Wi-Fi 7; mfumo Mpya wa wireless

Wi-Fi 7; mfumo Mpya wa wireless

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,027
Reaction score
20,414
Mwaka huu, mfumo mpya wa Wireless wa Wi-Fi 7 utaanza kuchukua nafasi na wiki hii kampuni nyingi zimetangaza zitaanza kutengeneza vifaa na chip ambazo zitakuwa zinakubali mfumo mpya wa Wi-Fi 7 ikiwemo kampuni ya Qualcomm.

Kwa sasa dunia ipo katika WiFi 6 na WiFi 6E; ila tayari WiFi inaanza kuingia sokoni na itakuwa na uwezo mkubwa kuliko mifumo ya Wireless ya zamani.

Katika upande wa Mabadiliko, WiFi 7 itakuwa na sifa zifuatazo:

1️⃣ WiFi 7 itakuwa inafanya kazi katika masafa ya 2.4GHz, 5GHz, na 6GHz bands kama WiFi 6E.

2️⃣ Itakuwa na speed ya 30GB kwa sekunde, ambapo ni speed kubwa kuliko speed ya 9.6GB ya WiFi 6.

3️⃣ Itakuwa na performance kubwa kwa sababu itakuwa inatumia channel bandwidth ya 320MHz mpaka160MHz.

Mfumo mpya wa Wireless unakubali hata vifaa vya zamani hivyo bado inaweza kufanya kazi na kuboresha speed ya vifaa vingi ambavyo vinatumika sasa.
 
Mwaka huu, mfumo mpya wa Wireless wa Wi-Fi 7 utaanza kuchukua nafasi na wiki hii kampuni nyingi zimetangaza zitaanza kutengeneza vifaa na chip ambazo zitakuwa zinakubali mfumo mpya wa Wi-Fi 7 ikiwemo kampuni ya Qualcomm...
Patents zipo kwa nani zaidi maana 5G tumeona Huawei anamiliki shea kubwa..
 
Patents zipo kwa nani zaidi maana 5G tumeona Huawei anamiliki shea kubwa..
5Ghz wireless inayozungumziwa hapo ni tofauti na 5G network unayoizungumzia wewe
tupo pamoja mkuu !!?

5Ghz wireless ipo kabla hata 5Gnetwort haijulikani kama itakuja lini
5Ghz wireless inabeba hata 2g network
na mambo mukide tuu

halafu INTERNET inakuja na CABLE kutoka ULAYA mpk BONGODASLAAM na Sio kutoka kwenye SATELLITE kama wengi wanavyodhani

haya mambo ya TEKELINALOKUJIA yanachanganya mno yaan sana ukiyafikiria kwa kina utakubaliana na mimi kuna VIUMBE toka SAYARI nyingine wenye maarifa mno tunashilikiana nao kuijenga hii DUNIA mana sio mchezo aiseee
qgixBot4C6EnTOlE.jpg
HDbdRlZFYmna5tZs.jpg
Subpost%202%20-%20Share%20this%20post%20with%20your%20friends_two_men_holding_hands_%20.%20.%2...jpg
Subpost%206%20-%20Share%20this%20post%20with%20your%20friends_two_men_holding_hands_%20.%20.%2...jpg


Sent from my SM-G935S using JamiiForums mobile app
 
Munaonaje tuungane kwa pamoja ku2mia wifi na kuachana na vifurushi vya simu!!!
Wifi inapitisha tu data hio data inaweza kuwa ya Mtandao wa simu, dsl, Fiber, Satelite etc. Yenyewe kama yenyewe haina Bando ndani.

Kwa wenzetu ulaya na hata hapa kwetu Wifi hutumika kupunguza waya, Mfano una movie kwenye laptop unataka kuplay kwenye tv no need ku connect chochote ama kuhamisha na flash unaweza play movie yako toka laptop hadi tv ikiwa vyote vina wifi. Wifi hutumika kustream games, na media nyengine vyote hivi bila internet.
 
wi-fi kifamilia wanamuita wizo, causin anaitwa cuzo, so katika kustaajabu speed ya gb 60 kwa sekunde mbili, ikabidi nijisemee tu wizo kama wizo niki refer wi-fi kama wi-fi.
Duh watu mpo faster kufikiria dah
 
Back
Top Bottom