KERO Wiki ya Maji Kinyerezi kanga hatuna maji

KERO Wiki ya Maji Kinyerezi kanga hatuna maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Doto12

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2023
Posts
759
Reaction score
1,348
Mh Rais ni wiki ya maji lakini kinyerezi hatuna maji.

Tumewalilia watendaji wa ukanda huu bila mafanikio.

Inavyoonekana upande huu unachangamoto na inakinzana nanmamlaka.

Mh Rais hii inavyoonekana hata waziri ameshindwa badala yake amekemea jambo bila kujua tatizo.

Tunapokea maji kutoka kimara, tunasubiri huruma ya kimara wafungur maji ndipo tupate, watendaji wanasingizia msukumo, kila siku wanadai msukumo, yapata mwezi wa nne sasa.

Tusaidie kuondoa adha hii.

Nakala alone
BonnaBMBUNGE
RC
DC
WAZIRI JUMAA
 
Maji ukiyapata huna habari na hutaona kero yake.

Maji yakose bana utatamani kumshangaa kiongozi
 
Mh Rais ni wiki ya maji lakini kinyerezi hatuna maji.

Tumewalilia watendaji wa ukanda huu bila mafanikio.

Inavyoonekana upande huu unachangamoto na inakinzana nanmamlaka.

Mh Rais hii inavyoonekana hata waziri ameshindwa badala yake amekemea jambo bila kujua tatizo.

Tunapokea maji kutoka kimara, tunasubiri huruma ya kimara wafungur maji ndipo tupate, watendaji wanasingizia msukumo, kila siku wanadai msukumo, yapata mwezi wa nne sasa.

Tusaidie kuondoa adha hii.

Nakala alone
BonnaBMBUNGE
RC
DC
WAZIRI JUMAA

Hiv huku Kinyerezi tuna mbuge kweli?mimi mpaka nilishasahau
 
Kinyerezi yote inahujumiwa.

Watu wanasystem zao za Maji, yaan bomba la Dawasa linapita hapa la mtu binafsi linapita pale.. wote wanafanya kazi ya kusupply Maji.

1000lts ambayo sawa sawa na 1 unit mtu binafsi anachaji 4000 Tzs.. wakati Dawasa anachaji chini ya 1700 Tzs.

Hawa watu binafsi wanasambaza maji katika mitaa na nahisi (Sina uhakika) wanahujumu miundombinu ya DAWASA, si hivyo tu.. bali wanahonga wale watendaji au wasimamizi wa kipande hicho maji yasitoke ili wao wauze.

Haiwezekani kwa wiki maji yanatoka mara moja, na yakitoka hayana nguvu.. na vile vile machafu kwasababu mabomba yanakaa muda mrefu bila maji.

JF wapush hii ishu iwafikie wahusika.. kuna hujuma zinaendelea huko. Ni KINYEREZI yote waifatilie na waongee na Wakazi / Wateja wao vzr watafunguka.
 
Mbunge wenu Bonnah anazidi kunawiri.at.your expense. Mpigeni chini
 
Back
Top Bottom