Wife kanibadilikia, msaada pls

Pole kakangu, ndio mambo ya ndoa hayo ila wanawake wengi wakishaingia kwenye ndoa huwa wanajisahau sana.

Ushauri wangu kwako, kwanza usimpe tena hela ya mafuta ya gari, hawezi kuweka mafuta kwenye gari kwa pesa yake apaki gari.

Pili anzisha utaratibu wa ibada pamoja kabla ya kulala kama anamuogpa Mungu lazima atashiriki ibada, kuna masomo mazuri sana kwenye Biblia yanayohusu ndoa, soma kitabu cha Methali, Waefeso, Wakoritho n.k (kama ni Wakristo lakini)na asubuhi kabla hamjatoka fanyeni sala ya pamoja.

Tatu anzisha utaratibu wa kutoka nae out, manenda matembezi mkiwa huko muanzishie story jinsi mlivyokuwa mnaishi mwanzo kwa amani na upendo na umweleze madadiliko yake at the end muombe abadilike. Yakishindikana haya, anza na wasimamizi wenu wa ndoa washirikishe nadhani wanaweza kuplay part kubwa ya kumbadilisha,wasimamizi wakishindwa basi ongea na wazazi, naamini hakuna kinachoshindikana atabadilika tu.

Na umatangulize Mungu katika kila hatua hope utarudi kwenye furaha yako ya mwanzo.
 
Kaka tulia na uvumilie ndivyo ndoa zilivyo. Ukisema umpige chini, utakwenda kwa yupi ambaye amekuwekea na anakusubiri????? labda uamue kuwa mseja.

Maoni yangu, hayo aliyoyafanya mbona madogo tu. Kuna makubwa wazee wazima tunayavumilia wala hatuthubutu kumwambia yeyote hata awe rafiki wa karibu au ndugu bali roho zetu ndizo zinayajua. Angalizo kwako, ukiwa mwepesi wa kuyatoa nje mambo ya ndoa hamtafika mbali.

Suala la kuwa na kidumu hilo usikatae wazoefu tunayajua, nasema wazoefu kwa maana kwamba ndoa yangu ina umri wa miaka 21 hilo la kuwa na kidumu nalo ni la kawaida ingawa vijana wa sasa ukisema ni la kawaida utaanzisha mjadala lkn sisi tunayaona ni ya kawaida ndiio maana tumefikisha umri wa miaka 21.

Uvumilivu na subira ni vitu muhimu kwani hayo atayafanya mpaka lini lazima itafikia hatua atabadilika
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Mh huyu nae kazidi kuchangia hachangii chochote bado na mafuta kwenye gari analotembelea mwenyewe umwekee, kaa chini zungumza nae kwa utaratibu na upole akueleze kinachomsibu baada ya hapo mweleze yako ya moyoni ,after hapo akishindwa kubadilika ndio basi tena huna cha kumfanya maana afanyalo mtu ndio aliloamua moyoni mwake huna namna mpaka amue mwenyewe.
 
Pole, inawezekana ana mimba changa inamsumbua mvumilie, Kikubwa ongea nae ! Ila kama siku hizi unahisi unamwogopa kuongea naye, rudi kwenu kawaambie wazee watajua cha kukusaidia.
 
M-bongotz

Kaka nakupa pole sana, wengine wanatafuta wanaume kama wewe yeye analeta gozigozi? Nafikiri ni wakati wako kumpa live ili kama anataka kuondoka aondoke. Mwambie huna hela ya fuel, wala lunch. Zaidi mtunze mwanao tu, nunua kila kinachomhusu halafu mruhusu atoke chumba cha pili aende kwa baba yake na mama waliomfundisha huo ujeuri.

Wnawake sisi tunapenda kukaribisha sana shetani. Ila kwa sababu ni mwanaume ebu jifanye mjinga sana, ukipepeleza nini kinaendelea. Kutakuwa na mtu kamdanganya, vijiwe vya kike huwa vina mambo mengi. Kama hujui kucheza na alama za nyakati unaishia kufanya *****.
 
Last edited by a moderator:
Kusema ile kweli, mimi wa kwangu alianza kama hivyo akataka kuwa yeye ndiye baba, nilijaribu kwa njia kibao za kidiplomasia kuweka mambo sawa ikawa ngumu. Bahati mbaya siku moja tu kichapo kikatembea mambo yakakaa sawa.

Sikushauri umchape lakini .......

Kichapo muhimu, sometimes huwa hatusikii mpaka yatukute. Mpe makofi ya kishikaji atatulia.
 
Acha kupotosha bana mali gani watagawana hapo na unasikia wanagawana elfu kumi asubuhi ya mafuta.......wanadaiana hela alotumiwa bibi kijijini....wanadiscuss mpaka diapers.......kun nini cha kugawana hapo?????

Hii ni ndoa changa inapitia changamoto za kawaida sana hapo wanavunja mayai ili kuoka keki so ni kuyavunja tu kwa idadi inayotakiwa ili kupata the best out of an oven tena mume ndo amshikishe mke awe mvunjaji mpaka wapate watakacho

Mkuu mtoa mada hii ni changamoto tu na atakuheshimu kama baba yake baada ya wewe kuweza kutuliza hiyo mawimbi sababu wenzetu hawa hupenda mwanaume strong na decissive.....sasa ukilega tu hapo the legacy will be hers

Komaa mkuu mtoa mada kama ni majukumu ulianza kwa mahari....nguo za harusi....kodi ya hapo mnapokaa (kama mmepanga) na hata wakati wa uchumba yawezekana Guest ulikuwa unalipa na gharama za kumrudisha kwao......gharama ni sehemu ya kuitwa baba ukikwepa hapo ndo utaitwa mzazi mwenzangu

Ntarudi bdae
kazi kwelikweli ngoja niendelee kusoma
 
Atleast nimejua kuwa siko peke yangu.,unachokisema ni kweli mkuu, lili fumbo la "wawili watakuwa mwili mmoja" huwa linaishia pale pale kanisani.

usiwe na mawazo ya kijinga...

ule mwili mmoja huwa hauji pale padre anapotamka maneno hayo!! kuufikia mwili mmoja unapitia safari ndefu sana kuanzia kwenye uchumba huko na hukamilishwa miaka mingi mkiwa ndani ya ndoa.

kuufikia mwili mmoja si mchezo na kunahitaji moyo na rehema za Mungu...kwa kifupi ni kwamba wewe na mkeo mmeishi kama mahawara kwa mda kisha ukaamua kufunga ndoa...bahati mbaya ni kwamba tabia yake hujaifahamu '' vionjo vyake''...jibidiishe kuvifahamu

jiulize kwa nini mwanzo mlikuwa namnaweka mshahara mezani na kupangilia nini cha kufanya lakini leo mwnezako hanunui hata chumvi ?!! nini kimembadilisha hapo katikati?!! je ni kwa sababu sasa ana hati miliki ya ndoa? jiulize .kwa mda weote huo amekaa kwako na kujifanya mnyenyekevu na kutoa ushirikiano lakini mara baada ya ndoa tu akabidilika je ni ndoa ndio alikuwa anaitafuta?......ulitafakari kwa kina au na wewe ni sawa na maneno ya ya lucky dube katika wimbo wake wa ''iti is not easy''?

Ndoa si mchezo bwana hasa unapokuwa baba wa familia..juzi Dark City alileta uzi humu wa sifa za mwanaume hasa wa kiafrika...jaribu kuuipitia kaka..kuna mahali lazima uwe mwanaume kweli na maamumiz yaw magumu...

fatili kwa nini mkeo amebadilika kiasi hicho na kwa nini hatoi ushirikiano ndani ya familia....

mwisho ndoa huwa haivunjwi na watu toka nje bali huvunjwa na wanando wenyewe.....
 
M-bongotz

Hizi sarakasi ulizoelezea hapa ni exactly kama ilivyotokea kwangu. Wanaoeleza kuwa ana mwanamme mwingine wako sahihi kabisa. Yaani kwangu ilikuwa kama sinema. Vivi hivi unavyoelezea. Ila wa kwangu ha-drive. Angalia jambo jingine. Atakuwa karibu sana na simu yake kuliko alivyokuwa huko mwanzo (wa kwangu alikuwa hivyo).

Nilipofuatilia nilithibitisha alichosema Boss (kuwa ni kidumu tu).
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Mkuu. Bahati mbaya hatuwezi kupata upande wa pili wa shilingi. Kiufupi hayo mambo yapo katika ndoa. Mtu ambaye uliweka matumaini ukamwamini anapobadilika kwa kiwango cha namna hiyo inasikitisha sana.

Nakushauri jaribu kujifunza aina ya watu anaopenda kuwa nao (marafiki zake).Huenda hawa ndio wanaompotosha Mkeo kwa ushauri na inaonyesha mkeo akipata ushauri hachanganyi na akili zake.

Nakumbuka kuna Dada mmoja aliwahi mshauri My Wife kwamba kwanini ananionyesha mimi (Mumewe) pesa yote badala ya kuwa kuificha (kama akiba yake)>Hebu fikiria kama Mke wangu naye angekuwa ansiliza ushauri wa namna hii ingekuwaje?

Kaa chini na Mkeo mweleze jinsi unavyoumia kutokana na kubadilika kwake.. na kuanzia sasa mafuta ya kwenye gari na lunch atumie mshahara na posho yake wewe baki na majukumu ya familia. Kama takuwa ametingwa kabisa ndio aombe kwako. Haiwezekani iwe kazi kwake hata kwenda ATM wakati pesa ni ya kwako Bro, vinginevyo hata hayo maendeleo mliyofanya pamoja itabaki historia very soon.

Kuwa strong Mkuu na wakati mwingine kuwa MKALI KIDOGO.
 
Inaonekana kuna problem between the two of you.I think ungekaa naye chini mkazungumza openly juu ya concerns zako na yeye pia akatoa dukuduku lake la moyoni.
 
fanya uchunguzi acje akawa na kibwana!......pili:ucmpe hela uone atanuna mpaka atachoka mwenyewe!....tatu,fanya unayotakiwa kufanya km baba,mengine achana nayo,then kuwa busy na mambo yako,ucmuulize chochote,wala kugombana nae!uone km hata rudi kwny mstari!
 
nadhani anatamaa na kishapata walimu wanaomfundisha, kaa nae umweleze nyie ni kitu kimoja hivyo inabidi muwe na safari moja, pia muulize nini tatizo sikuhizi mbona pesa zake hazionekani zinapokwenda? kisha punguza kumpa pesa hata akinuna wacha anune, na hapo ndipo utajua tabia yake hasa au kama kuna kitu amekipanga akilini mwake...akizidi zaidi mpe kichapo kikali sio bora kichapo kichapo hasa kile cha kupiga magoti chini na kuomba msamaha, ikiwezekana hata ajikojolee kabisa. shenzi type.
 
Watu wengi sana wanapenda kutumia "kumbe siko peke yangu" kujipa moyo. Hata kama hauko peke yako does it change the situation? Nani amefanya survey ya ndoa za watu na kuja na matokeo kuwa wote wanaishi na matatizo kama uliyoeleza.

Shughulikia tatizo lako kwani hata kama mko mia bado hamsaidiani kupunguza matatizo. Tatizo liko pale pale...wote nyumba mnaiona chungu.

Kwa kukusaidia tu nachoona hapo wewe pia una tatizo...ilikuwaje akawa anabadilika taratibu taratibe na wewe ukawa unamwacha tuuu. Kwa nini unampa ela ya mafuta na yeye ana kazi yake? Usipompa hataenda kazini??? Au atakunyima??? Mnawaendekeza wenyewe...wakikomaa mnakuja kulalamika humu..
 
Back
Top Bottom