyingi na vyanzo vingi vya maji lakini cha kushangaza baadhi ya mitaa wakina mama wanajitwisha ndoo kichwani, miaka ya nyuma kulikuwa hakunaga shida ya maji hii ilitokana na uchache wa nyumba zenye bomba na population ya watu, saizi kumekuwa na shida ya maji kiasi cha kina mama kuamka saa nane usiku kusubiria maji ambayo pia huwa yanakuja kwa msimu.

Lakini uongozi wa wilaya ni mwaka wa nne sasa hakuna juhudi zozote zinazofanywa ili kuongeza tank lingine la maji ili yaweze kutosha kwa watu wote badala ya kutegemea tank lililopo tangu miaka ya sabini.

Ni aibu kwa wilaya yenye maji mengi kiasi kile na vyanzo vingi vya maji kuanza kuvizia maji ya mvua au kufikiria kuchimba visima.

Maajabu sisi wa Dar hiyo shida ya maji kwa baadhi ya sehemu ishaanza kuwa historia lakini nilikaa pale tukuyu kwa zaidi ya wiki tatu niliona hayo mateso wanayopitia wamama wale na baridi kali ya Tukuyu mtu unaamka asubuhi kwa ajili ya maji.
 
Uandishi wako hadi unakera,haujaweka aya bali umerundika maneno.
Anyway, kila mtu apambane na hali yake, na wakati anapambana asitikise hali ya mwenzie.
 
Back
Top Bottom