ikhlas
JF-Expert Member
- Jun 25, 2015
- 1,038
- 1,278
Masilahi ya Taifa..kwann unakimbilia kuamini kwamba gazeti la citizen wanamsafisha Lowasa?kwani Lowasa amechafuka? Chombo ambacho kina mamlaka ya kusema Lowasa ni mchafu ni mahakama peke yake,je mahakama ilishawahi kutangaza?Gazeti la citizen wanajaribu kuwafumbua wananchi macho yao yaliofumbwa mda mrefu na wapinzani wa lowasa kua yeye ni fisadi.Gazeti "halimsafishi" lowasa bali lina "clear misunderstanding" kuhusu yeye.Watu wameaminishwa uongo huu mda mrefu lakini umefika mda sasa wa maji kujitenga na mafuta.Kwa bahati nzuri wasio mtakia mema Lowasa waliijua njia ya Lowasa anayotaka kupita,lowasa alionyesha dhamira ya kupambana na umasikini tokea"1995" hili wabaya wake hawakulipenda hata kidogo ndo mana wana muandama.Kwangu naamini wanaomchafua lowasa "2015" ndio hao hao walio anza kumchafua"1995".Hivyo naiomba kambi ya lowasa ijue kua Mkuu wao ana damu ya KUNGUNI hata akiwa Raisi baada ya uchaguzi wa mwaka huu haya yataendelea kumtokea.Kama lowasa hajui mwambieni kua yeye kusemwa na kutukanwa kwake ni "fate" au destine" yake,hayo ndo majaaliwa yake,kuchafuliwa ndio hatima yake,lakini asilan abadani hatima hii au majaaliwa haya hayatamzuia kuingia IKULU 2015, wapiga firimbi wanabadilisha wimbo tu,1995 walimwambia amejilimbikizia mali lakini hawasemi ameziibia wapi,baadae tena wakaja na hoja eti amefuja mradi wa" kituo cha mikutano cha kimataifa Arusha" walipo ona wimbo huo hauchezeke na watu wa kizazi cha dot com,wakaja na Richmond,ndo mana akaamua ajiuzulu kuonyesha kua yeye kwake "cheo sio ishu" na wala hatumii cheo kupata mali kama mnavyo taka sisi tuamini.Lowasa anadhamira ya dhati ya kufanya jambo flani kwa taifa,hata kama ataiba kama mnavyo sema,lakini nina imani kabisa kuna jambo zuri atatufanyia watanzania.Lowasa wamemchafua lakini sisi wapiga kura hatukumchafua,ndo maana tuna mlaki kwa maelfu na tunamdhamini kwa wingi sana.Tena wapiga kura wengi wala hawasomi mnacho andika kwani "wabongo"hatupendi kusoma vilivyo andikwa,sisi tuna penda kusikiliza,na masikio yetu tumempa Lowasa,
Wahenga wanasema"mchawi mpe mtoto alee" SISI na sio NYINYI tumeamua kumpa lowasa hii nchi kwa miaka 10 ijayo.ATATUVUSHA NDANI YA SAFARI YA MATUMAINI.
Nitukane kama utajiskia hivyo au nidharau kama utapenda.,
Wahenga wanasema"mchawi mpe mtoto alee" SISI na sio NYINYI tumeamua kumpa lowasa hii nchi kwa miaka 10 ijayo.ATATUVUSHA NDANI YA SAFARI YA MATUMAINI.
Nitukane kama utajiskia hivyo au nidharau kama utapenda.,