Wilaya mpya ya Wanging'ombe watishia kuhamia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wilaya mpya ya Wanging'ombe watishia kuhamia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mngendalyasota, Jun 25, 2012.

 1. M

  Mngendalyasota Senior Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF
  Wananchi wa wilaya mpya ya Wanging'ombe wametishia kuhamia CHADEMA kutokana na msimamo wa mkuu wa wilaya hiyo Estelina Kilasi kutaka ujenzi wa ofisi za wilaya uwe Mdandu na siyo Igwachanya kama ilivyotangazwa na Rais na ambapo ndiyo makao makuu ya wilaya hiyo.

  Hayo yamesemwa jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana Igwachanya (makao makuu ya wilaya) mbele ya Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya NJOMBE.

  Pia wamemlaumu sana mbunge wao Gerson Lwenge kwa kutowasaidia ktk sakata hilo. Hoja ya Mkuu wa wilaya kuhamisha ujenzi wa ofisi za wilaya ni kwamba anasema Igwachanya hapana ofisi za kutosha za wafanyakazi wa wilaya za kuanzia kazi kwa sasa.
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Waliopendekeza kwamba makao makuu ya wilaya ya Wanging'ombe yawe Igwachanya hawakureason vya kutosha.

  Maana waliangalia ukatikati tu, bila kujali historia ya Njombe kwa ujumla. Walisahau kwamba Mdandu ndiyo yalikuwa makao makuu ya wilaya yote ya ya Njombe hapo awali, kwanini msipaendeleze hapo?

  Mimi pia nayaunga mkono maamuzi ya mkuu wa wilaya, kwa kuwa ofisi za wilaya si za CCM bali ni za wananchi wote wakiwemo hao chadema na vyama vingine.

  So wakihamia chadema au wabaki CCM bado zitabaki ni ofsis zao tu. Mkuu wa wilaya atekeleze wajibu wake kutokana na vigezo alivyoviona. Bahati kubwa mliyonayo wana Wang'ombe ni kwamba huyo Estelina ni ndugu yenu, mtoto wenu wa kumzaa, kwa hiyo maamuzi anayoyafanya bila shaka ni kwa manufaa ya wana wangin'ombe na si vinginevyo.
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Naomba Mungu Mkuu wa Wilaya Akomae
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanging'ombe!
  Igwachanya!
  Mdandu!
   
 5. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,228
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Hao si watu wema maana kama hayo makao makuu yakiwekwa kwao basi hawaihitaji CDM. Hatutaki watu wanaotumia CMD kama silaha ya kujipatia matakwa binafsi. Tunataka watu wanaoipenda chadema kwa dhati bila masharti.

  Watu wa aina hiyo ndio hao CCM ikienda kwa eneo lao wakadanganyishiliwa kofia haraka sana wanarudisha kadi za CDM wanavuta za CCM. Upuuzi huo hatuutaki.

  Kama kweli wanaitaka CMD waje bila kujali makao makuu wa wilaya yatakuwa wapi.
   
 6. N

  Ndole JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kweli Mkuu. Hao wabaki huko huko......
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kwani wapi ni kati kati patakapo wafanya wananchi wafike mapema kutatuliwa matatizo yao?
   
 8. g

  greenstar JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu wa wilaya anatakiwa atumie busara zaidi katika maamuzi yaake kama mtendaji wa serikali,hao wafanyakazi wanaweza kukaa mdandu kwa muda wakati makazi yao yakishughulikiwa kwa kasi zaidi bila kuharibu jitihadi zilizofanyika kuweka makao makuu yawe Igwachanya.Kwa hili mbunge yupo pamoja na nyinyi bila kujali itikadi za chama,madiwani msiwe vigeugeu kufanya maamuzi kwenye vikao vya baraza la madiwani.Ishu ni kuharakisha ujenzi wa nyumba za watumishi kwa kasi zaidi.
  Mh.Lwenge unatakiwa ushirikiane na madiwani wako kuharakisha ujenzi wa nyumba za watumishi kwa nguvu zote bila kujali ugumu ktk utekelezaji !
   
 9. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hizi ndio siasa uchwara... sasa ccm na cdm na makao makuu ya wilaya vinahusiana vipi??? Zizingatiwe sababu za kijiografia na mengineyo muhimu na si ushabiki wa kisiasa
   
 10. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Wamehamia cdm mda mrefu!hawatishii walishafanya maamuzi,Tanganyika nzima wapo huko kasoro wazaramu na wakwere ambao wapo kwenye ukungu na tongo tongo usoni.
   
 11. a

  ambwene_ambwene Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli nia ipo makao makuu ya wilaya hayana impact, ina maanisha wakikubali mtarudi tena ccm kama mkihama usiingie mahali kwa masharti huo sio upenzi wa kweli. Acheni bendera fuata upepo wabena ndio maana hamendelei.

   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Wananchi wanahamia chadema au wanachama wa chama kingine ndo wanahamia chadema?

  Vyovyote vile, Karibuni kwenye harakati za ukombozi wa kweli wa tanzania tuitakayo!
   
 13. Fyengeresya

  Fyengeresya JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Kwa maelezo hayo, basi yawezekana kufikia mabadiliko ya kweli kazi ipo, kuna haja kwa wananchi kufafanuliwa kuhusu mambo ya chama na mambo ya Serikali.

  Mambo ya NyiNyieMu unaweza kufanya kama wanavyofanya wananchi lakini mambo ya Serikali kuna taratibu zake. Hata hivyo nae huyu Kilas kama kweli Rais alitangaza makao makuu kwa nini anabadilisha wakati yeye ni mtu mdogo.

  Kama kilichoandikwa ndo kilivyo na kauli hii ya huyu DC itatekelezwa basi Job Ndugai atakuwa hana ni DHAIFU kwa kumtoa nje kijana Mnyika kwamba Rais Kikwete ni DHAIFU maana hata mtu aliyemteua anatenda kivyake tofauti na maagizo yake.

  Mimi nitajenga imani kwa huyu kijana.
   
 14. m

  mamajack JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  siku hizi kama mabo hayendi mtaani kwako,tishieni kuhamia chadema tu,huduma zitarekebishwa faster!!!!!
  magamba bwana,wamekwisha.
   
 15. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mgendalyasota acha kutuposha na hii habari yako, kwanza usiseme wananchi wa wilaya ya Wanging'ombe wametishia kujiunga na CHADEMA, kwa kweli wananchi wengi wa wilaya hiyo ni wanachama wa CHADEMA hata kabla ya uamzi wa serikali kupeleka wilaya Wanging'ombe. Pili, mkuu wa wilaya hajaamua kujenga ofisi za wilaya huko Mdandu, Kilichopo ni kwamba kwa kuwa Mdandu kuna majengo ya ofisi tayari, basi kwa muda ofisi za wilaya ziwepo hapo Mdandu badala ya kuifunga shule ya msingi Igwachanya ambayo majengo yake yangetumika kama ofisi na kuleta usumbufu kwa walimu na wanafunzi kwa sababu za kisiasa.
   
 16. I

  Igwachnya Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hii nayo sio kweli. Kutumia majengo ya shule ya msingi sio tatizo kwa sababu Igwachanya tayari kuna ofisi nyingine kama zile za kata na hata shule ya msingi haikupaswa kufungwa bali kuhamishiwa sehemu ambapo tayari imeshajengwa ikisubiria finishing ndogo ndogo tu. Mi sidhani kama ni sahihi kuhamisha hamisha makao makuu ya wilaya eti yaanzie Mdandu Then Igwachanya. Kwanza ni matumizi mabaya ya rasilimali siku wakihamia Igwachanya si watataka kulipwa tena?

  Ingawa kuhusisha wazo la Makao makuu na kuhamia chadema kunafanana na ujinga binafsi naunga mkono uwepo wa makao makuu ya wilaya Igwachanya badala ya Mdandu.
   
 17. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kwanza sioni wapi mie nilipo danganya, Mdandu tayari kulikuwa na majengo ambayo yalikuwa yanakaa bure yakiwa na facilities zote ikiwemo umeme na maji, sasa hizo ofisi za kata pale Igwachanya zingechuliwa na mkuu wa wilaya hao watumishi wa kata wangekwenda wapi? shule mpya ka ulivyosema mwenyewe ilikuwa katika hatua za mwisho za ukamilishaji, sawa lakini majengo ya zamani yalihitaji ukarabati mkubwa kabla ya kuanza kutumika, sasa wakati wa ukarabati mkuu huyo angefanyia wapi kazi zake? Ndugu yangu, tukubaliane tu kuwa wananchi wetu hawakuhitaji wilaya mpya bali huduma bora za afya, elimu na kukuza kilimo chao. Kwangu mimi sioni umhimu wa wapi makao makuu yawe wapi, wanaweza kupeleka Chalove, Mtapa, Dindilimunyo, Usuka, Dulamu, Imalinyi au kokote! lakini je wabena wale wanahitaji mkuu wa wilaya?
   
 18. w

  winona New Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  big up mkuu wa wilaya wakoloni hawakukosea kuweka makao makuu ya wilaya enzi hizo mdandu kwenye asili ya neno Njombe.
   
 19. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Wasitishie, watende tu!!!!
   
 20. L

  Lihove JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kilasi ametekeleza ile kauli ya Akili za kumbiwa changanya na za kwako= MBAYUWAYU.
   
Loading...