Wikileaks: Aliyemhoji Hoseah ni jasusi aliyebobea

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Aliyemhoji Hoseah ni jasusi aliyebobea

Mwandishi Wetu

WAKATI wananchi wakimkosoa mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah kupinga taarifa ya Wikileaks iliyovujisha mazungumzo yake na ofisa wa ubalozi wa Marekani, imebainika kuwa Mmarekani huyo amepikwa "kijasusi" katika masuala ya usalama wa taifa, uhusiano wa kimataifa, jeshi na ni ofisa mwandamizi.

Ofisa huyo, D. Purnell Delly alipeleka taarifa ya mazungumzo nchini Marekani akiripoti kuwa DK Hoseah amemwambia kuwa Rais Jakaya Kikwete hayuko tayari kuachia sheria ichukue mkondo wake katika kuwashtaki vigogo wanaojihusisha na rushwa.

Dk Hoseah, ambaye kwenye taarifa hiyo anadai kutishiwa maisha kiasi cha kufikiria kuikimbia nchi, amekiri kuongea na ofisa huyo lakini akadai kuwa ofisa huyo alimkariri tofauti na alivyosema.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dk Hoseah amefafanua kuwa alichokisema ni kwamba Rais Kikwete hayuko tayari kuidhinisha vigogo wanaojihusisha na rushwa kufikishwa mahakamani bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yao.

Ubalozi wa Marekani umekataa kuzungumzia taarifa hizo za mawasiliano zilizovujishwa na mtandao wa Wikileaks ukisema kuwa hauna maelezo yoyote, kwa mujibu wa mkurugenzi wa kitengo cha mahusiano ya jamii cha ubalozi huo, Ilya D. Levin.

Ikulu ya Dar es salaam nayo haikutaka kuzungumzia suala hilo baada ya Mwananchi kuwasiliana na mwandishi wake, Premmy Kibanga.

Lakini Mwananchi imebaini kuwa ofisa huyo ni mzoefu katika kazi na amepitia mafunzo mbalimbali kiasi cha kumfanya aaminiwe na taifa hilo kubwa kufanya kazi hiyo inayofanana na ya kijasusi kwenye nchi tofauti, baadhi zikiwa ni zile zenye matatizo ya amani.

Taarifa ya Delly kwenda Ikulu ya Marekani ilivujishwa na mtandao wa wikileaks ambao umepata umaarufu mkubwa kwa kutoa siri za serikali mbalimbali duniani.

D. Delly alikuwa mkuu wa ujumbe wa wanadiplomasia wa Marekani kwenye Ofisi za ubalozi jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 9, mwaka 2005.

Kabla ya kuja Dar es Salaam kufanya kazi hiyo ya diplomasia, alikuwa msaidizi maalumu wa katibu msaidizi wa masuala ya Afrika kwenye Idara ya Serikali ya Marekani jijini Washington. Alipata nafasi hiyo baada ya kutumikia cheo cha naibu mkuu wa ujumbe wa Marekani jijini Khartoum, Sudan.

Delly alijiunga na idara hiyo mwaka 1983. Awali alikuwa mshauri wa mambo ya siasa na uchumi wa Copenhagen; naibu mshauri wa masuala ya Uchumi jijini Ankara, Uturuki na ofisa katika dawati maalumu nchini Sri Lanka.

Pia alifanya kazi hizo katika miji ya Edinburgh na El Salvador wakati wa vita na akajizolea heshima kubwa na hivyo kutunukiwa tuzo ya ujasiri na utumishi uliotukuka.

Dk Hoseah alieleza kuwa alikaririwa vibaya na ofisa huyo, lakini taarifa zinaonyesha kuwa Delly, ambaye anatokea Jimbo la Virginia, ni mtaalamu wa lugha akiwa amepata shahada yake ya kwanza katika Fasihi ya Lugha ya Kirusi kwenye Chuo Kikuu cha Dartmouth na shahada ya uzamili ya fasihi katika Chuo Kikuu cha Chicago.

Pia Mmarekani huyo alisomea Sheria za Kimataifa kwenye Chuo cha William na Mary, na shahada ya Uzamili ya Usalama wa Kimataifa na Uandaaji wa Mikakati ya Kijeshi katika chuo cha Newport, Rhode Island ambako wanafundishwa askari wa majini.

Chuo cha US Naval alichosomea Delly, ambaye alikuwa mwanachama na mwalimu wa vikosi vya ulinzi vya mwambao wa Marekani, kina kazi ya kuzalisha viongozi wa kuandaa Mikakati ya kijeshi na namna ya kuitekeleza.

Chuo hicho hutoa programu za fani za kijeshi zinazokwenda na wakati, usahihi, mahususi na zinazotekelezeka kwa idadi kubwa ya maofisa wa kijeshi wa Marekani, askari waajiriwa wa majini, waajiriwa raia ndani ya serikali ya Marekani na hata katika taasisi zisizo za kiserikali (NGOs), pamoja na maofisa wa kimataifa.

Chuo hicho hutarajia kupata kundi la viongozi wenye sifa ya uaminifu na kujiamini katika kila jukumu lao na wenye akili za kiutendaji na kimkakati, wenye tafakuri tunduwizi, uwezo mkubwa katika kuunganisha mambo na wapiganaji katika vita.

Mtaala wa chuo umegawika katika kozi kuu tatu za masomo; mikakati na sera, usalama wa taifa katika kufanya maamuzi na namna ya kuunganisha operesheni za kijeshi.

Kozi ya Mikakati na Sera imewekwa kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi kufikiria kulingana na mikakati kuhusu nadharia za kijeshi kuanzia mwanzo wa vita katika bahari kati ya Athens na Sparta hadi sasa. Lengo ni kuweka uhusiano kati ya Malengo ya Taifa kisiasa na namna ambayo mbinu zake za jeshi zinakuwa mahususi kutumika ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa (Ushindi).

Kozi ya pili ya Usalama wa Taifa katika Maamuzi imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watendaji wakuu katika jeshi na wananchi kukabiliana na hoja za kisiasa, kiuchumi, na kijeshi katika kufanya maamuzi sahihi kwenye masuala ya Usalama wa Taifa.

Kozi ya tatu ya kuunganisha operesheni za kijeshi inawasaidia wakuu wa taasisi za kijeshi kutafsiri mikakati ya kijeshi na hasa ya kikanda katika vita vya majini.

Karibu nusu ya wanafunzi wanaotoka Marekani ni maofisa kutoka jeshi, vikosi vya anga, majini, ulinzi wa mwambao na katika meli na kampuni na wakala wa ulinzi binafsi.

Uzoefu huo wa kazi na elimu kubwa ya ofisa huyo wa Marekani ulimfanya mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba kutokuwa na wasiwasi na ripoti ya Delly kwenda Ikulu ya Marekani.

“Delly hana sababu ya kumzulia Hoseah. Ni mzoefu na anajiamini katika kazi zake; haya ya kusema kwamba nimenukuliwa vibaya, ni ujanja ujanja wa kulindana tu,” alisema Profesa Lipumba ambaye alisomea shahada yake ya uzamili, akijikita katika uchumi kwenye Chuo Kikuu cha nchini Marekani.

“Yale yaliyoandikwa katika mtandao wa Wikileaks na baadaye kuchapishwa katika gazeti la The Guardian la Uingereza ni ya kweli ya Dk Hoseah na yale ya kukanusha ni ya kulindana.”

Prof Lipumba alidai kuwa ni kweli Rais Kikwete hayuko tayari hata siku moja kuona rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa au waziri mkuu wake, Frederick Sumaye wakisimamishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi.

Alisema mambo hayo yanafanana kabisa na yaliyoandikwa katika gazeti hilo mwaka 2007 kwamba Hoseah anatembea na mlinzi mwenye silaha kutokana na kuhofia usalama wake.

“Jambo la msingi ambalo tunaliona hapa ni kwamba tuna udhaifu mkubwa katika uongozi na viongozi hawana utashi na ujasiri wa kupambana na rushwa... Hoseah na hata Kikwete hawawezi kupambana,” alisemai.

“Fedha ile (dola 12.4 milioni alizolipwa Shailesh Vithlani katika ununuzi wa rada) haina mjadala kuwa ni rushwa, ni rushwa ambayo alilipwa Vithlani kifisadi kufanikisha zabuni ya uuzaji wa rada kwa serikali ya Tanzania.”

Wakili wa siku nyingi nchini, Profesa Abdallah Safari alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa taarifa iliyotolewa na mtandao huo ni ukweli.

"Kuamini utetezi wa Dk Hoseah ni vigumu kutokana na mwenendo wake," alisema Profesa Safari. "Alijaribu kumsafisha (mwanasheria na mbunge wa Bariadi Magharibi) Andrew Chenge katika kashfa ya rada.
“Amekuwa akitofautiana na ripoti mbalimbali mpaka za bunge kama ile ya Richmond. Kwa hiyo CCM ni watu wasioaminika na serikali yao... wana mambo yao bwana.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alitazama suala hilo katika sura tatu, akielezea sura ya kwqanza kuwa ni nchi za Kiafrika kuanzisha taasisi zisizo huru na zinazoendeshwa kwa kutegemea msaada wa wahisani, akitoa mfano wa Takukuru.

“Hata ukisoma hiyo taarifa kwa umakini kwenye mtandao, utona kabisa kuwa Dk Hoseah alikuwa anajipendekeza kwa ajili ya kulinda ufadhili,” alisema Bashiru.

Alisema endapo Takukuru ingekuwa ni taasisi huru na inayojitegemea kwa kila kitu, basi kusingekuwa na sababu ya mkurugenzi wake kuzungumza na Wamarekani.

Katika mtazamo wake wa pili, Bashiru alisema wasomi, wanahabari na wanasiasa wana kazi kubwa ya kuangalia lengo la mtandao huo kufichua habari kama hizo zinzolihusu bara la Afrika na Asia.

“Lazima tujiulize kwa nini hizi siri zinafichuliwa wakati huu/ kwa nini Marekani na nchi kama Uganda, Iraq na Tanzania; kwa nini hakuna siri za Marekani na nchi nyingine tajiri kusema ni jinsi gani wanavyopanga kutugandamiza,” alisema Bashiru.

Kwa sura ya tatu, Bashiru alisema inakuwa vigumu kwa sasa kuangalia hatima ya mapambano ya rushwa, akisema ni lazima mtu ajitoe mhanga katika vita ya rushwa na kwamba kama hakuna dhamira ya kweli, huwezi kupambana.

“Dk Hoseah amekanusha baadhi ya mambo kwa hiyo labda tusubiri wamarekani wenyewe watuambie kama wamemlisha maneno, lakini kweli kwenye mapambano ya rushwa lazima mambo ya kutishiana maisha yawepo kwa sababu yanahusu watu wazito,” alisema Bashiru.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kukuza demokrasia nchini Agenda Participation 2000, Moses Kulaba alisema mtandao huo umefungua macho ya Watanzania.

Alisema siri zilizofichuliwa zimekuwa uthibitisho wa masuala ambayo Watanzania walikuwa wakiyawaza kwa muda mrefu.

“Mimi mwenyewe nimeusoma ule mtandao, bado kuna mengi ni mapema mno kwa Dk Hoseah kuanza kukanusha,” alisema Kulaba.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Uchumi, Adolf Mkenda alimtaka Dk Hoseah ajiuzulu iwapo ni kweli alimuelezea Rais Kikwete kuwa hapendi vita dhidi ya rushwa.

Mkenda alisema kitendo cha Dk Hoseah kueleza mambo ya ndani kwa maofisa wa ubalozi wa Marekani wakati anajua yeye anawajibika kwa serikali ni ukiukwaji wa maadili ya kazi yake na hivyo anapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu.

“Ni jambo la ajabu sana kwa Dk Hoseah kufanya kitendo hicho, kama taarifa hizi ni za kweli inabidi ajiuzulu mwenyewe kwani hafai kuendelea kuiongoza Takukuru” alisema Mkenda na kuongeza kuwa iwapo atajiwajibisha, serikali haina budi kumchukulia hatua.

Mkenda pia alieleza kuwa kama Rais Kikwete hapendi sheria ichukue mkondo wake katika vita dhidi ya rushwa, amekiuka katiba.

Chanzo: Mwananchi

My take:

Huyu jamaa vipi? Yaani pamoja na elimu yake yote hadi ya u-PHD bado hajui kama maafisa wengi katika balozi za Marekani duniani kote ni majasusi wa CIA? Yaani hakuhisi kabisa afisa huyo huenda alikuwa jasusi wa CIA -- na badala yake yakaanza kumtoka maneno kama vile hana akili nzuri?

Nashangaa kwa nini hadi sasa Hosea hajajiuzulu -- kwani si mtunza siri kabisa! Ni mtu hatari hasa kwa ma-wihstleblowers -- wale wanaopeleka taarifa za ufisadi kwake -- kwani anaweza kabisa kudisclose identities zao kwa watuhumiwa -- na hivyo kuwahatarisha maisha yao. Kuna watu tayari pengine wameshakufa.

JK, kama unaipenda nchi hii fukuza hii mutu. Sijui ameshatoa siri ngapi za mazungumzo yenu. Huyu mutu Pambaff kabisa!
 
Aliyemhoji Hoseah ni jasusi aliyebobea

Mwandishi Wetu

WAKATI wananchi wakimkosoa mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah kupinga taarifa ya Wikileaks iliyovujisha mazungumzo yake na ofisa wa ubalozi wa Marekani, imebainika kuwa Mmarekani huyo amepikwa "kijasusi" katika masuala ya usalama wa taifa, uhusiano wa kimataifa, jeshi na ni ofisa mwandamizi.

Ofisa huyo, D. Purnell Delly alipeleka taarifa ya mazungumzo nchini Marekani akiripoti kuwa DK Hoseah amemwambia kuwa Rais Jakaya Kikwete hayuko tayari kuachia sheria ichukue mkondo wake katika kuwashtaki vigogo wanaojihusisha na rushwa.

Dk Hoseah, ambaye kwenye taarifa hiyo anadai kutishiwa maisha kiasi cha kufikiria kuikimbia nchi, amekiri kuongea na ofisa huyo lakini akadai kuwa ofisa huyo alimkariri tofauti na alivyosema.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dk Hoseah amefafanua kuwa alichokisema ni kwamba Rais Kikwete hayuko tayari kuidhinisha vigogo wanaojihusisha na rushwa kufikishwa mahakamani bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yao.

Ubalozi wa Marekani umekataa kuzungumzia taarifa hizo za mawasiliano zilizovujishwa na mtandao wa Wikileaks ukisema kuwa hauna maelezo yoyote, kwa mujibu wa mkurugenzi wa kitengo cha mahusiano ya jamii cha ubalozi huo, Ilya D. Levin.

Ikulu ya Dar es salaam nayo haikutaka kuzungumzia suala hilo baada ya Mwananchi kuwasiliana na mwandishi wake, Premmy Kibanga.

Lakini Mwananchi imebaini kuwa ofisa huyo ni mzoefu katika kazi na amepitia mafunzo mbalimbali kiasi cha kumfanya aaminiwe na taifa hilo kubwa kufanya kazi hiyo inayofanana na ya kijasusi kwenye nchi tofauti, baadhi zikiwa ni zile zenye matatizo ya amani.

Taarifa ya Delly kwenda Ikulu ya Marekani ilivujishwa na mtandao wa wikileaks ambao umepata umaarufu mkubwa kwa kutoa siri za serikali mbalimbali duniani.

D. Delly alikuwa mkuu wa ujumbe wa wanadiplomasia wa Marekani kwenye Ofisi za ubalozi jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 9, mwaka 2005.

Kabla ya kuja Dar es Salaam kufanya kazi hiyo ya diplomasia, alikuwa msaidizi maalumu wa katibu msaidizi wa masuala ya Afrika kwenye Idara ya Serikali ya Marekani jijini Washington. Alipata nafasi hiyo baada ya kutumikia cheo cha naibu mkuu wa ujumbe wa Marekani jijini Khartoum, Sudan.

Delly alijiunga na idara hiyo mwaka 1983. Awali alikuwa mshauri wa mambo ya siasa na uchumi wa Copenhagen; naibu mshauri wa masuala ya Uchumi jijini Ankara, Uturuki na ofisa katika dawati maalumu nchini Sri Lanka.

Pia alifanya kazi hizo katika miji ya Edinburgh na El Salvador wakati wa vita na akajizolea heshima kubwa na hivyo kutunukiwa tuzo ya ujasiri na utumishi uliotukuka.

Dk Hoseah alieleza kuwa alikaririwa vibaya na ofisa huyo, lakini taarifa zinaonyesha kuwa Delly, ambaye anatokea Jimbo la Virginia, ni mtaalamu wa lugha akiwa amepata shahada yake ya kwanza katika Fasihi ya Lugha ya Kirusi kwenye Chuo Kikuu cha Dartmouth na shahada ya uzamili ya fasihi katika Chuo Kikuu cha Chicago.

Pia Mmarekani huyo alisomea Sheria za Kimataifa kwenye Chuo cha William na Mary, na shahada ya Uzamili ya Usalama wa Kimataifa na Uandaaji wa Mikakati ya Kijeshi katika chuo cha Newport, Rhode Island ambako wanafundishwa askari wa majini.

Chuo cha US Naval alichosomea Delly, ambaye alikuwa mwanachama na mwalimu wa vikosi vya ulinzi vya mwambao wa Marekani, kina kazi ya kuzalisha viongozi wa kuandaa Mikakati ya kijeshi na namna ya kuitekeleza.

Chuo hicho hutoa programu za fani za kijeshi zinazokwenda na wakati, usahihi, mahususi na zinazotekelezeka kwa idadi kubwa ya maofisa wa kijeshi wa Marekani, askari waajiriwa wa majini, waajiriwa raia ndani ya serikali ya Marekani na hata katika taasisi zisizo za kiserikali (NGOs), pamoja na maofisa wa kimataifa.

Chuo hicho hutarajia kupata kundi la viongozi wenye sifa ya uaminifu na kujiamini katika kila jukumu lao na wenye akili za kiutendaji na kimkakati, wenye tafakuri tunduwizi, uwezo mkubwa katika kuunganisha mambo na wapiganaji katika vita.

Mtaala wa chuo umegawika katika kozi kuu tatu za masomo; mikakati na sera, usalama wa taifa katika kufanya maamuzi na namna ya kuunganisha operesheni za kijeshi.

Kozi ya Mikakati na Sera imewekwa kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi kufikiria kulingana na mikakati kuhusu nadharia za kijeshi kuanzia mwanzo wa vita katika bahari kati ya Athens na Sparta hadi sasa. Lengo ni kuweka uhusiano kati ya Malengo ya Taifa kisiasa na namna ambayo mbinu zake za jeshi zinakuwa mahususi kutumika ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa (Ushindi).

Kozi ya pili ya Usalama wa Taifa katika Maamuzi imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watendaji wakuu katika jeshi na wananchi kukabiliana na hoja za kisiasa, kiuchumi, na kijeshi katika kufanya maamuzi sahihi kwenye masuala ya Usalama wa Taifa.

Kozi ya tatu ya kuunganisha operesheni za kijeshi inawasaidia wakuu wa taasisi za kijeshi kutafsiri mikakati ya kijeshi na hasa ya kikanda katika vita vya majini.

Karibu nusu ya wanafunzi wanaotoka Marekani ni maofisa kutoka jeshi, vikosi vya anga, majini, ulinzi wa mwambao na katika meli na kampuni na wakala wa ulinzi binafsi.

Uzoefu huo wa kazi na elimu kubwa ya ofisa huyo wa Marekani ulimfanya mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba kutokuwa na wasiwasi na ripoti ya Delly kwenda Ikulu ya Marekani.

"Delly hana sababu ya kumzulia Hoseah. Ni mzoefu na anajiamini katika kazi zake; haya ya kusema kwamba nimenukuliwa vibaya, ni ujanja ujanja wa kulindana tu," alisema Profesa Lipumba ambaye alisomea shahada yake ya uzamili, akijikita katika uchumi kwenye Chuo Kikuu cha nchini Marekani.

"Yale yaliyoandikwa katika mtandao wa Wikileaks na baadaye kuchapishwa katika gazeti la The Guardian la Uingereza ni ya kweli ya Dk Hoseah na yale ya kukanusha ni ya kulindana."

Prof Lipumba alidai kuwa ni kweli Rais Kikwete hayuko tayari hata siku moja kuona rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa au waziri mkuu wake, Frederick Sumaye wakisimamishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi.

Alisema mambo hayo yanafanana kabisa na yaliyoandikwa katika gazeti hilo mwaka 2007 kwamba Hoseah anatembea na mlinzi mwenye silaha kutokana na kuhofia usalama wake.

"Jambo la msingi ambalo tunaliona hapa ni kwamba tuna udhaifu mkubwa katika uongozi na viongozi hawana utashi na ujasiri wa kupambana na rushwa... Hoseah na hata Kikwete hawawezi kupambana," alisemai.

"Fedha ile (dola 12.4 milioni alizolipwa Shailesh Vithlani katika ununuzi wa rada) haina mjadala kuwa ni rushwa, ni rushwa ambayo alilipwa Vithlani kifisadi kufanikisha zabuni ya uuzaji wa rada kwa serikali ya Tanzania."

Wakili wa siku nyingi nchini, Profesa Abdallah Safari alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa taarifa iliyotolewa na mtandao huo ni ukweli.

"Kuamini utetezi wa Dk Hoseah ni vigumu kutokana na mwenendo wake," alisema Profesa Safari. "Alijaribu kumsafisha (mwanasheria na mbunge wa Bariadi Magharibi) Andrew Chenge katika kashfa ya rada.
"Amekuwa akitofautiana na ripoti mbalimbali mpaka za bunge kama ile ya Richmond. Kwa hiyo CCM ni watu wasioaminika na serikali yao... wana mambo yao bwana."

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alitazama suala hilo katika sura tatu, akielezea sura ya kwqanza kuwa ni nchi za Kiafrika kuanzisha taasisi zisizo huru na zinazoendeshwa kwa kutegemea msaada wa wahisani, akitoa mfano wa Takukuru.

"Hata ukisoma hiyo taarifa kwa umakini kwenye mtandao, utona kabisa kuwa Dk Hoseah alikuwa anajipendekeza kwa ajili ya kulinda ufadhili," alisema Bashiru.

Alisema endapo Takukuru ingekuwa ni taasisi huru na inayojitegemea kwa kila kitu, basi kusingekuwa na sababu ya mkurugenzi wake kuzungumza na Wamarekani.

Katika mtazamo wake wa pili, Bashiru alisema wasomi, wanahabari na wanasiasa wana kazi kubwa ya kuangalia lengo la mtandao huo kufichua habari kama hizo zinzolihusu bara la Afrika na Asia.

"Lazima tujiulize kwa nini hizi siri zinafichuliwa wakati huu/ kwa nini Marekani na nchi kama Uganda, Iraq na Tanzania; kwa nini hakuna siri za Marekani na nchi nyingine tajiri kusema ni jinsi gani wanavyopanga kutugandamiza," alisema Bashiru.

Kwa sura ya tatu, Bashiru alisema inakuwa vigumu kwa sasa kuangalia hatima ya mapambano ya rushwa, akisema ni lazima mtu ajitoe mhanga katika vita ya rushwa na kwamba kama hakuna dhamira ya kweli, huwezi kupambana.

"Dk Hoseah amekanusha baadhi ya mambo kwa hiyo labda tusubiri wamarekani wenyewe watuambie kama wamemlisha maneno, lakini kweli kwenye mapambano ya rushwa lazima mambo ya kutishiana maisha yawepo kwa sababu yanahusu watu wazito," alisema Bashiru.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kukuza demokrasia nchini Agenda Participation 2000, Moses Kulaba alisema mtandao huo umefungua macho ya Watanzania.

Alisema siri zilizofichuliwa zimekuwa uthibitisho wa masuala ambayo Watanzania walikuwa wakiyawaza kwa muda mrefu.

"Mimi mwenyewe nimeusoma ule mtandao, bado kuna mengi ni mapema mno kwa Dk Hoseah kuanza kukanusha," alisema Kulaba.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Uchumi, Adolf Mkenda alimtaka Dk Hoseah ajiuzulu iwapo ni kweli alimuelezea Rais Kikwete kuwa hapendi vita dhidi ya rushwa.

Mkenda alisema kitendo cha Dk Hoseah kueleza mambo ya ndani kwa maofisa wa ubalozi wa Marekani wakati anajua yeye anawajibika kwa serikali ni ukiukwaji wa maadili ya kazi yake na hivyo anapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu.

"Ni jambo la ajabu sana kwa Dk Hoseah kufanya kitendo hicho, kama taarifa hizi ni za kweli inabidi ajiuzulu mwenyewe kwani hafai kuendelea kuiongoza Takukuru" alisema Mkenda na kuongeza kuwa iwapo atajiwajibisha, serikali haina budi kumchukulia hatua.

Mkenda pia alieleza kuwa kama Rais Kikwete hapendi sheria ichukue mkondo wake katika vita dhidi ya rushwa, amekiuka katiba.

Chanzo: Mwananchi

My take:

Huyu jamaa vipi? Yaani pamoja na elimu yake yote hadi ya u-PHD bado hajui kama maafisa wengi katika balozi za Marekani duniani kote ni majasusi wa CIA? Yaani hakuhisi kabisa afisa huyo huenda alikuwa jasusi wa CIA -- na badala yake yakaanza kumtoka maneno kama vile hana akili nzuri?

Nashangaa kwa nini hadi sasa Hosea hajajiuzulu -- kwani si mtunza siri kabisa! Ni mtu hatari hasa kwa ma-wihstleblowers -- wale wanaopeleka taarifa za ufisadi kwake -- kwani anaweza kabisa kudisclose identities zao kwa watuhumiwa -- na hivyo kuwahatarisha maisha yao. Kuna watu tayari pengine wameshakufa.

JK, kama unaipenda nchi hii fukuza hii mutu. Sijui ameshatoa siri ngapi za mazungumzo yenu. Huyu mutu Pambaff kabisa!

Penye red:
Wewe unafikiri tuna rais? Yupoyupo tu kwa nguvu za Wahindi wawili watatu hivi basi. Hawezi kumfukuza mtu yoyote labda msukumo huo utoke kwa mmoja wao -- kama vile RA.
 
The weak link is the President who has forgotten the presidency is an institution and he remember persoanal friendship at the expense of national issues. He has privatised the presidency
 
Nami nashangaa kwa nini Hoseah anang'ang'ania madaraka -- pamoja na yote negative yanayotokea kuhusu yeye! Lakini yote tisa -- hii ni just too much!
 
Habari za uhakika nilizopata kuhusu huyu mjamaa -- ukishampigisha Grants kama nne hivi, basi ujue unavuna bonge la info kuhusu wala rushwa katika serikali. He's very loose!
 
Nami nashangaa kwa nini Hoseah anang'ang'ania madaraka -- pamoja na yote negative yanayotokea kuhusu yeye! Lakini yote tisa -- hii ni just too much!

Mkuu tatizo si Hosea bali kikwete mwenyewe. Tulipong'ang'ania kuwa Hosea atoke si wote tuliokuwa tunasema hivyo kwa sababu ya issues za richmond tu. Pia na weaknesses binafsi za huyu jamaa. Tumefanya naye kazi na wengine amewafundisha katika baadhi ya vyuo hapa nchini. For sure he doesnt fit that possesion anatakiwa awe chuo tu akifundisha japo hata ufundishaji wake ni kama wa kusoma imla tu.

Kikwete alipaswa kuwaita watu waliokuwa mstari wa mbele kutaka amwondoe Ukurugenzi takukuru, badala yake akawalabel kama wapinzani maadui. Sasa inakula kwake. Siku kikwete akigundua kuwa Hosea ndiye mvujishaji mkuu wa siri na nyaraka za serikali, it will be too late.
 
Sikumbuki ni lini but nilisoma hio habari kwene gazeti la mwananchi jinsi HOSEAH alivyomrubuni mwandishi mmoja ambaye aliandika maovu yake na kwamba Hoseah hakustahili kupewa hio nafasi, huyu mzee wa watu akaishia jela, sasa leo ni yeye, kwanza akamatwa na kufungwa yy anadhani hawajamaa wanaropoka bila evidence, sema tu sasa hatuna Rais makini but huyu hakustahili kuwepo hapo alipo
 
Deputy Chief of Mission

About D. Purnell Delly

dpurnelldelly.jpg
D. Purnell DellyD. Purnell Delly became Deputy Chief of Mission at the U.S. Embassy, Dar es Salaam, on July 9, 2005. Before arriving in Dar es Salaam, he was Special Assistant to the Assistant Secretary for African Affairs at the State Department in Washington. He became Special Assistant after serving as Deputy Chief of Mission in Khartoum, Sudan.

Mr. Delly joined the State Department in 1983. His previous postings include assignments as Counselor for Political and Economic Affairs in Copenhagen, Deputy Economic Counselor in Ankara, and Desk Officer for Sri Lanka. He has also served in Edinburgh, and in El Salvador during the war. He has received Superior and Meritorious Honor awards and the Award for Valor.

A native of Virginia, Mr. Delly received a Bachelor's degree in Literature with minor in Russian language from Dartmouth College, a Master's in Literature from University of Chicago, a J.D. with concentration in international law from William and Mary, and a Master's in National Security and Strategic Studies from the Naval War College in Newport, Rhode Island. He is a member and instructor for the U.S. Coast Guard Auxiliary.

This site is managed by the U.S. Department of State.
External links to other Internet sites should not be construed as an endorsement of the views or privacy policies contained therein.
Home | About Us | American Citizen Services | Visas | Policy News | Resources
Contact Us | Frequently Asked Questions | Privacy | Webmaster
 
Bao la kisigino hilo.. Kalaghabao Hoseah!!
Tena nahisi hawa majasusi kuna mengi wanayoyajua kuhusu nchi yetu zaidi hata ya hili..
Tena kwa kupewa habari na sisi wenyewa...
 
Hii thread ni ya wabaya wa Hoseah na wala si wazalendo wa taifa langu. Amesema hajasema it doesnt matter. What matters we have the weakest president ever
 
Mimi naona wote wawili wanastahili kujiuzulu.
Hosea ajiuzulu kwa kutoa siri na JK ajiuzulu kwa kuwa hayuko tayari kuachia sheria ichukue mkondo wake katika kuwashtaki vigogo wanaojihusisha na rushwa hususani mafisadi. Kwani tangu tuanze kusikikia habari za mafisadi JK ameshatoa tamko gani yeye kama Rais juu ya ufisadi kama ana support au la. Yupo silent. Na siku zote silence means YES - Ana support ufisadi. He has to step down immediately
 
Mkuu tatizo si Hosea bali kikwete mwenyewe. Tulipong'ang'ania kuwa Hosea atoke si wote tuliokuwa tunasema hivyo kwa sababu ya issues za richmond tu. Pia na weaknesses binafsi za huyu jamaa. Tumefanya naye kazi na wengine amewafundisha katika baadhi ya vyuo hapa nchini. For sure he doesnt fit that possesion anatakiwa awe chuo tu akifundisha japo hata ufundishaji wake ni kama wa kusoma imla tu.

Kikwete alipaswa kuwaita watu waliokuwa mstari wa mbele kutaka amwondoe Ukurugenzi takukuru, badala yake akawalabel kama wapinzani maadui. Sasa inakula kwake. Siku kikwete akigundua kuwa Hosea ndiye mvujishaji mkuu wa siri na nyaraka za serikali, it will be too late.

Hapa mnataka nini?? Kama kasema kakosa nini hapo hamueleweki maana kama Kikwete anawalinda Rostam na Lowasa akisema kuna ubaya gani?? siyo siri kuwa Kikwete ndiye aliyenyuma ya Richmond, Dowans na Uchafu wote wa Kifisadi hapa Tanzania! Bravo Hoseah siri chafu kama hiyo ya nini, siri ya kutuibia afiche ya nini kama kasema yupo sahihi kabisa endelea kufichua uozo wote
 
Back
Top Bottom