Wife material only Kanda ya ziwa

Abdullah01

Member
Jul 5, 2023
13
36
Habari wapendwa wote hapa jukwaani.

Najitokeza kutafuta mke wa maisha yangu. Natamani kuwa na familia bora yenye upendo na furaha. Familia bora huanza na mama bora, pamoja na majukumu thabiti ya baba kujali na kutunza / kuhudumia familia yake, bado nafasi ya mama bora kujenga umoja na upendo ndani ya familia halikwepeki.

Hivyo natafuta mwanamke mwenye nia ya kweli ya kuwa mke wangu wa maisha na mwenye matamanio ya kuwa mama bora wa familia ili tuishi kwa upendo na furaha katika familia yetu.
Sifa za huyo mwanamke angalau awe na hizi zifuatazo:
1. Mwenye kumcha Mungu/ hofu ya Mungu - awe dini yeyote Ile maana sisi sote ni wa Mungu mmoja kasoro ni madhahebu tu.
2. Awe kutoka kanda ya ziwa - Mwanza, Geita, Mara, Kagera
3. Kabila lolote lile Tanzania
4. Umri kuanzia miaka 25 hadi 35.
5. Akiwa na mtoto awe mmoja tu sio zaidi ya hapo.
6. ELIMU: kuanzia - FORM FOUR + CERTIFICATE HADI CHUO KIKUU
7. Awe tayari kupima HIV endapo tutaafikiana kusonga kwa hatua za posa Kisha ndoa.

SIFA ZANGU.
1. Elimu ya chuo kikuu.
2. Mwajiriwa serikalini
3. Nipo mwanza mjini
4. Nina mtoto mmoja
5. Muislam lakini naweza kuoa mwanamke wa dini yeyote Ile kikubwa ni maelewano na upendo wa kweli.
6. Nipo tayari kupima HIV muda wowote 24/7 (Mimi sio mtu wa mambo mengi)
7. Mwenyeji wa mikoa ya kusini mwa Tanzania.
8. Umri wangu miaka 37.

Nawakaribisha hasa kwa wanawake wenye nia ya dhati na wenye sifa hizo hapo au kama una sifa za ziada itapendeza zaidi ili Mungu atubariki tuweze kujenga familia bora yenye upendo na furaha.

ASANTE, KARIBUNI MWANZA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom